Simulizi ya ukweli penzi langu

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2022
22,548
42,354
SIMULIZI: PENZI LANGU


SEHEMU YA 01





ANZA ...Mkoani Tabora walionekana watu wawili ambapo Kwa kuwatazama tu ni kama vile walikua wapenzi ambao wamuda mrefu sana wakati huo mwanamke alikua ameshika kimfuko kidogo huku mwanaume akiwa ameshika mkono wake wakiwa wanatembea hadi walipofika kwenye kituo cha treni mwanamke akazungumza.





"Suma naomba sana usinisahau sababu nakupenda sana na nakutegemea wewe Suma kumbuka wewe na mama yako ndio familia yangu kwasasa na kumbuka wapi umenitoa Suma nakupenda sana"





"Aisha usijali nakuahidi kua kidogo chochote nitakachokipata nitawatumia sababu sitaki mpate shida we na mama yangu kumbuka kua naenda mjini ni vile nahitaji kubadilisha maisha yetu sababu sitaki tubaki kuwa wakulima wadogo naenda kutafuta ili tuweze kuwa wakubwa zaidi na wenye kutumia pembejeo za kisasa mpenzi"





"Nakuamini sana na kama alivyokupa baraka mama yako na mimi pia nakupa baraka zangu"





Aisha alikua anahuzuni sana kuagana na mpenzi wake ambae alikua anampenda sana na kumheshimu Kwa kiasi kikubwa.





Haukupita muda mrefu mara treni ambayo alitakiwa apande ilifika na Suma alipanda kwenye treni akakaa kwenye siti huku akimpungia mkono mpenzi wake Aisha.





Na watu wengine walipanda pia kisha treni ikaanza safari yake kuelekea dar es salaam.





Aisha alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake na Suma akiwa amekaa kinyonge Aisha akamsogelea mama yake Suma na kumwambia.





"Mama usijisikie vibaya naamini kua anatupenda sana hawezi kutuacha wenyewe hata kidogo naomba tuweke Imani kwenye hilo sababu tukiwa na mawazo mabaya itamuwia vigumu hata kwa upande wake"





"Nakuelewa sana Aisha usijali mimi nipo sawa kabisa na nitafurahia sana endapo nitamuona kijana wangu Suma amerudi salama na kuja kufunga ndoa na wewe mwanangu mpole mwenye heshima"





"Asante mama ila wacha niandae chakula halafu niende shambani nikamalizie kupalilia shamba"





Basi Aisha alifanya hivyo na kisha akaondoka kuelekea shambani na kumuacha mama Suma nyumbani sababu alikua mgonjwa wa miguu hivyo alikua anapata shida sana kwenye kutembea.





Wakati Aisha anaelekea shambani mara Ghafla akakutana na mwanaume mmoja ambae alionekana kua na maongezi na yeye Aisha alipomkaribia tu kabla ya huyo kijana kuzungumza akamwambia.





"Joel naomba tafadhali niache nipite sitaki usumbufu wa aina yoyote maana ukiendelea kunifata fata nitakuja kukufanya kitu kibaya sana"





"Hahaha Aisha unaonekana kuwa na msimamo sana lakini safari hii nimekuja mwenyewe ila siku ambayo nitakuja tena nitakuja na wenzangu najua kiherehere chako kitakuisha"





"Huwezi kunitisha kwa chochote kile na ukijifanya mjuaji na mimi nitakukomesha"





Aisha alimsukuma Joel na kuondoka zake, Joel alimshangaa sana na kujiuliza


"Huyu mwanamke anajiamini nini na mbona mpenzi wake ambae alikua anamtetea ameshaondoka kwanini bado anajiamini kiasi hiki lakini pia yupo tofauti na wasichana wa hapa kijijini labda ndio maana anajiamini sana maana wasichana wa hapa ukimuonesha hata elfu moja tayari washakubali unaipata show yako moja kisha unatulia ila huyu sasa ni mgumu sana ila nitamkomesha siishii hapa"





Joel aliondoka zake.





Muda ulizidi kwenda hatimae jioni iliwadia Aisha alitoka shambani akiwa na mizigo yake na moja kwa moja hadi kwa mwenyekiti akamsalimia na kumwambia.





"Samahani mwenye kiti ninashida nataka nikuambie"





Mwenyekiti na yeye alikua anamtamani sana Aisha kwa muda mrefu sana lakini Aisha alikua na msimamo sana hapo kijijini sababu alikua anampenda sana na kumuheshimu Suma kutokana na jinsi alivyompata na kumsadia, hivyo mwenyekiti kabla Aisha hajasema shida yake akamwambia.





"Aisha kwanza vipi kuhusu nilichokuambia sababu mpenzi wako ameshondoka tayari"





"Mwenyekiti sikuja hapa kwaajili ya kujadili hayo mambo nataka unisaidie kuna vijana wananisumbua na wamepanga kunifanyia kitendo kibaya muda wowote ambao nitakua peke yangu nikienda shambani au kisimani pia"





"Ooh jamani usijali kuhusu hilo Aisha mpenzi nitashughulikia wala usiwe na wasiwasi"

Aisha alisimama na kuondoka zake huku akimuacha mwenyekiti amejawa na tamaa za kimwili na yeye, Aisha alipoondoka mwenyekiti akasema.


"Yani huyu mtoto kila nikikutana nae lazima tu niwe na mshawasha hivi ananini lakini? ila mh mtoto mashallah anavutia kila idara kwanza mweupe ana shape nzuri yaani dah natamani ile siku ningemuokoa mimi lakini ningewezaje sasa wakati nguvu ya kumtoa nilikua sina, ila ananichanganya sana huyu binti lazima nimpate"





Aisha alirudi nyumbani kwao na kumkuta mama yake mkwe anapika Aisha akamuuliza.





"Mama kwanini unapika si nitapika mimi jamani?"





"Aisha unafanya kazi nyingi hadi nakuonea huruma ona sasa hivi ulivyokonda wakati haukua hivi, Aisha kumbuka kua wewe hukutakiwa kuishi maisha ya shida ila sema ndio hivyo hatuna uwezo"





"Mama mimi najiona heri ya umaskini wenye furaha kuliko utajiri wenye kuishi kwa wasiwasi na tangu nifike hapa kwako nimekua na amani sana na furaha hivyo usijali mama"





"Kweli unafuraha ukiwa kwenye Maisha haya?"





"Zaidi ya sana mama na Wala usiwe na wasiwasi kuhusu Mimi"





Basi Aisha alisogea kibandani na kuendelea na mapishi ambayo aliyaanza mama yake na Suma.





Upande wa kwenye treni Suma alikua anawaza tu endapo atafika huko mjini ataishi wapi sababu hana ndugu Wala jamaa hio kitu ilikua inamuwazisha sana akilini mwake.





Baada ya siku tatu walifika jijini dar walishuka kituoni na kila mmoja kuingilia sehemu anayoijua yeye.





Upande wa Suma alikua hajui mitaa Wala hakua anajua wapi anaelekea alichojua yeye amefika Dar basi Kambi yake itakua popote ambapo ataona patamfaa.





Alitembea sana siku hivyo hadi inafika majira ya jioni, akiwa zake maeneo ya kwenye soko la tandale mara ilikuja gari ambayo ilikua imepata hitilafu kidogo na dereva alishuka kwenye gari mara Moja na kutaka kutazama shida Nini akawa haelewi Nini afanye mara akageuka geuka na kumuona Suma akiwa amekaa kinyonge akamuita.





"Oya we kijana njoo mara Moja"


Suma alisimama haraka na kusogea pale kisha akaambiwa.





"Em niangalizie hapa mana sielewi hata"





Kwakua Suma alishajifunza funza kijijini kwao jinsi ya kutengeneza magari pikipiki na baiskeli hivyo haikumuwea vigumu kugundua tatizo la kwenye hiyo gari, akatengeneza fasta na kumwambia.





"Jaribu kuwasha gari"





Mwenye gari alifanya hivyo na mara hii gari ikawaka safi kabisa Suma hakutaka kuwa na pupa alifunga pale palipofunguliwa kisha akasogea pembeni na yule jamaa alikua anaongea na simu na baada ya kumaliza akamuita tena Suma alisogea na kisha akamwambia.





"Shika hii pesa itakusaidia pia Asante Kwa kunitengenezea gari yangu"





"Kaka asante pia ila Mimi sitaki pesa nataka unisaidie kazi na sehemu ya kulala"





"Ioh kumbe hauna makazi?"





"Ndio kaka mie ni mgeni hapa ndio nimefika leo tu kutoka Tabora"





"Oh panda kwenye gari tuondoke"


Suma alikimbilia mfuko wake na kisha kurudi Kisha akapanda kwenye gari na kuondoka na huyo jamaa.





Gari iliendeshwa Hadi kwenye maeneo ya kinondoni kisha gari ikapaki kwenye nyumba moja hivi Kisha akamwambia.





"Hapa ndio napoishi karibu ndani"





"Asante sana kaka"


waliingia ndani na kisha wakapata chakula pamoja Kisha akamuonesha sehemu ya kuogea kisha akampa shuka akalala seblen na yeye akaingia chumbani kwake.





Suma alimshukuru sana na kusema.


"Asante mama kwa Dua zako Mungu amejibu maombi yenu Kwa siku ya kwanza napata msamaria mwema wa kunisaidia, wengi naskia wanapata shida sana kuhusu sehemu za kulala ila Mimi Leo nalala ndani Asante saña Mungu wangu"





Suma alilala pale seblen Hadi asubuhi mapema, aliamka na kuanza kupanga vitu vizuri mara ghafla mlango wa chumba ukafunguliwa na akatoka yule jamaa na mke wake akimuweka vizuri tai na kumchana nywele Kisha akazungumza.





"Dogo huyu ni mke wangu jana sikukutambulisha sababu alikua amelala hivyo huyu mke wangu na pia mama watoto huyu ni yule kijana ambae nilikuambia hivyo atakaa hapa huku nikimfanyia mchakato wa kazi na sehemu ya kuishi"





"Sawa mme wangu, karibu sana shemeji"





"Asante sana"


basi walitoka nje na kumwambia.





"Dogo sikia wacha Mimi niende kazini halafu kuna sehemu pale nitakuangalizia kisha kesho utaanza kazi au hata leo nitamtuma mtu akufate"


"Sawa kaka hakuna shida"

yule jamaa aliondoka na kumwacha Suma na mke wake.



Upande wa kijijini sasa Aisha aliamka kama kawaida yake na kuelekea shambani lakini akiwa njiani simu iliita na kuanza kuzungumza na hakua mwingine alikua Suma alifurahi sana kumsikia na baada ya kumuulizia mama yake akamwambia kua yupo shamba na muda ambao atarudi atamwambia ili ampigie ukweli siku hiyo ilikua ya furaha sana kwa Aisha na aliwahi kufika mapema sana shambani na kuanza kulima lakini ghafla walitokea vijana watatu na kumbeba Aisha mpaka mafichoni kwa ajili ya kutaka kumbaka wakati wawili wanafanya doria kwaajili ya watu ambao watakaokua wanapita hapo.



Kwenye harakati za kutaka kumbaka Aisha mara Ghafla walifika vijana wengine wanne walionekana kuwa na nguvu sana kisha wakasikia sauti ikizungumza.



"Vijana mnajifanya wanaume ambao mnajali sana hisia zenu kuliko utu wa mtu sio? Sasa basi leo nitawafundisha jinsi ya kuishi na watu vizuri, vijana shika hao waadhibiwe haraka"



Wale vijana wanne waliwakamata Joel na wenzie walipigwa sana na wakachomwa moto kabisa, kisha mwenyekiti akamwambia Aisha.



"Umeona nimeamua kuwateketeza Kwa namna ile ya kukutoa wasiwasi mpenzi na yeyote ambae atakusumbua basi niambie mapema nitamshughulikia, lakini sasa naweza kupata penzi lako?"



"Lakini sio leo mwenyekiti sababu nipo kwenye siku zangu naomba nivumilie kidogo"



"Ooh kumbee sawa Binti ukiwa tayari utaniambia maana nina hamu sana ya kuwa na wewe faragha maana kila nikikutazama yaani napandwa na hisia sana angalia kwanza mtoto una kiuno kizuri macho yako yanavutia sana urembo wako rangi yako ndio umezidi kuniteka mwenzio"



"Basi mwenyekiti inatosha wacha nirudi nyumbani Sasa"



Mwenyekiti alimruhuau Aisha alirudi nyumbani kwao lakini moyoni alikua anawaza sana jinsi ya kumuepuka mwenyekiti huyo maana tayari ameshaanza mazowea ya kijinga kwake na ukizingatia yeye na Suma tayari wamekula kiapo cha kutosalitiana Maisha Yao yote.



Alipofika nyumbani kwao aliondoa sura ya huzuni na kuiweka sura ya furaha ili mama yake na Suma asigundue chochote haraka alimsalimia kisha akamwambia.



"Mama Suma alinipigia wakati naenda shambani amefurahi sana hata Mimi nimefurahi kuongea nae na pia alisema anataka kuongea na wewe"



Mama yake pia baada ya kusikia hivyo alifurahi sana na kumwambia.

"Mpigie nimeshammisi mwanangu jamani"



Aisha alitafuta ile namba ambayo ilimpigia lakini alipokea mwanamke na kumwambia kua hakuna mtu yoyote ambae alimpigia kifupi aliwajibu vibaya sana kiasi kwamba Aisha alihisi huenda Suma amepata mwanamke mama yake akamwambia.



"Aisha usijali labda Suma aliazima tu simu kwa mtu usimfikirie vibaya najua umejitahidi sana kumuelezea lakini amekua mgumu kuelewa najua na Nina imaani kua Suma atapiga Tena."



Upande wa dar Suma alikua kachukuliwa na kijana wa boda boda na kupelekwa sehemu ambayo aliagizwa na baada ya kufika akamwambia.



"Dogi hapa ndipo utakapokua unafanya kazi changamka usiwe na unyonge ikija gari msaidiane ili mpate pesa sawa"



"Asante sana kaka"



"Poa badae basi"

yule jamaa aliondoka na kumwachia Suma akiwa na wenzake wanapiga story.

Kwa muda mfupi tu Suma alikubalika Kwa story zake na Kwa muonekano tu alionekana kua na mipango na akili nyingi sana.



Mmoja akamwambia

"Kwahiyo Suma we mtu wa wapi?"



"Mimi mtu wa Tabora na nimetoka huko nyumbani nimeacha mama na mwanamke ambae ananipenda sana"



wenzake wakamtazama na mmoja akasema

"We ndio hujielewi yani kwa sifa ulizotoa kuhusu mwanamke wako huwezi kumkuta kama ulivyomuacha broo yaani hapo ukipata demu wa huku pita nae usawazishe mana huwezi kubaki na ugumu siku zote eti hadi upate pesa ya watu wako kuja mjini wakati huku mademu wapo wengi tu, ona sisi tupo hapa mwaka wa pili sasa lakini hatuna chochote mpaka sasa hivi halafu wewe unakuja kutuletea umama hapa"



ITAENDELEA.......



Yajayo yanafurahisha, wakati Aisha yupo na misimamo yake, huku Suma ameshaanza kupewa mawazo potofu. Je! Itakuaje? Jina la simulizi ni PENZI LANGU Je! Limefanya nini? 🤷🏻‍♂️
 
Well if you give me 10 bitches then I'll https://jamii.app/JFUserGuide all 10
Seen the homie Snoop Doggy sipping juice and gin
Don't slip, I'm for the set-trip, to get papers
Styles vary, packing flavor like Lifesavers
Ain't that something?
Talk shit and I'm dumping
I had the fuckin' whole block bumpin'
Don't sweat, but check the technique. I'm unique like China
 
SIMULIZI: PENZI LANGU


SEHEMU YA 02





ILIPOISHIA.......





"We ndio hujielewi yani kwa sifa ulizotoa kuhusu mwanamke wako huwezi kumkuta kama ulivyomuacha broo yaani hapo ukipata demu wa huku pita nae usawazishe mana huwezi kubaki na ugumu siku zote eti hadi upate pesa ya watu wako kuja mjini wakati huku mademu wapo wengi tu, ona sisi tupo hapa mwaka wa pili sasa lakini hatuna chochote mpaka sasa hivi halafu wewe unakuja kutuletea umama hapa"





ENDELEA NAYO.......





"Sikia ndugu zangu mimi nimekuja mjini Kwa malengo maalum na sijakurupuka na Kila nitakachokipata tayari nina mpango nacho kama mmekuja kwaajili ya wanawake sjui nanini me sipo hivyo"





Wakati wanaendelea kupiga story ilifika gari Moja nzuri sana wote walisogea karibu kutaka kuiwahi kuiosha lakini mlango wa gari ulifunguliwa na kushuka mwanamke mwenye shape nzuri sana amependeza sana sana, urembo wake shepu yake vilibebwa na rangi yake pia, alifunga mlango wa gari na kuzungumza.





"Washkaji zangu nani alinioshea gari yangu? Maana sina kawaida ya kuosha gari Kila siku lakini ona leo nimekuja tena"





Kila mtu alikua anajikataa yule mdada kasema


"Yule mbona kajitenga ni mwenzenu au?"





"Ndio boss ni mwenzetu lakini mgeni hajazoea mazingira na ndio kwanza kafika leo"





"Anhaa ohk anaitwa nani?"





"Sumaa njoo hapa"


mmoja akamuita. Suma alisimama na kupiga hatua Hadi pale alipo, yule mwanamke akampa mkono Kwa kumsalimia.





"Habari yako Suma?"





"Safi tu karibu"





"Asante mbona ulikua umekaa kule wakati wenzio wanachangamka?"





"Aah nilikua nasubiri muelewane ndio nije kusaidia"





"Anhaa ohk sasa washkaji sikia leo nipo mwenyewe hapa siondoki na gari yangu namkabidhi Suma alioshe akinizingua kama mlivyozingua jana nitaondoka na sitarudi tena kuosha gari hapa"





"Hapana madam boss usiseme hivyo"





"Sawa basi Suma fanya hivyo"





Kisha akatoa pochi na kuwapa hela ya chakula kisha akaingia kwenye gari na kuwasha mziki kisha akasogea kivulini kwa ajili ya kusubiri gari yake.





Suma alijitahidi sana kuiosha gari kwa umakini sana Kisha akasogea Kwa huyo mdada na kumwambia.





"Madam boss gari iko tayari"


huyo mwanamke alisimama na kusogea karibu na gari na baada ya kuchunguza akaona utofauti mkubwa sana akampatia elfu20 Kisha akamwambia.





"Hii pesa ya kwako usimuoneshe mtu yoyote na hii elfu 20 nyengine mtagawana elfu5 kila mtu"





"Asante sana"





Suma alisogea kwa wenzake na kuwapa kila mmoja Tano Tano lake, madam boss wao aliondoka na kuwaacha wakiendelea na story zao Juma akamuuliza Suma.





"Kwahiyo unaweza kutuambia huyo mwanamke ulivyompata? Maana umesema wewe ni domo zege mbele ya msichana huyo mwanamke ulimpataje?"





"Ni story ndefu sana ila wacha nifupishe tu ilikua hivi Mimi na mama yangu tulilikua tunarudi shambani majira ya sa11 jioni sasa tulifika sehemu Moja hivi ya msituni kulikua kunawaka moto halafu pia kulikua na sauti ikisikika kuomba msaada na niliposogea nikasikia kabisa inaomba msaada sana lakini watu waliokuwepo hadi mwenyekiti alikua anasua kutoa msaada basi nikamuomba mama anipe baraka zake na bila ya kuchelewa nikazama msituni moto ukiwa mkali sana lakini sikujali chochote nikamkuta huyo mwanamke amefungwa kamba tena akiwa na midamu mingi kutokana na kipigo nikamfungua na kumbeba na kutoka nae ukweli nilikua nimechoka sana kutokana na kukosa kupumua vizuri kutokana na Moshi lakini yule dada tayari alishazimia sababu ya kuwa ndani ya moto kwa muda kidogo basi nikamlaza chini watu wakiwa wamenijalia pale na Kwa bahati hua tukitoka shambani tunapitia mtoni kubeba Maji hivyo nilichukua ndoo ya Maji na kujimwagia Mimi na yule msichana ili joto lipungue mwlili mwake pia na Mungu alitusaidia na muda mchache tu aliweza kuamka.





Na mwenyekiti akanikabidhi Mimi yule mwanamke huku akisema kua atafanya uchunguzi ajue chanzo cha msichana huyo kuwepo pale.





Basi niliondoka na yule dada Hadi nyumbani nikaanza kumuhudumia Kwa dawa na Kila kitu na baada ya kumuulizia juu ya kilichotokea akanisimulia Kila kitu na kuomba kuishi pale na sisi mama hakupinga na Mimi pia sikua na sababu ya kukataa.

Basi baada ya siku chache nikaona mabadiliko maana msichana yule alianza kunishika shemu tofauti za mwili wangu na mwisho akaniambia kua ananipenda na vile sikua na mahusiano na wasichana wa pale kijinini basi ikawa fursa kwangu ukweli tulikua na furaha sana hasa baada ya kuweka huru mapenzi yetu wengi waliona wivu sababu nikianza kutakaka Kwa penzi lake moto.





Na yeye ndio alienishauri nije kutafuta Maisha huku kwaajili ya Maisha yetu ya baadae"





Juma akasema


"Nyie huyu Suma anaonekana ni muongo sana hivi nyie hii movie hamjawahi kuiona kabisa?"





Wote walicheka Kisha mwingine akasema.


"Juma sio Kila kitu ni movie mbina yanatokea hayo mambo?"





"Aah Ramso sio Kwa Suma bwana huyu bwana anaonekana kabisa ni muongo"





Suma akamwambia


"Kama unahisi ni uongo sawa lakini siku Moja utakuja kuamini kile nachokuambia"





Suma alisimama na kuwaambia


"Muda umeenda Wacha niondoke"





"kwahiyo Suma unaondoka sa12 hii wakati muda Bado kabisa kuna magari ambayo hujaga usiku wewe"





"Hapana Kwa leo nimepata hii pesa itanisaidia Kwa kesho Wacha tu niende"





Suma aliondoka eneo lile na baada ya kufika mbele kidogo akasogea kibandani na kuomba kupiga simu aliweka namba na kupiga simu Kisha wakaongea sana na vipenzi vyake na Kisha akawatumia ile elfu 20 Kisha akaagana nao.





kutoka hapo Hadi sehemu aliyosaidiwa ni mbali sana na ilikua usiku wa Saa Moja Suma hakuweza kutambua njia ili apite ili aweze kufika kwenye hiyo nyumba ukweli ilikua inamchanganya sana akaamua tu kurudi ambapo ametoka na kabla hajafika popote wahini walimvamia na kumpora elfu5 ambayo alibakiwa nayo siku hivyo ilikua ya uchungu sana kwake lakini akajisemea.





"Asante Mungu sababu Nina furaha kua nilichokipanga Kwa familia yangu nimetimiza na pesa iliyobakia nimeibiwa sawa lakini Mimi mwanaume nitavumilia tu na mengine yataendelea.





Suma alipiga hatua kurudi pale wanapooshea magari na kutafuta sehemu nzuri na kujihifadhi.





Usiku mzima kwa upande wa Suma ulikua wa mateso kwasababu ya baridi kali sana na mbu walimshambulia sana hadi inafika asubuhi.





Kwa upande wa yule jamaa ambae alimsaidia alipoamka asubuhi akawa anajiandaa kwaajili ya kuelekea kazini alivyotoka sebleni hakumuona Suma akamuulizia mke wake.





"Ina maana yule dogo hajarudi Jana?"





"Mie nimesubiri sana arudi lakini sijamuona"





"Mmh nawasiwasi sana kuhusu yeye na hii inawezekanaje?"





"Hata mie sielewi mume wangu"





"Sawa Wacha nijaribu kupitia pale nilipompeleka kwanza nitakupa taarifa"





Basi waliagana na mke wake na kisha kuondoka zake.





Alipofika kwenye eneo husika alimuona mtu kwa mbali akiwa amelala na ilikua muda ya sa12 asubuhi,alishuka kwenye gari na kumpiga hatua hadi pale na kumuuliza.





"We Suma mbona umelala hapa shida Nini?"





"Aah kaka za asubuhi?"





"Nataka kujua mbona umelala hapa wakati nimekukaribisha kwangu au mke wangu amekuambia kitu chochote kibayaa?"





"Hapana kaka ila tu nilipotea na sikujua wapi kwa kupitia na pia sina simu nikaamua nirudi kulala hapa maana hata wenzangu sikuwakuta"





"Dah pole sana dogo vipi utafanya kazi au utaelekea kupumzika maana hapo ulipolala sidhani kama utakua sawa kutwa ya Leo"





"Usijali kaka Mimi nipo Sawa kabisa nitafanya kazi"





"Poa basi jioni nitakupitia turudi nyumbani wote"





"Asante kaka"





Yule jamaa aliondoka na kumwacha Suma akiwa bado kile kibaridi kinamtetemesha kidogo, alisogea kwenye benchi na kukaa huku akiwaza sana mbele yake itakuaje na tayari amewakumbuka sana mama yake na Aisha mpenzi wake.





Mara Juma na Rama walifika na kumsalimia Suma aliitikia na kuwakaribisha na story ili wasigundue chochote kuhusu yeye, aliogopa kuchekwa na hawakusubiria sana mara mwenzao mwingine alifika na kuendelea kupiga story.





Upande wa kijijini kwao taarifa za vijana watatu kuchomwa moto ilifika kituo cha polisi na baada ya kuhoji chanzo Aisha yeye alikua msemaji hivyo akaona ni fursa ya kumuweka mbali mwenyekiti hivyo alielezea kila alichokiona hadi sababu kuu ya kufanya hivyo na mwenyekiti alifungwa kwa kosa la kujichukulia sheria mkononi maana hao vijana hawakupaswa kufa ila walipaswa kupewa adhabu ili wajifunze na kupewa nafasi ya pili lakini yeye hakutaka kuwaonya wala

kuwapa nafasi hivyo kwa ushahidi tosha wa Aisha ulimfanya mwenyekiti kuvuliwa cheo chake na kutumikia kifungo kwa kosa la mauwaji.





Mama yake Suma akamuuliza.


"Aisha mbona hukuwahi kuniambia kuhusu tatizo hilo huoni ni jambo kubwa na umenificha muda wote huo?"





"Mama kumbuka haupo sawa kiafya lakini pia najua kuwa ningekua nakuambia kila kibaya nachopitia ningekua nakuchosha Kwa mawazo mengi Huku umuwaze Suma huku uniwaze mimi ukweli sikutaka uwe kwenye wakati mgumu mama"





"Lakini Aisha...!!"





"Mama usijali Mimi ni mtu mzima naweza kujimudu na isitoshe Kuna jambo nataka kukwambia nahisi utakubaliana na mimi"





"Jambo Gani Tena mara hii tu tayari ushataka kunibadilishia mada?"





"Hapana mama sio hivyo lakini nataka tu kukushirikisha, siwezi fanya maamuzi bila kukuambia wewe"





"Sawa mwanangu niambie tu Wala hata usijali"





"Mama nimeona kuwa sasa ni muda sahihi wa Mimi kurudi mjini mama Tena sio mimi tu na wewe pia siwezi kukuacha hapa"





"Unamaanisha nini, na unataka kwenda kufanya Nini wakati ulisema kuwa unawindwa?"





"Nikweli mama lakini nimeongea na mwanasheria wa baba amenipa taarifa kuwa wote waliofanya kitendo cha kikatili kwa wazazi wangu na pia walifanya kwenye familia nyingine, walishashtukiwa na Sasa wapo kwenye mikono ya sheria"





"Mimi naogopa sana kwenda huko mjini Aisha bora niishi hapa Kwa amani kama ilivyokua unasemaga mwanzo mwenyewe"





"Nikweli mama na ninajua fika kuwa adui huwa wengi sana lakini sioni sababu tena ya kujificha sababu Sasa hivi Nina nguvu kutokana na Nina family ambayo inanipenda sana"





"Hapana Aisha siwezi kwenda naogopa kufa kabla ya kuona mjukuu wangu na nyie mkiwa kwenye sura mpya ya ndoa"





Aisha aliendelea kumbembeleza mama yake Suma ili waende mjini lakini bado mama yake Suma hakua mrahisi kihivyo, hivyo ikabidi amuache afikirie na akiwa tayari atamwambia lakini Aisha tayari akili yake ilishakumbuka mjini na kutamani kuyaona makaburi ya wazazi wake.





Upande wa mjini siku nzima walifanya kazi kama kawaida Yao lakini Suma hakua vizuri kuna hali flani ambayo alikua anajihisi Kwa muda lakini inakuja na kupotea kitu ambacho Juma kilimfanya amuulize.





"Vipi mzee wa bongo movie uko Sawa kweli?"





"Hii Juma inamaana ushampa jina mwenzio?"





"Rama we huoni kama Suma ni muongo sana?"





"Aah we Juma ukianza kubishana humalizi ngoja tu niendelee na kazi yangu"





Rama aliwaacha kisha Juma akamuuliza tena Suma na safari hii hakua ameleta Tena utani.





"Suma naona kama haupo Sawa leo unatatizo Gani?"





"Aah Juma siko Sawa kabisa Yani ila naamini kua nitakua Sawa"





"Pole sana kijana utakua Sawa"


basi walisaidiana kufanya kazi zao maana siku hiyo ilikua ya neema sana kwa upande wao maana magari yalikua yanasubiria foleni ya kuoshwa hivyo wote walifanya kazi kwa kujituma na bidii ya hali ya juu sana.





Mpaka inatimu jioni wote walikua wamechoka sana na kabla hawajapumzika vizuri ilikuja gari nyingine kwaajili ya kutaka kuoshwa pia Suma akawambia.





"Kama mmechoka Wacha Mimi nioshe kisha tuondoka au mnaonaje?"





"Suma bwana Wacha iende tu hiyo gari maana kama unataka kuiosha Sawa ila sisi tunaondoka"





Wale watatu wakaondoka na kumwacha Suma pekee, Suma alianza kuiosha ile gari huku akisubiri kuja kufatwa na kaka yake hadi anamalizia kusafisha gari bado kaka yake alikua hajafika.





Suma alikua anatamani sana kwenda kupiga simu kibandani ila alihisi akitoka tu pale ataibiwa hivyo alikua mtulivu sana pale pale hadi inafika saa mbili usiku bado huyo kaka yake hajafika.





Ukweli ilikua inamuumiza sana kuzidi kuwaza kwanza mitaa haijui na simu Hana alikua na subra pale pale.





Mara Ghafla ilipita gari kwa kasi lakini Ghafla ilirudi na kupiga honi Suma aligeuka na kuhisi kua huenda ni kaka yake hivyo alisogea haraka eneo liliposimama gari lakini alipofika akamuona mwanamke akamsalimia vizuri yule mwanamke akashuka kwenye gari na kumuuliza.





"Nafikiri kama sijakosea wewe ni Suma?"





"Aah ndio ni Mimi umenijuaje?"





Yule mwanamke alitoa miwani na kumwambia.


"Nilikuja jana ukanioshea gari yangu"





"Ooh madam boss..!!, sikuweza kutambua kama ni wewe kutokana na gari hii sio ile ambayo umekuja nayo jana"

"Ndio lakini Mimi naitwa Nadya sio madam boss sababu hilo jina hawa vijana ndio hupenda kuniita ila sio jina langu"



"Anhaa sawa pia ni vizuri sababu kwanza linakupendeza sana"



"Anhaa Asante pia lakini mbona uko mwenyewe wenzako wameenda wapi?"



"Wao wameondoka lakini Mimi...."



"Suma haupo na sehemu ya kuishi sindio?"



Suma kama vile alipatwa na kigugumizi flani.



"Aah mi, ni ...aah"



"Suma usijali sawa ingia kwenye gari twende"

Suma aliangaza huku na huko kisha akapanda kwenye gari ya Nadya kisha Nadya aliwasha mziki na kuondoka maeneo yale hadi nyumbani kwake.



Baada ya kufika nyumbani kwa Nadya, Suma hakuacha kushangazwa na uzuri wa nyumba ambayo anaishi Nadya na magari yalivyojipanga kwenye parking utafikiria kua ni ya watu au wafanyakazi wa kampuni husika, Suma alishindwa kuvumilia akamuuliza.



"Inamaana Kila kitu unamiliki wewe madam boss?"



Nadya alimgeukia Suma na kumshika mabegani na kumwambia.

"Naitwa Nadya sitaki hilo jina, haya twende ndani"



Suma ilimbidi afunge Domo lake Huku aliendelea kushangazwa na uzuri wa bustani na mazingira ya ile nyumba.



Upande wa yule jamaa alirudi nyumbani kwake na kusahau kabisa kua aliagana na Suma kuwa ataenda kumfata.



Alifika alioga akala chakula na kuingia kulala mke wake akamuuliza.



"Mume wangu leo ni siku ya pili shemeji Suma hajarudi lakini kwanini?"



"Aah nimeshachoka Mimi, pesa anapata anashindwa kujiongeza kuchukua boda boda hadi hapa nimechoka kumfikiria bwana, yule hanihusu kwa chochote kama anashindwa kujiongeza basi leo ndio mwisho wangu na kama hatarudi tena itabidi tu nguo zake zichomwe moto kabisa"



"Mume wangu sio vizuri lakini"



"Ndio hivyo mwanaume gani unakaa nyuma nyuma kama mifuko ya suruali achana nae na ulale sitaki kelele mimi hapa"



Basi yule mwanamke aliamua kutulia na kuheuka upande wa pili na kulala.



Huku Kwa Suma mambo ni moto maana Nadya aliandaa chakula kizuri Kwa haraka na kumkaribisha Suma mezani, japokua alikua na kauoga flani lakini Nadya akamwambia.



"Kuwa huru humu ndani niko peke yangu tu usiwe na wasiwasi"

Suma japokua alitolewa wasiwasi lakini hakuweza kumuamin Nadya bado alijisemea mwenyewe kua wasiwasi ndio akili.



Wakati wanaendelea kula chakula mara mlango uligongwa kwa nguvu sana, Nadya alipatwa na wasiwasi sana sababu tangu aanze kuishi hapo hakuwahi kugongewa mlango usiku tena kwa nguvu, hivyo hali ya wasiwasi wa Nadya ilimshtua hadi Suma pia ikabidi pia aache kula na kujificha jikoni, Nadya alipiga hatua Hadi mlangoni na kugusa kitasa cha mlango kwa kusita sana na kufungua mlango.



ITAENDELEA.......



Je! Nini kitaendelea?
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 03

ILIPOISHIA.......

Wakati wanaendelea kula chakula mara mlango uligongwa kwa nguvu sana, Nadya alipatwa na wasiwasi sana sababu tangu aanze kuishi hapo hakuwahi kugongewa mlango usiku tena kwa nguvu, hivyo hali ya wasiwasi wa Nadya ilimshtua hadi Suma pia ikabidi pia aache kula na kujificha jikoni, Nadya alipiga hatua Hadi mlangoni na kugusa kitasa cha mlango kwa kusita sana na kufungua mlango.

ENDELEA NAYO......

Nadya Baada ya kufungua mlango akakutana na mzee akamsalimia na kumwambia.

"Mzee kigo umenishtua sana kwa kweli, kama unavyojua naishi mwenyewe humu ndani halafu ulivyogonga huo mlango nimeogopa Sana"

"Aah samahani mjukuu wangu lakini Kuna muda uliniambia nije ila sijakukuta nilikuja kukwambia kua tayari kazi ulinipa nimemaliza na hiyo hela nilikua nahitaji Kwa haraka sana"

"Ooh Sawa babu ngoja nikupatie, kweli ndio nimerudi muda mfupi tu Leo nilikua na kazi nyingi sana"
Kwakua kipochi alikua nacho karibu basi alitoa pesa na kumpatia.

"Napenda mabinti wanaojituma kama wewe lakini kwanini unaishi pekee kwenye hii nyumba?"

"Usijali babu hivi karibuni nitaanza kuishi na mtu usijali"

"Anha nilijua hakuna kabisa nilitaka kuja kuhamia"

Nadya alicheka sana Huku akifunga mlango na kuanza kumuita Suma.

"Suma..! Suma...!, uko wapi em njoo bwana"

Suma alitoka alipokua amejificha Nadya alicheka sana na kumwambia "Inamaana kumbe inawezekana kingenitokea kitu kibaya wakati mwanaume upo ndani kweli Suma?"

"Hapana madam boss unajua...."

"Suma ukitaka kunikwaza niite tena hilo jina"

"Sawa samahani lakini nimeshazoea, ila tuachane na hayo lazima nijilinde sababu jinsi ulivyo halafu unasema nyumba yote hii uko peke yako siwezi kuamini hivyo nikajua Moja Kwa Moja nimefumaniwa nikaamua kujificha kujiokoa"

"Suma sina mume Wala mpenzi nimeamua kufokasi kwenye kazi kuliko mapenzi na Kila napojaribu naona mauzauza tu ndio maana nikaamua kuwa hivi"

"Sawa bwana hongera"

"Asante kwahiyo utakula Tena au niondoe vyombo?"

"Aah hapana nimeshahisi nimeshiba tayari"

"Basi Sawa Kaa pale ungalie movie"

Suma alikaa kwenye sofa wakati huo Nadya anaondoa vyombo mezani kisha akaingia chumbani kwake akaoga na safari hii alivaa khanga nyepesi kabisa tofauti na mwanzo alioga na kuvaa tenge na tisheti lakini baada ya kula alioga Tena na kuvaa khanga nyepesi na kutokea sebleni wakati huo Suma alioga na kuvaa Tena nguo zake zilezile.

Nadya alivyotoka chumbani akaja kukaa kwenye sofa karibu na Suma, Suma alikua bize kuangalia movie hakumtazama kabisa Nadya na hakuweza kujua Nini amevaa alikua mshamba wa TV hakuwahi kuangalia tv Kwa uhuru tangu azaliwe.

Nadya alivyoona Suma hamjali Yuko bize akamshika kifuani kwake na kumwambia
"Suma muda umeenda twende basi ukalale"

"Aah hapana Wacha tu nitalala hapa hapa usijali"

"Suma naogopa kulala peke yangu bwana"

Suma alivyosikia sauti ya madeko kutoka kwa Nadya ikabidi Sasa amtazame Nadya kwanini kazungumza hivyo? Alivyotupa jicho akamuona Nadya mwili wake na hasa pale jinsi alivyokaa na kile kikanga kifupi hivyo asilimia ya mapaja yake yalikua nje Suma alishindwa hata kupepesa macho Kwa kuyatamani maungo ya Nadya na alipopandisha macho yake juu akakutana na chuchu zikiwa zimesimama ipasavyo Suma akajihisi msisimko wa ajabu sana na Nadya alimgundua mapema sana Suma wa jinsi ilivyoonekana.

Mara Ghafla kwenye ile movie ikasikika mripuko flani hivi ambao ulimfanya Nadya ajisogeze Kwa karibu zaidi na Suma, na kumkumbatia Kwa kungu Huku akiigiza kua anaogopa, Suma alishindwa kumtoa kwasababu tayari mambo yalishamuwea magumu kwake.

Nadya alijisogeza zaidi na kumkalia Suma mapajani kwake na kuchukua rimoti na kuzima tv Kisha akaanza kumchezea vindevu ambavyo vilikua vimeota vibaya sababu ya kukosa pesa yaani kuna ndevu za kimaskini na ndevu za kitajiri, afu Kuna ndevu za kukosa helaau basi... Maana hizi zangu sizijui zipo kundi gani.

Nadya alianza kucheza na ndevu za Suma mara aguse kifuani kwake Huku akicheza na mwili wake Suma wakati huo pia Suma hakua nyuma na yeye alikua anampapasa mgongoni kwake Hadi kwenye kiuno chake na kurudi juu mpaka pale walipoona tayari mambo Yako moto.

Na shughuli ilianzia sebleni na kwenda kumalizika chumbani, hapo kila mmoja alikua hoi sana na haikuchukua mda mrefu Kila mmoja alipitia na usingizi.

Upande wa kijijini pia mama yake Suma alikua hazungumzi na Aisha kutokana na yale mambo ya kumwambia kuwa waende mjini lakini Kwa siku hiyo Aisha nae aliamua kuwa mbali kidogo na mama yake Suma maana hakutaka kumkwaza Tena.

Mama yake Suma akamuita.
"Aisha kipenzi nisamehe sana kwa kile kilichotokea najua na wewe nimekufanya uwe mwenye mawazo lakini yote kutokana na uoga wangu lakini sasa nimefanya maamzi yangu mwanangu"

"Mama usijali kuhusu hilo sijajiskia vibaya lakini sikua nataka kukukwaza ndio maana nilianza kukaa mbali ,na Nina shauku ya kutaka kujua umeamua kipi?"

"Aisha mwanangu nimekubali kuungana na wewe kuelekea mjini"

Aisha alifurahi sana na kumkumbatia mama yake Suma Kwa furaha sana kisha akamwambia.
"Asante sana mama kwa kunikubalia ombi langu na Nina furaha isiokifani natamani hata nikupe zawadi kwaajili tu ya kukubali ombi langu"

"Usijali hata kidogo Binti yangu najua umepitia kipi na sikua nataka kufanya ukose furaha kwa kitu ambacho umekipanga pia najua ukiwa unafuraha wewe hata na mimi nakua na furaha hata mwanangu Suma pia atakua na furaha sababu mioyo yenu tayari ipo karibu na inafanya mawasiliano sana"

"Kweli mama na natamani hata angelikua na simu nikamueleza hili lakini hapana ninataka kumfanyia surprise au unasemaje mama?"

"Ndio ni vizuri sana natamani pia atafurahishwa na safari yetu"

"Basi mama sasa hivi ni usiku pumzika kesho tutapanga vizuri kuhusu safari yetu"
Mama Suma alilala akiwa anatabasamu baada ya kumuona Aisha anafuraha sana.

Asubuhi mapema Suma aliamka na kujikuta amemkumbatia Nadya tena wakiwa uchi kabisa akataka kujitoa kwenye lile kumbato lakini Nadya hakutaka kumuacha Suma ndio alizidi kumkumbatia Kwa ukaribu zaidi kitu ambacho kiliamsha hisia za Suma upya na kujikuta wanapata Tena na cha asubuhi kisha Nadya aliamka kwaajili ya kujianda kwenda kazini.

Akiwa bafuni anaoga, huku upande wa Suma alikua mwenye kujilaumu sana kwa kile kilichotokea na Nadya, baada ya kutoka bafuni akamkuta Suma hayupo Sawa akamuhuliza.

"Mbona upo hivyo Suma unanini?"

"Nadya kwanini umenipitisha kwenye majaribu kwanini uliamua kufanya hivyo?"

Nadya alimsogelea Suma Kwa ukaribu na kumwambia.
"Ni kwasababu Moja tu Suma, kwanza kabisa nilitamani kuwa na mpenzi Kwa muda mrefu lakini sikua nae sababu sikua na hisia na mwanaume yoyote lakini we nilipokuona Kwa mara ya kwanza tu moyo wangu ukaripukwa na upendo nikawa nashindwa jinsi ya kuanza lakini nashukuru Mungu kwa kunipa ujasiri huu nilioupata kwaajili yako pia nimeinjoy sana na penzi lako maana sijawahi kuinjoy mapenzi tangu nianze kuyajua ila wewe ndio fundi wangu"

"Unaongea ujinga sana Nadya Mimi Nina mpenzi wangu huko kijijini ananitegemea kwanini umefanya nimsaliti kwaajili yako?"

"Ooh mpenzi kijijini? unajuaje kama yeye anaweza kujikontroo usijipe donda la roho Suma huwezi jua yeye huko kijijini anafanya mangapi changamka wewe au mie sio mtamu eeh?"

Suma alichukia sana na maneno ya Nadya akasimama na kutoka zake nje, Nadya alitabasamu na kumwambia.
"I love you Suma na hapa ndio umeshafika huwezi kuniacha labda nitake mie"

Nadya alichukua handbag yake na kutoka chumbani na kumkuta Suma amekaa kwenye sofa, alisogea na kumbusu kisha akamwambia.

"Naondoka Suma mpenzi ila sitachelewa kurudi ukiwa na njaa stoo chakula kipo kwenye friji pia Kuna mahitaji pika ule usikae na njaa na sitaki utoke humu ndani"

Nadya aliondoka zake, Suma alibaki akiwa amekaa anawaza anawezaje kuishi hapo kuendelea kumsaliti mpenzi wake Aisha ambae anampenda sana kuliko kitu chochote.

Ukweli ilimuwia vigumu sana Kwa upande wake na alikua na mawazo sana sana, ikabidi ajiinue na kwenda kuoga ili kuufanya mwili uweze kufikiria jambo la kufanya tofauti na mawazo ambayo alikua nayo.

Upande wa Huku kibaruani kwake marafiki zake walifika na Kila mmoja kumuuliza mwenzake kuhusu Suma lakini kila mmoja alisema waliondoka kivyao wakiwa wanaendelea kubishana mara ilifika gari na akateremka mwanaume ambae ni yule jamaa ambae aliemleta Suma kufanya kazi hapo akawauliza.

"Nyie mwenzenu yupo wapi?"

"Kaka sisi hatujui hata yuko wapi lakini jana tulimuacha hapa akisema kuwa anakusubiria wewe"

"Ndio nilimwambia anisubiri lakini nikapitiwa sikuja kumchukua na hata nyumbani hakuja pia na sasa basi kama amepotea au yuko wapi atajua mwenyewe sihitaji kujua na nimekuja na nguo zake kifupi simtaki tena nyumbani kwangu"

"Lakini broo yule kama mdogo wako kwanini umchukulie hasira wakati ni mgeni huwezi jua amekumbana na Nini huko alipo"

Juma alizungumza na wote wakatikisa kichwa kua wamekubaliana na alichozungumza lakini jibu la yule jamaa lilikua.
"Akija mwambieni kua simuhitaji kwangu hivyo mtajua wenyewe jinsi ya kumsaidia"

Kisha karusha kifuko cha nguo za Suma kisha akondoka zake na wakati ameondoka mara kuna gari ilifika pale na waliposogelea gari hiyo wakamkuta Nadya ambae ndio hupenda kumuita madam boss walimsalimia kisha akawauliza.

"Nimeona yule jamaa bonge hapa alikua anawafokea kwani ndio boss wenu?"

"Hapana yule bwana ndio aliemleta Suma hapa na anasema siku ya mbili hajalala kwake na ukiondoa siku Moja ambayo alimkuta kalala hapa hapa"

"Mh! kwahiyo hata nyie hamjui Suma yupo wapi?"

"Ndio madam boss tupo hapa tunajiuliza wapi alipo maana Jana tulimuacha hapa akimsubiri yule jamaa lakini anasema alipitiwa na hakuja kumchukua, sasa nani mwenye makosa na ukizingatia Suma ni mgeni?"

"Anhaa poleni sana washkaji zangu badae nitapita kwaajili ya kujua nini kinaendelea kama amepatikana au lah"

"Sawa boss Asante Kwa kutuunga mkono"

Nadya alitoa pesa na kuwapa washkaji zake wakapate chai kisha akaondoka zake bila ya kuwambia kua Suma yupo kwake.

****

Maisha ya Suma na Nadya kwenye nyumba ya Nadya yaliendelea na Suma hakua mnyonge Tena, kiufupi alimtolea uvivu kabisa Kila anapohitaji Nadya Suma humpa kile anachohitaji Tena Kwa Kasi hasa.

Kiufupi Suma alishakubaliana na Kila kitu kuhusu Nadya na kusahau kabisa kuhusu Aisha.

Maisha yaliendelea hivyo na Suma alikua anafanya Kila kazi pale ndani kwa Nadya kiasi kwamba hata usiku Nadya akihitaji penzi la Suma, Suma hua anakua amechoka sana japokua anampa anachohitaji lakini Nadya alikua hariziki kabisa.

Upande wa kijijini pia Aisha na mama yake Suma walikua na furaha ya kujiandaa kwaajili ya kwenda mjini.

Mama yake Suma akazungumza
"Kwahiyo Aisha itakuaje kuhusu mashamba yetu na mazao ambayo tunayaacha na vipi kuhusu nyumba yangu na vitu vilivyomo ndani?"

"Mama usijali kuhusu Chochote maana Kila kitu tayari nimeshaandaa sababu kwanza hapa nyumbani nimeongea na msichana ambae atakuja kuishi pia kule shamba nimemuachia maagizo yote ambayo ni sahihi"

"Kama ni hivyo sawa nimekuelewa Sasa tunaweza kwenda"

Wakiwa wamekaa mama yake Suma akamuuliza.
"Mbona hatuendi stendi?"

"Mama hatutamia gari la watu wote tutatumia gari binafsi"

Kabla Aisha hajamaliza kuelekeza mara ilifika gari aina ya BMW kisha Aisha akamwambia
"Gari hiyo hapo twende mama"

Mama Suma aliamka na Aisha alimfungulia mlango wa nyuma na mama Suma akaingia kisha akachukua mabegi Yao na kuweka kwenye buti kisha yeye akaingia kwenye gari kisha safari ikaanza Huku wakipiga story za hapa na pale.

Hasa Aisha alikua anamuuliza huyo dereva kuhusu kulivyobadilika huko mjini, mama Suma alikua Hana vha kuuliza sababu hakua anajua Chochote kuhusu Jiji hilo hivyo alikua kimya tu.

ITAENDELEA......

Yajayo yanafurahisha, Suma yupo ndani ya mikono ya Nadya na huku Aisha na mama yake Suma wanaingia ndani ya jiji. Je! Itakuaje? Najua humu wengi wanapenda story hizi basi usishangae kuna mtu anatamani kunifuata aseme ni fupi lkn hadithi iliyopita hakunifuata.
 
SIMULIZI: PENZI LANGU
SEHEMU YA 04

ILIPOISHIA.......

Aisha alikua anamuuliza huyo dereva kuhusu kulivyobadilika huko mjini, mama Suma alikua Hana vha kuuliza sababu hakua anajua Chochote kuhusu Jiji hilo hivyo alikua kimya tu.

ENDELEA NAYO....

Ilikua siku ya Jumamosi Nadya akamwambia Suma.

"Leo nahitaji kutoka na wewe mpenzi si tunatoka pamoja eeh?"

"Aah Nadya mie siwezi kutoka"

"Kwanini?"

"Lakini...."

"Suma hakuna cha lakini lazima tutoke kama wewe ni mpenzi wangu hivi hutaki marafiki zangu wakujue shemeji Yao?"

"Aah sawa kama umeamua hivyo nipo tayari"

Basi Nadya alifurahi sana baada ya Suma kukubali kutoka nae.

Maandalizi yalikua pambe tu Nadya alimtolea nguo Suma na kumwambia.
"Baby hizi nguo nimekununulia mda mrefu lakini nilisahau kukupatia sababu ya mambo kuwa mengi"

"Ooh asante sana Nadya wangu ndio maana nakupenda sana"

"Usijali bwana basi Wacha nikaoge kwanza maana hili joto ni la hatari"

Nadya aliingia chumbani na kuweka vizuri nguo ambazo zimo kwenye kabati lile ambalo ametoa nguo na kumpatia Suma kisha akafunga kabati na kurudisha funguo kwenye handbag yake.

Aliingia bafuni alioga kisha akabadilisha nguo na kutoka sebleni akamkuta Suma ametulia zake kwenye sofa. Nadya kama kawaida yake yaani hupenda sana kumtumia Suma wakati anajua mwenzake amechoka.

Alienda kukaa karibu nae huku manukato mazuri yakinukia na kikanga chake kifupi, Suma akamuhuliza.

"Mbona umevaa hivyo Nadya unataka nini?"

"Suma inamaana hujui nachotaka kwako hivi we ni mwanaume wa aina gani lakini eeh, wenzako wengine wanatamani wapate kutwa mara tatu kwa kila siku lakini we unajiregeza tu hapa aah ohk basi am sorry"

Nadya alikasirika na kuingia chumbani kwake alivaa viatu vyake na nguo zake nzuri ambayo ilimpendeza vema sana kisha akatoka na kumwambia Suma.

"Mie naondoka zangu na kuhusu kutoka na wewe nimebadilisha wazo langu hivyo nitakukuta kwa heri"

Nadya aliondoka zake na kumwacha Suma akiwa hajali wala Nini.

*****

Kama mjuavyo safari ya kutoka Tabora hadi Dar hua ni safari refu sana watumia trein hufika kama sio siku tatu au nne inategemea, hivyo hata Aisha na mama mkwe wake siku hiyo hadi inafika usiku bado walikua njiani ikabidi Aisha atafute hotel ya karibu ili kuweza kupumzika usiku huo.

"Mama mama amka basi tumefika hotelini twende ukajinyoshe kidogo"

"Japana mwanangu usijali mimi nimeshalala hapa panatosha"

Basi baada ya mama Suma kusema vile Aisha hakua na jinsi ikabidi tu na wao washushe siti zao waweze kulala kwenye gari mle mle.

Upande wa Suma alikua ameikumbuka sana familia yake na zilipita kama wiki 4 hivi bila ya kuwasiliana nao na kwasababu hakua na simu lakini tayari Nadya alimfanyia shopping ya vitu muhimu hivyo ikiwemo na simu.

Aliingia chumbani na kuchukua suruali yake ambayo alikua amevaa wakati amefika hapo na kusachi kwenye mfuko na kukuta karatasi ya namba akachukua simu na kubofya sehemu kadhaa kisha akaingiza namba na kupiga.

Simu ambayo ilimshtua Aisha kutoka usingizini alipokea na kuzungumza na Suma Kwa furaha sana.

"Vipi mpenzi wangu tumekua na wasiwasi sana kuhusu wewe kwanini ulikua kimya sana?"

"Aah Aisha jamani nimekumisi pia mke wangu lakini kama unavyojua mambo bado yameniwea magumu lakini afadhali sasa kua nimepata simu tayari nivumilieni kidogo nitakua nawatumia pesa ya mahitaji mke wangu"

"Suma nakupenda sana mpenzi wangu zaidi ya sana naomba usinisaliti mwenzio nitaumia sana"

"Aah .. a..Aisha siwezi kukufanyia hivyo najua wapi tumetoka mpenzi wangu"

"Basi sawa pumzika kipenzi changu"

Suma alikata simu huku akiwaza kua tayari Aisha amemdanganya na vipi kuhusu mama yake kuanzia hapo Suma alikuaa na wasiwasi sana na mawazo yalikua mengi kupitiliza.

Ilikua yapata majira ya saa 7 usiku Nadya alirudi akiwa amelewa sana siku hiyo, Suma alimshangaa sana sababu hakuwahi kumuona kabla Nadya akiwa yupo hivyo, alimchukua na kumpelekea chumbani akamlaza kitandani akamvuta viatu na kumfunika shuka kisha akawa anamtazama tu hakua amemuuliza Chochote kile.

Alitoka sebleni akiwa bado anawaza sana. Asubuhi mapema aliamka mapema na kufanya usafi kwenye nyumba nzima kisha akaandaa supu kwaajili ya Nadya kisha akaenda kumuwamsha Nadya, aliamka na kumkumbatia Suma na kumwambia.

"Baby nimekumiss sana mwenzio"

"Nadya kipenzi amka ukaoge kwanza kisha nimekuandalia kitu ambacho kitakusaida kukuweka sawa basi amka usiwe mvivu"

Nadya aliamka na kuingia bafuni alioga kisha akarudi na kubadilisha nguo kisha akatokea sebleni na kukuta mambo ya supu mkate na mayai alikula na kumshukuru sana Suma.

"Suma mpenzi Asante sana Kwa kunijali pia nisamehe kwa kilichotokea Jana sikutegemea kufanya vile ila nilikutana na marafiki zangu ambao walinipa vishawishi Hadi nikanywa kupitiliza"

"Usijali kuhusu Hilo Nadya wangu nakupenda sana"
Suma alisogea karibu na nadya na kumbusu kwenye lipsi zake kisha akaondoa vyombo na kuviweka kwenye vyombo vichafu kisha akarudi kumwambia.

"Leo kwakua Jumapili basi nenda kapumzike Mimi namalizia kazi kisha nitakuja pia"

"Really baby?"

"Ndio nitakuja"

Nadya aliingia chumbani kwake na kujitupia kitandani alitoa ile khanga aliyokua amevaa na kubaki mtupu akajifunika shuka akimsubiria Suma wake.

Upande wa safari ya wahamiaji kutoka kijijini ilikua imetaradadi pia dereva alikua anakanyaga mafuta sio poa Huku story za hapa na pale zikiendelea.

Aisha alikua anawaulizia marafiki zake na majirani, huyu dereva alikua anampa story mbali mbali ambazo zilikua zinamfurahisha sana Aisha na kumuhuzunisha pia.

Suma alimaliza kusafisha vyombo kisha alikaa sebleni akiwa anawaza.

"Hivi Nadya ananichukuliaje Mimi, kwanini ananitumikisha sana kingono hata kama nikimwambia kua nimechoka yeye bado hunihitaji tu tatizo lake nini hasa mbona nashindwa kabisa kumuelewa huyu mwanamke..mmh naona Huyu dada ananitumia pasi na mafanikio yoyote maana kama ananipenda asingeniweka tu ndani kama mfanya kazi wake, sawa nakula nalala lakini Sina imani nae kabisa lazima nichangamke sikuja Huku kufata mapenzi nimekuja kufanya kazi kwaajili ya familia yangu, Sasa nikisema nibweteke mama yangu na Aisha wangu watapata shida sana eeh Mungu nipe ujasiri kijana wako"

Hatimae wasafiri walifika salama jijini Dar es salaam na Moja Kwa Moja gari ilielekea maeneo ya msasani ndiko ambapo kulikua na nyumba Yao ambayo watu wengine hawaifahamu.

yule dereva akamwambia
"Dada Aisha nimekuleta hapa sababu ndio sehemu salama kwako hivyo utaishi hapa juku tukiendelea kufanya kitu kizuri kwaajili Yako"

"Aah sijaelewa unamaana gani kusema hivyo kwani Kuna kitu gani nyuma ya hili ambacho sikijui?"

Yule dereva aliona anaelekea kuharibu mipango hivyo akajikuta anampoteza Aisha ili asishtuke akajifanya kumuuliza.

"Kumbe bado una wasiwasi na kilichotokea?, usijali dada Aisha ni muda mrefu sasa umepita na usichokijua ni kwamba hao waliohusika tayari wameshatiwa kizuizini hawawezi kukufikia Tena"

"Ooh Dan nenda tuache tupumzike kwanza"

"Sawa dada Kila kitu kipo stoo ila ukihitaji chochote nipigie simu nitakuja"

"Sawa kwaheri"

Dan aliondoka na kuwaacha Aisha na mama yake Suma, Aisha akamwambia mama mkwe wake
"Mama hapa ndio nyumbani na tutaishi hapa"

"Nyumba ni nzuri sana lakini ipo kimya sana"

"Nikweli mama sababu hakukua na mtu yoyote ambae anaishi hapa tangu wazazi wangu wamefariki ilikua imefungwa tu na hatukua tunaishi hapa kabla, tulikua tunaishi kwenye nyumba nyingine huko masaki"

"Ooh wazazi wako walikutengezea mazingira mazuri sana binti ila vijana wenye roho mbaya ya kwanini ndio iliyowafanya wateketeze familia Yako pole sana"

"Asante mama na sitaki kukumbuka kile ambacho kimetokea nataka kuanza upya na familia yangu mpya ambayo ni wewe na mpenzi wangu Suma sababu nawapenda sana"

"Aisha Wacha tu nikwambie kua na sisi tunashukuru sana kwa ujio wako umetuvumbua mambo mengi sana pia hata akili zetu pia umezinyoosha kutokana kutotaka kutafuta maendeleo kwenye maeneo mengi sababu ya uoga lakini Suma pia alikua muelewa kwako na akaamua kutuacha na kuja Huku bila ya uoga japokua ilimuwia vigumu sana kutuacha watu ambao anatupenda lakini hakua na jinsi"

"Mama usijali kuhusu Hilo naamini kua Suma ridhiki yake kama iliandikwa atapata Kwa kuja mjini basi atapata mafanikio makubwa sana"

"Nikweli mwanangu, ila tuachane na hayo ukweli nimechoka sana Nina uchovu mwingi sana nahitaji kupumzika"

Aisha alimpeleka chumbani na kumwambia
"Utakua unalala huku ndani siku zote na mimi nitakua nalala chumba cha pili kama ukiona huelewi utanishtua tu nitaamka hata atakaporudi Suma pia tutakua na furaha zaidi"

"Sawa mwanangu"

Aisha alitoka chumbani na kurudi seblen kisha akajilaza kwenye sofa huku akikumbuka mambo mengi ambayo yametokea kipindi Cha nyuma Cha maisha yake.

Alikua anawaza sana kuhusu kulipiza kisasi Kwa wale watu ambao wamemuulia wazazi wake lakini moyo wake ulijawa na wasiwasi sababu alikua anawaza kama ataianzisha vita upya atawapoteza Suma na mama yake hivyo ni jambo ambalo lilikua linamfikirisha sana.

"Hahahaha Binti mrembo sana mashallah bwana Abdul na mke wake wamebahatika kupata Binti mrembo sana angalia macho yake kama mzungu pua yake mdomo wake angalia hata mwili wake pia, akiwa mkubwa atakua mtam sana huyu, hahahahahah"

Ni sauti ambazo zilikua zinajirudia kwenye kichwa cha Aisha na huku alijaribu kukumbuka sura za watu ambao wamewafanyia ukatili wazazi wake.

Aliamka kutoka pale seblen akaingia bafuni akajimwagia maji kisha akajipumzisha kitandani kutokana na kuchoka Kwa safari iliyokua ndefu sana.

Kwa upande wa Suma pia alimaliza kazi zake mapema sana kisha akajilaza kwenye sofa mara akasikia mngurumo wa gari Suma alijifanya amelala fofoo, mara mlango wa nyuma pia ukafunguliwa na Nadya akaingia pia na kufunga mlango kisha akasogea hadi karibu na Suma kisha akambusu kwenye paji la uso na kuingia chumbani kwake akajimwagia maji na kutoka sebleni akiwa na kanga yake nyepesi kama kawaida yake akasogea karibu na alipoegesha Suma kichwa chake na kutoa mto ambao amelalia na kumuweka kwenye mapaja yake huku akichezea nywele zake.

"Mpenzi jamanii kulala Gani huko jamanii nimerudi mke wako"

Suma alijifanya kujinyoosha na kutaka kuamka Nadya akamzuia na kumwambia.
"Sitaki uamke kipenzi yaani natamani hata nisiwe naenda kazini tuwe tunakaa hivi Kila mara nataka kuimarisha upendo wangu kwako Kila siku"

"Ooh Nadya unanipenda kiasi Gani?"

"Yaani Suma sijawahi kumpenda mwanamme kama navyokupenda wewe sababu kwanza ni watofauti na wengine hauna tamaa mpole mkarimu kifupi unanivutia sana"

"Ooh asante sana kipenzi changu, ila leo nimeandaa chakula kizuri kwaajili yako"

"Baby lakini nimeshiba tayari leo ofsini kulikua na...."

"Nadya tafadhali nataka ule japo kidogo tu mke wangu"

Nadya alivyoitwa mke wangu alifurahi sana na kukubali kula chakula alichopika Suma.

Walikula huku story za hapa na pale zikiendelea, Suma nikama akitaka kuzungumza kitu lakini alipokumbuka kihusu maneno ambayo ameyazungumza Nadya kuwa yeye ni mwanamme wa tofauti hana tamaa ikabidi ajitulize na kile alichotaka kumwambia abaki nacho moyoni mwake.

Walikula chakula Hadi wakashiba na kuzima taa kwaajili ya kwenda kulala.

Usiku huo ulikua wa mawazo sana kwa Suma sababu alikua na mipango mingi sana kichwani kwake na ya kupata pesa hivyo akawa anatafuta njia ya kumueleza Nadya kuhusu mpango wake.

Asubuhi mapema kama kawaida Suma aliamka na kuandaa kila kitu na kumuamsha Nadya wake akajiandaa kisha akatoka sebleni kwaajili ya kunywa chai.

Wakati Nadya anakunywa chai muda huo Suma alikua anasafisha viatu vya Nadya na kuviweka mlangoni na kisha akamsogelea na kumwambia.

"Nadya mke wangu leo nataka kuwafanyia surprise marafiki zangu wa kina Juma sababu nimewamiss sana, maana nilipotea machoni mwao tu ghafla na nataka niwambie sehemu nilipo ili wasiwe na wasiwasi juu yangu"

"Ooh Suma sitaki ukawambie sehemu ulipo kama unaenda tu kupiga nao story ni sawa ila sitaki uwambie ulipo kwa Sasa"

"Ooh kuhusu Hilo tu mke wangu ondoa shaka si unaniamini basi wala hata usijali na sitachelewa kurudi, nitarudi mapema na kukuandalia chakula kama kawaida"

"Sawa mpenzi wangu nakupenda sana Suma, usiniache sawa mme wangu?"

"Naanzaje kukuacha mwanamke mzuri kama wewe"

Suma alitaka kumbusu Nadya lakini ghafla simu ya Nadya ikaita hivyo hiko kitendo kikakatishwa na hiyo simu kisha akapokea na baada ya muda mfupi alimuaga Suma Kwa haraka na kuondoka zake.

Suma alimshika kiuno chake na kusema.
"Chelewa chelewa utakuta mwana si wako Suma"

Suma aliingia chumbani na kuanza kupekua alifunga droo ya kitanda akakuta funguo nyingi akachukua zote na kuanza kufunguka kabati ambalo lilikua kubwa sana akafungua mlango wa kwanza akakutana na nguo za kiume nyingi sana akafungua mlango wapili akakuta viatu vya Kila aina pia vya mwanaume na akaendelea kufunguka milango yote na mwisho kabisa akakutana na kisanduku akakifungua pia na alichokikuta kilimfanya astaajabu sana na kumfanya ashangae sana.

ITAENDELEA......

Ukiiona ni fupi, basi nisaidie kuirefusha shubaamit.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom