Simulizi: Maisha ya ajabu ya mganga anayehusishwa na vifo vya kutisha

Mzee Rufiji

JF-Expert Member
Aug 24, 2024
208
315
Dodoma/Singida. Ni safari ya kilometa 27 ndani ya eneo lenye miti mingi hadi kufika nyumbani kwa mganga wa kienyeji, Nkamba Kasubi anayedaiwa kuwauwa na kuwazika watu 10 kwenye vijiji vya Makuro na Poribanguma katika mikoa ya Singida na Dodoma.

Katika mji wake, eneo la Sawekwa lililopo kijiji cha Poribanguma, yalifukuliwa makaburi sita ya Seni Jishabi (28), Mohames Juma (27), Daudi Msanku (27) na Ramadhan Yusuph (26).

Wengine ni Mwekwa Kasubui (miezi minne) ambaye ni mtoto wa mganga huyo na Maka Shaban ambaye ni mtoto wa Selemani Nyalandu, mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya mauaji inayomkabili Kasubi na wenzake.

Makazi ya mganga huyo katika eneo la Sawekwa yamezingirwa na pori pande zote na amejenga nyumba ndogondogo zaidi ya tatu za kuishi, kibanda cha mashine ya kusaga, huku kingine akikijenga kwa umbo la duara.

Ukifika katika eneo hilo, unakutana na nyumba tatu zilizokuwa zikitumiwa na Kasubi, wenza wake na watoto saba.

Barazani mwa nyumba moja ya tope iliyokuwa imeezekwa kwa nyasi kuna jiwe linalodaiwa kutumika kusaga mwili wa Daudi, baada ya kuchomwa moto kabla ya majivu yake kuwekwa katika ndoo yenye ujazo wa lita 20.

Nyuma ya nyumba hiyo, ndiko kulikojengwa kibanda cha mashine ya kusaga iliyokuwa ikitumiwa na familia hiyo pekee katika eneo hilo na nyuma yake ndiko kilichojengwa kibanda cha duara.

Mbele ya kibanda cha duara, kulikuwa na shimo lililokuwa na urefu usiozidi mita tatu, ndilo linalodaiwa kuwa na mwili wa Daudi kabla ya kuchukuliwa na kwenda kuchomwa moto na kusagwa.

Ushirikiano na majirani
Balozi wa Shina namba 2, Meru Darema alisema mganga huyo alijisajili katika ofisi ya kijiji mwaka 2021 na tangu amefika katika kijiji hicho huwa hajihusishi katika shughuli za maendeleo.

Hata hivyo, alisema mganga huyo alikuwa ni mtu anayependa ubinafsi na wananchi walikuwa hawafiki katika mji wake.
“Sisi tunabaki kuona pikipiki ama magari yakiingia na kutoka lakini yeye mwenyewe alikuwa hana ushirikiano na mtu. Alikuwa na mashine yake binafsi ambayo aliitumia na familia yake tu,” alisema.

Alisema hakuna huduma aliyokuwa akichukua kijijini zaidi ya maji na kuwa huduma zingine alikuwa akizipata katika eneo la Kwamtoro.

“Sisi tukihitaji mchango kuna mtu anamwagiza, tukihitaji ushiriki wa shughuli ya maendeleo kuna kijana mmoja alikuwa akimtuma kuja katika kazi ya maendeleo,”alisema.

Alisema hakuwahi kutoka katika maendeleo, misiba wala mikutano ya wananchi au kwenye huduma yoyote.

Akorofishana na majirani
Darema alisema Aprili 2024, mganga huyo alichimba mashimo marefu porini ambayo yalisababisha mbuzi na ng’ombe kudumbukia humo.

Alisema baada ya kukuta mifugo hao wametumbukia katika moja ya shimo, waliitisha mkutano uliomshirikisha mwenyekiti wa kijiji na askari ili kulitafutia ufumbuzi.

Alisema mganga huyo alivyoona wingi wa watu alikimbilia Kituo cha Polisi, jambo ambalo liliwafanya viongozi kwenda katika kituo hicho ili kueleza kilichotokea.

Darema alisema mganga huyo alikubali kweli alichimba mashimo kwa ajili kutafuta maji ya chini lakini aliyakosa.

“Alisema wenye ng’ombe anawalipa ambapo kila mmoja aliuliza anataka alipwe shilingi ngapi, mwenye ndama wa ng’ombe akasema anataka Sh220,000 na wa mbuzi Sh35,000,” alisema.

Alisema mkuu wa kituo cha Polisi aliwahoji endapo mashimo hayo yakiukiwa, kama wanaweza kuendelea kuishi naye katika kijiji hicho, jambo ambalo walilikubali kwa kuwa yatafukiwa.

“Hata hivyo, tulimtaka kuja kuomba radhi kwa wananchi kwa kuwa walishakasirika. Tulipanga tuitishe mkutano ambao niliitisha lakini kwa bahati mbaya mvua kubwa ilinyesha iliyojaza makorongo hivyo polisi walishindwa kuvuka wakashindwa kupita,” alisema.

Alisema hata mganga huyo hakufika katika kikao husika kwa ajili ya kuomba msamaha kama walivyokubaliana.

Alisema mbali na uganga hakuna shughuli nyingine ambayo alikuwa akiifanya zaidi ya kulima nusu ekari ya mpunga.

Alisema walipokwenda walikuta wanawake wanne na watoto saba katika familia hiyo ilibidi tuwaweke ndani wasipigwe na wananchi.

Aidha, baada ya tukio hilo wananchi walibomoa na kuchoma moto nyumba zake, huku mifugo ikichukuliwa.

Pia katika nyumba hizo kulikutwa magari mawili madogo yasiyotumika pamoja na trekta dogo aina ya power tiller.

Wananchi washtuka
Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Porobanguma, Hamis Songoro alisema saa 2.00 usiku Agosti 24, mwaka huu akiwa katika televisheni alisikia taarifa Kasubi amekamatwa kwa mauaji.

“Baada ya kusikia habari hiyo na sisi kuna watu ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha nilimpigia Mkuu wa Kituo cha Polisi Kwamtoro saa 11.00 alfajiri kuwa tuna shaka na mtuhumiwa aliyekamatwa Singida kwa kuwa kuna watu waliofariki kijijini katika mazingira ya kutatanisha,” alisema.

Alisema mkuu wa kituo hicho alimshauri kwenda na watu wachache kwa ajili ya kubaini kama kuna viashiria vyovyote vya watu kuzikwa kwenye eneo hilo.

Walipofika kwa Kasubi, alisema waliona viashiria vya watu kuzikwa na walitoa taarifa polisi, kisha ilithibitika kuwa wapo waliozikwa.

Alisema mkuu wa kituo hicho cha Polisi aliwaagiza kuweka ulinzi katika eneo hilo na walitekeleza kuanzia Agosti 25 hadi 26 mwaka huu.

Agosti 27, 2024, alisema mkuu wa kituo cha Polisi, timu kutoka wilayani na Mkoa wa Singida ilifika ikiwa na watuhumiwa na waliwaongoza hadi sehemu waliyozikia watu.

Waliyokutana nayo
Darema alisema walipofika katika eneo hilo walikuta wanawake wanne na watoto saba katika familia ya mganga huyo.

“Ilibidi kwanza tuhakikishe usalama wao kwa kuwaweka ndani na kuwalinda ili wasipigwe na wananchi waliokuwa na hasira kali kabla ya kuendelea na jambo jingine,” alisema.

Akielezea kuhusiana na kibanda hicho, Darema alisema kilikuwa na milango miwili na mbele ya mlango mmoja kulikuwa na kaburi, huku ndani ya nyumba kulikuwa na mwili wa mtu aliyekalishwa.

“Yaani amekatwa kuanzia katika kiuno na kukalishwa ndani ya kijumba hicho kilichojengwa kwa mduara na sehemu ya juu ilikuwa imeezekwa, juu yake kulikuwa na kitu kama ungo uliozungushiwa ushanga na juu yake kulikuwa na chungu kidogo ambacho kilikuwa na vitu vya ajabu ajabu,” alisema.

Alisema ndani ya kibanda hicho cha mduara walikutana na sime imechomekwa chini, kisu na kipande cha muwa na baada ya kuchimba walikutana fuvu la kichwa cha binadamu.

Kwa upande wa zizi la ng’ombe, walikuta kaburi moja walikozikwa watoto wawili.

Katika zizi hilo pia, alisema walikuta beberu wa mbuzi aliyefukiwa katika siku zisizozidi mbili na alitobolewa sehemu ndogo katika kifua.

Alivyoingia Singida
Maisha ya mganga huyo yangemshangaza yeyote kutokana na tabia zake, ikiwemo kuweka fedha njiani, kuchota mchanga kwenye eneo alilokanyaga mtu na tabia nyingine za ajabu, kama inavyoelezwa na Mjumbe wa Kijiji cha Makuro mkoani Singida, Rashid Ibrahim.

Tabia hizo kwa mujibu wa mjumbe huyo, alianza kuzionyesha muda mchache baada ya kupokelewa na mwenyeji wake, Wawa Ramadhan Novemba mwaka jana na hakukuwa na aliyejua shughuli yake rasmi.

Kutoka kuwa mwenyeji, mjumbe huyo alisema baadaye Wawa aligeuka kuwa mkwe wa mganga huyo, baada ya kumuozesha binti yake ambaye hata hivyo alikuwa ni mke wa mtu mwingine. Kwa maneno mengine alioa mke wa mtu.

Kaka yake Wawa, Yusuph Ramadhani alisema pamoja na kumkanya ndugu yake atengane na mganga huyo mara kadhaa, hakuwahi kufanikiwa.

Alisema Wawa alikuwa akijibu kuwa mganga huyo ni mkwe wake hivyo asingeweza kujitenga naye, akisisitiza ujio wake ulivuruga hata uhusiano na familia.

Kwa mujibu wa Ramadhan, mdogo wake alibadilika mara tu alipompokea mganga huyo, hakuwa tena karibu na familia yake.

Tabu Ramadhani, dada wa Wawa, alisema anachokikumbuka aliwahi kuibiwa nguo ya ndani na kaka yake ikapelekwa kwa mganya huyo.

Tukio hilo, alisema lilifikishwa hadi polisi na baadaye wakaamua kulimaliza kifamilia, baada ya nguo hiyo kurudishwa ingawa ilishatobolewa.

Wanachosema majirani Singida
Hatua ya mganga huyo kuruhusiwa kujenga katika eneo hilo jirani, haikukubaliwa na wenyeji kutokana na sifa mbaya alizokuwa nazo.

Elibariki Hango, alieleza kuwa mganga huyo alijadiliwa kwenye vikao mbalimbali na taarifa zake kupelekwa kwa diwani na wilayani na muda mchache baadaye ilisikika kuwa ameua.

“Shughuli nyingine mimi sielewi kwa sababu mimi simjui ila nasikia tu yupo ila kwa sura simjui ila uganga wake ulikuwa wa kijambazijambazi tu,” alisema.

Alisema hali ya maisha katika eneo hilo imerejea kuwa shwari baada ya mganga huyo kukamatwa na eneo alilokuwa anaishi lipo chini ya usimamizi wa jeshi la polisi.

Kingine kinachostaajabisha, anasema eneo la nyumba mpya aliyokuwa anajenga mganga huyo kuna shimo na mfuniko wake uliandikwa: ‘Siku ya Hango” ni tarehe ’14/8/2024’.

Diwani
Diwani wa Makuro, Jumanne Salum alisema taarifa za mganga huyo kuanza ujenzi wa nyumba ya kuishi alizipata kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji.

“Nilimuuliza mwenyekiti wangu wa kijiji, alisema hajui jambo hilo lakini mwenyekiti wangu wa chama alisema nilimwambia muiteni kwenye kamati ya siasa, baadaye alikiri kuwa yeye ndiye aliyemkaribisha” alisema.

Baada ya taarifa za kupotea kwa kijana wa kwanza aliyetambulika kwa jina la Samwaja Agosti 8, mwaka huu, alisema mtu mmoja alikamatwa kwa kuwa ndiye aliyekuwa karibu na aliyepotea siku ya tukio.

Kinachowaumiza wakazi wa eneo hilo ni kile alichoeleza, hatua ya mwenyekiti kumpokea na kumkaribisha mganga huyo ajenge katika eneo lao.

Alisema hadi sasa mwenyekiti wa kijiji hicho hajulikani alipo, inadaiwa kuwa ametoroka baada ya tukio hilo.

“Mwenyekiti anajua utaratibu wa kuwapokea wageni na vitimbwi vya mganga vilianza tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini jambo hili la kumpokea mganga amelifanya Julai,” alisema.

Joshua Majengo ni mkazi wa kijiji hicho, anasema mganga huyo alianza kwa kukusanya vinyesi vya ng’ombe na vitambaa vya nguo chakavu na ilidaiwa anakwenda kutengeneza mazindiko.

"Kuna siku alikamata ng’ombe wa kijana mmoja na alimkata kichwa na kukitupa ndani ya shimo lenye mifupa mingi ya mbuzi na dawa nyingi za asili na matambara.

“Baada ya kuita askari walienda kufanya ukaguzi kwenye nyumba aliyokuwa anaishi mganga huyo na kukuta nyama za ng’ombe kwenye shimo la choo,” alieleza.

©Mwananchi
 
Unasoma ukuukitetemeka kwa woga,waganga wengi wanaroho za kishetani sana,nawengi ni wachawi kujua wao ni jambo dogo sana,sema intelijinsia ya vyombo vya dola iko kwa marathi ya viongozi sio kwa wananchi
 
Unasoma huku unatetemeka kwa uoga,waganga wengi wana roho za kishetani sana,na wengi wao ni wachawi,kuua mtu kwao ni jambo la kawaida mno,intelijinsia ya vyombo vya dola ingebaini haya mapema,ila iko kwa masirahi ya viongozi sio rai wa nchi
 
GSqeB5lXQAAPBV9.jpeg
 
Huyu mganga ni aina ya serial killer
 
Uganga wa jadi wa kiafrika huu, uliohusisha ukatili, sometime heri dini zilikuja kufuta Utamaduni huu. (kafara za kuchimbia watu chini miaka 1800+ kwa Afrika zilipamba moto sana.)
Katika baadhi ya makabila ya Tanganyika, kulikuwa na utamaduni wa kuuzika mwili wa chifu/mtemi pamoja na mtu aliye hai. Na familia iliyokuwa ikimtoa mtu wa kuzikwa na marehemu ilikuwa ikiliaona hilo kama jambo la heshima kwao.
 
Uchaggani, kulikuwa na shida hii.
 
Back
Top Bottom