Asha D Abinallah
Senior Member
- Apr 5, 2015
- 140
- 904
ILANI: Huu ni mwendelezo na sehemu ya pili ya makala za Simu za mikononi katika Mahusiano ikiwa sehemu ya pili.
Unaweza kusoma sehemu ya kwanza hapa:
Mahusiano ni sehemu mhimu na nyeti katika maisha ya kila siku ya binadamu. Mahusiano ya Kimapenzi yana nafasi kubwa katika kuathiri au kushamirisha mienendo za kibinadamu katika maisha yetu ya kila siku, iwe katika utendaji wa kazi, maamuzi ya msingi katika maisha ya kila siku, mikakati/mipango kwa ujumla na maeneo mengine mengi.
Mahusiano ya kimapenzi ni sehemu muhimu kwa wanadamu wengi, bila kujalisha ni kijana ama mzee, mwanamke au mwanaume, mlemavu au mzima, wote huwa ama hutamani kuwa na watu ambao wana nafasi kubwa katika maisha kama wapenzi wao, iwe mahusiano ya kawaida ama wenza.
Mawasiliano ni moja ya misingi wa kushamiri/kuimarika kwa mahusiano ya wapenzi. Hivyo basi, simu imekuwa kifaa cha msingi kwa Wapenzi katika maisha yao ya kila siku hata ikiwa wanaishi pamoja. Wapenzi hutegemea simu zaidi katika kuwasiliana na kujulishana wapi, nini wanafanya, nini wanahitaji ama nini wanataka kuwasilisha haswa pale wasipokuwa pamoja.
Watu huzeeka umri na mwili, ila linapokuja suala la Mapenzi (being in love) tabia za vijana, watu wazima ama wazee hufanana kwa kiasi kikubwa kwa namna watakavyowasiliana na wapenzi wao iwe ana kwa ana au kwa simu. Tofauti huwa tu watu wazima (si wote), kuna busara huwa wanajiongeza katika baadhi ya maamuzi linapokuja suala la mahusiano ya Kimapenzi.
Simu zina faida nyingi sana, ila hapa tutajikita zaidi kwenye faida katika mawasiliano dhidi ya wapenzi na jinsi inavyoweza msaidia kila mmoja au wote kwa namna yake.
1. Mawasiliano ya mara kwa mara
Mara nyingi Wapenzi hawahitaji sababu ya msingi katika kuwasiliana. Mtu naweza akawa amemkumbuka tu mpenzi wake akaamua kumjulia hali, au kujua kama kala au kama siku yake inaenda vizuri. Simu imeweka wepesi wa kuwasiliana kila mara (ama pale inapobidi), mara nyingine hata kwa kutumia teknolojia inayoruhusu kuweza kumuona mwenzio wakati wa mawasiliano.
Mawasiliano ya mara kwa mara hustawisha mahusiano ya wapenzi na hata marafiki (ikumbukwe mara kwa mara ya kundi moja la wapenzi inaweza kuwa tofauti na kundi lingine la wapenzi) na pia kasi ya mawasiliano yanapoanza huwa ni tofauti pale mahusiano hayo yakikomaa, ingawa kuna wachache wamefaulu kuwa consistent.
Angalizo: Inapotokea kati ya wapenzi wawili mmoja akiwa anapenda mwenzie huku mwenzie akiwa 'anamchukulia poa' ama kujilazimisha katika hayo mahusiano; mawasiliano ya mara kwa mara hugeuka hitaji kwa upande mmoja na kero kwa upande mwingine. Kwa kiasi kikubwa, kama unampenda, unasukumwa kumtafuta mwenzio kila uwezapo (ingawa nayo ina mipaka, isizidi sana).
Mawasiliano kama Kipima joto cha Mahusiano
Faida nyingine ya Mawasiliano, ni msingi mzuri wa kupima hayo mahusiano yako una nafasi ipi na endapo yana uhai kiasi gani. Mawasiliano yanapokuwa ni sawa (mutual); wote mnatafutana, kujaliana na kutaka kuwasiliana sawa na hivyo huwa ni kheri kwa wapenzi hao. Ila inapotokea mawasiliano siku zote ni upande mmoja na huo upande mwingine ukikaa kimyaa ndo unapotea moja kwa moja, jua fika hapo hakuna kitu. Yaani hakutafuti, na kila atakapokutafuta anakuwa na shida, iwe ni mahitaji ya pesa, kukutana kimwili au msaada wowote ule, hapo ni wazi kwamba anakutumia.
Angalizo: Kutumika si wakati wote huwa kitu kibaya. Kuna wakati mtu anaweza akawa anakutumia ukajua anakutumia, ukapima ukaona huoni athari zozote za kutumika na mwisho wa siku una furaha katika hayo mahusiano una haki ya kuendelea kufurahia nje ya ukweli kuwa humaanisha ‘huoni thamani yako’. Na pia, kuna kujua unatumika, alafu wewe kumbe wamtumia kwa namna ambayo aidha anafahamu ama hafahamu na mwaridia kutumiana.
Kumsoma Mwenzio tabia
Simu imekuwa kifaa kizuri cha kuweza kutumia kumsoma mtu tabia. Kila binadamu ana mapenzi na misimamo yake, hilo linafanya misingi na vigezo ambavyo watu hutumia katika kuchagua watu wanaowafaa kuwa wapenzi wao kutofautiana. Je, hujui password yake ya simu au ni muoga sana wewe kugusa simu yake? Then, kwa kiasi kikubwa siyo lazima iwe na maana kuwa kuna mtu mwingine, ila ni kiashiria kizuri kuwa kwa namna moja ama nyingine hakuamini. Je, kila akiwa na wewe hawezi kuweka simu chini unless mnakutana kimwili? Inaweza kuwa hakueshimu, wewe na yeye hamna same interest za kufanya muongee au tu inaweza kuwa sababu ni tabia yako pia. Jinsi gani anawasiliaana na simu? Ana heshima/ustaarabu kwa watu anao wasiliana nao? Ni watu wa aina gani anawasiliana nao mara kwa mara? Hii yote hutoa picha nzuri ya kumwelewa mpenzi wako.
Angalizo: Simu ni kifaa cha mkononi maalum kwa ajili ya mtumiaji. Kuna tofauti ya kutaka kutumia simu ya mwenzio na kutaka kuipekua kila mara. Wenye tabia ya kupekua siku zote lazima upate ulichokuwa unakitafuta. Inaweza kuwa kitu kizuri au kibaya kutegemeana na malengo ya hiyo Taarifa ni nini.
Kwa upande mwingine, kama ambavyo simu huimarisha mahusiano ndiyo ambavyo inaweza haribu. Simu imekuwa na nafasi kubwa zaidi katika kubomoa kuliko hata kujenga tokana na watumiaji wamefanya kifaa hicho kiwafanye watumwa na kukosa weledi wa kutathmini pale wanapokuwa wamekosea.
Kuipa simu umuhimu zaidi. Mara kwa mara kutoka kusikiliza simu
Simu zimekuwa na uwezo wa kuhifadhi vitu vingi sana ambavyo ni msingi na mengine hata si msingi. Zaidi kuliko vyote ni ukuaji wa matumizi ya Mitandao ya Kijamii kama vile WhatsApp, Telegram, Instagram, Facebook, Twitter, Youtube na tovuti yetu pendwa ya JamiiForums.
Hivi vitu usipojiwekea muongozo na nidhamu ya matumizi ya simu, inaweza kukugeuza mtumwa katika Maisha yako mwenyewe. Changamoto moja wapo ya wengi walio kwenye mahusiano ni kuwa wakishazoeana 'wanachukuliana poa' kiasi cha kusahau wajibu na majukumu ya Kimahusiano kwa mpenzi wake, iwe katika kumpa attention, kumkabidhi mwili na akili inapobidi na hata tu kufanya mazungumzo ya kawaida ili kuelewa mwenzio siku imeendaje.
Kuruhusu simu zisizo na tija mida ambayo si sahihi
Moja ya kitu ambacho ni kero wakati wa faragha, ni kukatishwa starehe hio sababu tu simu inaita hapo na mwisho wa siku ikipokelewa unakuta ni mawasiliano ambayo kwa wakati huo hayakuwa na tija wala haraka. Kila wapenzi wanatakiwa kuweka misingi ya muda wao ‘us time’, muda wao ambao wanauhitaji kwa ajili yao tu. Bila kujalisha wanafanya nini, inapokuwa hakuna utaratibu wa kudhibiti simu (unless unatarajia simu za muhimu) inakuwa si haki kwa mwenzako. Kitendo cha kukatisha starehe au kupokea simu kila mara wakati wa faragha si haki na ni moja ya kero kubwa katika baadhi ya mahusiano.
Kuwa na simu moja pamoja na kazi
Kuna baadhi ya kazi zipo demanding na zinakuhitaji uwe unapatikana wakati wowote ule. Pia kuna kazi ambazo hazihitaji demand hiyo ila tu taratibu ni mbovu. Unapokuwa na simu ambayo ipo busy sana kikazi, ni vema kuwa na simu ya ziada (back-up phone) ambayo ni ya nyumbani tu, kwamba kila ukirudi nyumbani au kila unapokuwa na mwezio ama nyakati kama za weekend unaizima ili kutuliza akili na kumpa nafasi nzuri mwenza wako ukiwa umeweka kando kidogo masuala ya kazi ama marafiki.
Kupiga picha za utupu/uchi
Mapenzi ni matamu sana. Wangapi wamefanya vitu ambavyo wanakuja juta sababu tu ya mapenzi au mpenzi? Mapenzi hutufanya wakati mwingine kujisahau na kufanya baadhi ya vitu ambavyo usingeweza kufanya wakati huna hizo hisia (feelings) zinazopita damuni kwa wakati huo. Wapenzi wengi ambao wameachana na waliokuwa wapenzi wao na kujikuta walijipiga picha aidha kwa ajili ya kutuma au wakiwa wote, hubaki na majuto. Ni vema kutamaniana na kutazamana ili kufurahisha macho, nafsi na sehemu husika bila kuhusisha picha. Hili suala wahanga mara nyingi huwa ni wanawake, na tukiachilia mbali za kurekodiwa bila kujitambua, wengi huwa wanaridhia tokana na uaminifu ambao anakuwa nao kwa mwenzake. Kukubali kupiga picha ya ngono ni suala la kutathmini kwa kina kabla ya kufanya hivyo.
Kurekodi maongezi ya mwenzie
Kistaarabu, kum-rekodi mtu anapoongea inapaswa umtaarifu mhusika na aridhie kuwa unamrekodi. Nje ya applications ambazo hutumika kwenye simu (haswa wa android) wakati wa kuongea, kuna wapenzi ambao mara nyingi kwa nia ‘ovu’ ya kutaka kumchafua au kumharibia mwenzie, inaweza ikatokea akamtega mhusika kwa kuhakikisha wataongea kile wanachotaka kurekodi na kisha waka rekodi.
Hii mara nyingi hutumika wa wachepukaji (pengine kupeleka kwa mpenzi mwingine kutaka ku prove hoja fulani), mashushushu (pale wanapokuwa wameingia kwenye mahusiano kwa lengo mahususi), mchepushwaji na yule ambaye hutaka aje aitumie kumhujumu pale watakapoachana. Ogopa sana mpenzi ambaye anaweza kukurekodi bila ridhaa na kwa siri, iwe sauti ama video.
Ku hack (install) apps za kumfuatilia (Kupekua)
Hili ni suala ambalo watu wengi wanatamani wangekuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwenye simu za wapenzi wao. Na hii mara nyingi ni pale ambapo nyenendo na tabia hubadilika ukifananisha na huko nyuma katika mahusiano hayo. Hili suala linaweza kukuvutia sana, ila siyo mwarubaini wa kutatua lolote hilo linalowasumbua katika mahusiano zaidi ya kujenga ubovu zaidi. Binadamu wana tabia ya kuchokana, inaweza ikawa bora ukaachia ngazi au mpa nafasi (space) na ukatumia muda huo kujitathmini na kuangalia kile kilicho bora kwako.
Kwa upande wa wanawake, wengi wanapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi malengo na juhudi za kuwafanya wawe bora Zaidi na kuwa na mafanikio Zaidi kupungua. Kuna wakati mahusiano yakiisha huwa kheri kwao ingawa si wakati wote.
Kutokariri namba ya Mpenzi wako
Ni vigumu kukarili namba za watu za simu, ila inashauriwa kuwa walau na nambari 3 hadi 5 ulizokumbuka kichwani ili kuweza kuzitumia wakati wa dharura kama vile uwe umekwama mahala na wahitaji mawasiliano ya haraka. Ikiwa katika hizo namba unazokumbuka ya mwenzio haipo kichwani, ni kiashiria kikubwa kwamba si mtu wako wa muhimu kama inavyostahili.
Unless hiyo namba yake ni Mpya bado. Inaweza kuchukuliwa kwa wepesi sana, ila jiulize, kama mpenzi wako (tena wa muda mrefu) anajua namba kadhaa kichwani, na yako haijui inaweza kuwa na maana gani? Hili jibu kila mmoja analo.
Kutojibu ujumbe au kupiga simu (return call) kwa wakati
Kuna wakati inaweza kutokea ukatuma/ukatumiwa ujumbe kwa mpenzi wako au ukapiga/akapiga na asiwe kajibu mara moja. Kinachofuata hapo ni mhimu katika ustawi wa mawasiliano. Kuna wapenzi wana tatizo sugu la kutokuwa wazuri katika mawasiliano kwa sababu mbali mbali.
Sababu tatu za msingi huwa
(a) Ni mtu yupo busy sana na majukumu si mtumiaji wa simu hadi inapobidi,
(b) Ni mtu simu yake ipo busy sana kiasi kwamba anachoka kuna wakati anaamua kutotilia simu yake maanani
(c) Ni mtu ambaye hajali au kuchukulia poa na kutoona umuhimu wa kukojibu ama kukupigia kwa sababu zozote zile alizonazo
Sababu ikiwa (a) ama (b) ni muhimu kumwelewa mwenzio anapokuwa kachelewa, ila pale inapokuwa wazi mwenzio anapenda sana simu na popote alipo hawezi kukaa bila kuishika na kutumia simu yake na kila akiwa na wewe ana simu mkononi ila asipokuwa na wewe ndiyo ana sababu lukuki za kutoona ujumbe hapo kuna walakini.
Moja ya njia ya kutatua tatizo la mawasiliano na kuhakikisha ume customize milio ya text ana simu za mpenzi wako ama watu wa karibu ambao mawasiliano nao ni msingi. Ukiwa na mlio tofauti inakusaidia pale akikutafuta kupokea ama kujibu kwa wakati.
Kupokea simu ya mwenzio
Simu ya mkononi ina mmiliki mmoja katika matumizi yake (tofauti na simu zinazowekwa nyumbani kwa matumizi ya pamoja). Kupokea simu ya mpenzi wako inapoita bila ridhaa yake, au kama hamjakubaliana ni makosa.
Kuna baadhi ya wanawake na hata wanaume wakiona namba ambayo ni ngeni na kwa hisia tofauti au kujisikia kutokuwa na imani na hiyo simu watapokea hiyo simu na kumuhoji, kumkaripia au kum harass mpigaji wa simu bila kujua aliyepiga simu ni nani. Kuna mifano katika jamii ambayo baadhi ya watu wapenzi wao waliwahi kutukana mabosi au wafanyakazi wenzao. Kuna wale ambao wanaweza wasipokee ila wakachukua hiyo namba na kutuma meseji za vitisho au matusi kwa wahusika kwa njia moja ama nyingine.
Angalizo: Kuna tofauti ya kupokea simu ya mtu ambaye tayari wamjua ikiwa mwenzako hayupo kwenye nafasi nzuri ya kupokea, na pia kuna wakati namba inaweza ikiwa imepiga sana ukahisi ni dharula na ukaipokea kumpa ujumbe mpigaji wapige wakati mwingine au wasubiri na mwenye simu kutokuwa karibu. TAFADHAILI kama mahusiano yenu si ya kikazi au ki ndoa na ni ya kimchepuko ni marufuku kabisa kuipokea.
Ushauri
Heshima ni msingi mkubwa katika mawasiliano, na heshima huonyweshwa vema kwa vitendo na si maneno. Kama binadamu, kuna wakati inaweza tokea ukajikuta umejisahau sana katika mahusiano, na kujisahau mara nyingi hutokana na wapenzi hao kubweteka (wanawke kwa wanaume). Akishajua ama kuridhia kuwa huyo mwanaume ama Mwanamke ni wake hata iweje, wengine anaacha kufanya Jitihada za kumvutia, kumfurahisha, kum surprise au tu kuleta shamrashamra za ziada katika mahusiano kiasi kwamba inafika wakati watu wachachokana na kujikuta mbadala ukawa ni simu.
Simu ni suala la kutathimini kwa karibu, imekuwa ni kigezo kikubwa cha mahusiano mengi kuharibika na hata kuvunjika. Ni vema kujiuliza, ni kitu gani unafanya katika simu ambacho mwenzio akijua au kuona kitamuumiza? Je, kinastahili (is it worth it?), Je una haja ya kuacha jumbe ambazo zinamvunjia heshima mwenzio kwa namna moja ama nyingine? Na je kuna lolote au namna yoyote unayowasiliana na baadhi ya watu inayoweza kuhatarisha mahusiano yako? Weka mazoea ambayo yatalinda mahusiano yako ya Kimapenzi (kama ni ya mhimu kwako). Ni bora kuepuka kufanya kile ambacho hutotaka kwa namna yoyote ile mwenzio akufanyie.
Simu na matumizi yake imekuwa sehemu nyeti sana, nadhani imefika wakati mapema kabisa katika mahusiano, kujadili kama wapenzi misingi mizuri ya mawasiliano ambayo mtakubaliana na kufika katikati (compromise) ili kila mmoja awe na amani. Ila muhimu kuliko yote ili kulinda mahusiano yenu.
Angalizo: Huu ni mtazamo na maoni yangu binafsi, inaweza tukawa tunaona tofauti, tafadhali shirikiana na mimi kujadili hoja hii kwa kina.
Unaweza kusoma sehemu ya kwanza hapa:
Simu za mikononi katika Mahusiano | Mwenendo wa Walezi/Wazazi kwenye familia
Simu ni moja ya kifaa cha msingi katika maisha yetu ya kila siku, ndiyo inatuunganisha kirahisi pale tunapokuwa hatupo katika uwepo wa wale tunaotakiwa kuwasiliana nao. Zaidi ya kuweza kuendesha maisha yetu kijamii na kikazi, simu ina uwezo wa kuboresha mahusiano kama ambavyo ina uwezo mkubwa wa...
www.jamiiforums.com
Mahusiano ni sehemu mhimu na nyeti katika maisha ya kila siku ya binadamu. Mahusiano ya Kimapenzi yana nafasi kubwa katika kuathiri au kushamirisha mienendo za kibinadamu katika maisha yetu ya kila siku, iwe katika utendaji wa kazi, maamuzi ya msingi katika maisha ya kila siku, mikakati/mipango kwa ujumla na maeneo mengine mengi.
Mahusiano ya kimapenzi ni sehemu muhimu kwa wanadamu wengi, bila kujalisha ni kijana ama mzee, mwanamke au mwanaume, mlemavu au mzima, wote huwa ama hutamani kuwa na watu ambao wana nafasi kubwa katika maisha kama wapenzi wao, iwe mahusiano ya kawaida ama wenza.
Mawasiliano ni moja ya misingi wa kushamiri/kuimarika kwa mahusiano ya wapenzi. Hivyo basi, simu imekuwa kifaa cha msingi kwa Wapenzi katika maisha yao ya kila siku hata ikiwa wanaishi pamoja. Wapenzi hutegemea simu zaidi katika kuwasiliana na kujulishana wapi, nini wanafanya, nini wanahitaji ama nini wanataka kuwasilisha haswa pale wasipokuwa pamoja.
Watu huzeeka umri na mwili, ila linapokuja suala la Mapenzi (being in love) tabia za vijana, watu wazima ama wazee hufanana kwa kiasi kikubwa kwa namna watakavyowasiliana na wapenzi wao iwe ana kwa ana au kwa simu. Tofauti huwa tu watu wazima (si wote), kuna busara huwa wanajiongeza katika baadhi ya maamuzi linapokuja suala la mahusiano ya Kimapenzi.
Faida ya Simu kwa Wapenzi
Simu zina faida nyingi sana, ila hapa tutajikita zaidi kwenye faida katika mawasiliano dhidi ya wapenzi na jinsi inavyoweza msaidia kila mmoja au wote kwa namna yake.
1. Mawasiliano ya mara kwa mara
Mara nyingi Wapenzi hawahitaji sababu ya msingi katika kuwasiliana. Mtu naweza akawa amemkumbuka tu mpenzi wake akaamua kumjulia hali, au kujua kama kala au kama siku yake inaenda vizuri. Simu imeweka wepesi wa kuwasiliana kila mara (ama pale inapobidi), mara nyingine hata kwa kutumia teknolojia inayoruhusu kuweza kumuona mwenzio wakati wa mawasiliano.
Mawasiliano ya mara kwa mara hustawisha mahusiano ya wapenzi na hata marafiki (ikumbukwe mara kwa mara ya kundi moja la wapenzi inaweza kuwa tofauti na kundi lingine la wapenzi) na pia kasi ya mawasiliano yanapoanza huwa ni tofauti pale mahusiano hayo yakikomaa, ingawa kuna wachache wamefaulu kuwa consistent.
Angalizo: Inapotokea kati ya wapenzi wawili mmoja akiwa anapenda mwenzie huku mwenzie akiwa 'anamchukulia poa' ama kujilazimisha katika hayo mahusiano; mawasiliano ya mara kwa mara hugeuka hitaji kwa upande mmoja na kero kwa upande mwingine. Kwa kiasi kikubwa, kama unampenda, unasukumwa kumtafuta mwenzio kila uwezapo (ingawa nayo ina mipaka, isizidi sana).
Mawasiliano kama Kipima joto cha Mahusiano
Faida nyingine ya Mawasiliano, ni msingi mzuri wa kupima hayo mahusiano yako una nafasi ipi na endapo yana uhai kiasi gani. Mawasiliano yanapokuwa ni sawa (mutual); wote mnatafutana, kujaliana na kutaka kuwasiliana sawa na hivyo huwa ni kheri kwa wapenzi hao. Ila inapotokea mawasiliano siku zote ni upande mmoja na huo upande mwingine ukikaa kimyaa ndo unapotea moja kwa moja, jua fika hapo hakuna kitu. Yaani hakutafuti, na kila atakapokutafuta anakuwa na shida, iwe ni mahitaji ya pesa, kukutana kimwili au msaada wowote ule, hapo ni wazi kwamba anakutumia.
Angalizo: Kutumika si wakati wote huwa kitu kibaya. Kuna wakati mtu anaweza akawa anakutumia ukajua anakutumia, ukapima ukaona huoni athari zozote za kutumika na mwisho wa siku una furaha katika hayo mahusiano una haki ya kuendelea kufurahia nje ya ukweli kuwa humaanisha ‘huoni thamani yako’. Na pia, kuna kujua unatumika, alafu wewe kumbe wamtumia kwa namna ambayo aidha anafahamu ama hafahamu na mwaridia kutumiana.
Kumsoma Mwenzio tabia
Simu imekuwa kifaa kizuri cha kuweza kutumia kumsoma mtu tabia. Kila binadamu ana mapenzi na misimamo yake, hilo linafanya misingi na vigezo ambavyo watu hutumia katika kuchagua watu wanaowafaa kuwa wapenzi wao kutofautiana. Je, hujui password yake ya simu au ni muoga sana wewe kugusa simu yake? Then, kwa kiasi kikubwa siyo lazima iwe na maana kuwa kuna mtu mwingine, ila ni kiashiria kizuri kuwa kwa namna moja ama nyingine hakuamini. Je, kila akiwa na wewe hawezi kuweka simu chini unless mnakutana kimwili? Inaweza kuwa hakueshimu, wewe na yeye hamna same interest za kufanya muongee au tu inaweza kuwa sababu ni tabia yako pia. Jinsi gani anawasiliaana na simu? Ana heshima/ustaarabu kwa watu anao wasiliana nao? Ni watu wa aina gani anawasiliana nao mara kwa mara? Hii yote hutoa picha nzuri ya kumwelewa mpenzi wako.
Angalizo: Simu ni kifaa cha mkononi maalum kwa ajili ya mtumiaji. Kuna tofauti ya kutaka kutumia simu ya mwenzio na kutaka kuipekua kila mara. Wenye tabia ya kupekua siku zote lazima upate ulichokuwa unakitafuta. Inaweza kuwa kitu kizuri au kibaya kutegemeana na malengo ya hiyo Taarifa ni nini.
Kwa upande mwingine, kama ambavyo simu huimarisha mahusiano ndiyo ambavyo inaweza haribu. Simu imekuwa na nafasi kubwa zaidi katika kubomoa kuliko hata kujenga tokana na watumiaji wamefanya kifaa hicho kiwafanye watumwa na kukosa weledi wa kutathmini pale wanapokuwa wamekosea.
Makosa ambayo Wapenzi hufanya kuhusiana na Simu kwa Wapenzi wao