Simu bora kwa laki 5 au 6

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,788
6,570
Nataka simu bora kwa charge, speed, net work had 5 G, picha nuzri sana kwa sh laki 5 au 6. Nomba ushauri
 
Chukua Infinix Note 12 hutajutia... check specs zake hapa chini..
 
Kwa budget hiyo huwezi kupata simu zenye majina makubwa yenye specification za kuridhisha labda ukanunue refurb za miaka mitatu nyuma nenda kwa hizi kampuni za kichina utapata simu mpya kali yenye feature za kisasa kwa 600k Redmi, Vivo, oppo, infinix, Realme
 
Chukua Nokia X10.
Nunua pepsi bariiidi, anza kuvuta fundo huku unaifanyia cofiguration simu yako mpya
 
Chukua Infinix Note 12 hutajutia... check specs zake hapa chini..
Yaani mtu atoe laki ananunue haya matakataka ya tecno, infinix sijui nini, huu utakuwa ni ujuha.

Mbona Samsung wana mida range nzuri tu, bado kuna google, Iphone refurb n.k
 
Nataka simu bora kwa charge, speed, net work had 5 G, picha nuzri sana kwa sh laki 5 au 6. Nomba ushauri
Mkuu Samsung Galaxy A33 5G inakidhi haya mahitaji. Ina 5G, battery nzuri, camera. Issue yake ni kwamba mtaani bei ni laki 7 (ambazo naziona online) pengine ukizunguka vizuri unaweza pata laki 6 ama 6 na nusu.

Sababu 5G imeishaingia TZ ni vyema kununua simu yenye 5G na band za kutosha A33 ina band nyingi sana kwa midrange

1, 3, 5, 7, 8, 20, 28, 38, 40, 41, 66, 78 SA/NSA/Sub6

Kwetu sisi tuna band hizi ambazo TCRA wameuza
2300 ama 40
2600 ama 38
3500 ama 78
700 ama (12 au 28)

Hapo sina uhakika kwenye hio 700 kama 700 yetu ni 12 ama 28 kama ni 28 ina maana ukiwa na A33 uhakika mtandao wowote ukitoa 5G kipindi cha karibuni simu yako inashika.

Hata kama hutanunua A33 hakikisha hio simu ina hizo bands.
 
Jamani kwa laki 5 naweza PATA simu Gani nzuri ya specifications nilizosemahapo juu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom