Yanga inafanya mkutano na waandishi wa Habari muda huu, fuatilia hapa kitakachojiri
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick amekiri uwepo wa kesi hiyo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Baraza la wadhamini wa Yanga SC ambapo ilisikilizwa upande mmoja na kupelekea kutolewa hukumu ya Julai August 2, 2023.
Aidha, mwezi wa 6 mwaka huu, Yanga SC ilipata taarifa ya ombi la Mahakama kutaka uongozi wote utoke madarakani, ambapo Eng. Hersi aliekekeza idara ya sheria kufuatilia suala hili na kugundua kuwa kesi hii iliendeshwa upande mmoja, pia waligundua kughushiwa kwa saini za wajumbe wa bodi ya Baraza la wadhamini. Pia, waligundua uwepo wa kundi la watu nyuma ya wazee hao linalotumika kuvuruga amani ya Yanga hivyo kwa kutumia vyombo vya dola wanashughulikia suala hili.
Kwa hatua ya sasa, Yanga imepekela maombi ya kuomba kuongezewa muda wa mapitio ya hukumu na kesi hiyo sababu hawakushirikishwa tangu awali, kwakuwa watu walioshiriki awali hawakuwa na uhalali kisheria (hawakuwa watu sahihi pia walifoji saini za wajumbe wa bodi ya Baraza la wadhamini)
Pia, itapeleka ombi la kuzuia utekelezaji wa hukumu hiyo ili uongozi usiondolewe pamoja na kuzuia wazee wasikabidhiwe timu kwa sasa.
Wakili Simon amesema Yanga itafungua kesi ya Jinai kwa wahusika wote waliopeleka kesi hii mahakamani kwani walighushi saini za wajumbe wa bodi ya Baraza la wadhamini wa Yanga.
Pia soma:
1. Hii hapa Hukumu ya kutotambulika kwa Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga. Yumo Mwigulu, Mwambe na Tarimba
2. Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!