Simiyu: Mkuu wa Mkoa athibitisha kifo cha Mtu mmoja katika Maandamano ya Busega

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,452
13,070
Meshaki Daudi (20) mkazi wa Kitongoji cha Makanisani Kata ya Lamadi, wilayani Busega Mkoani Simiyu, amefariki kwa kudaiwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi, lililokuwa katika oparesheni ya kudhibiti maandamano ya wananchi walioandamana katika kituo cha polisi Lamadi, yaliyokuwa yanashinikiza serikali na jeshi la polisi kudhibiti matukio ya watoto kupotea.

Pia soma: Simiyu: Wananchi wavamia Kituo cha Polisi wakidai kuna matukio mengi ya Watoto kupotea

Meshaki Daudi ni muhitimu wa kidato sita katika shule ya sekondari Loliondo, iliyopo mkoani Arusha mwaka huu umauti, umemfika pindi akiwa anasubiri kwenda chuo kikuu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi, amethibitisha kifo cha kijana huyo.

Pia soma: Serikali kugharamia mazishi ya kijana Meshack Daudi Paka aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwenye maandamano ya Simiyu
 
Meshaki Daud (20) mkazi wa Kitongoji cha Makanisani Kata ya Lamadi, wilayani Busega Mkoani Simiyu, amefariki kwa kudaiwa kupigwa risasi na Jeshi la Polisi, lililokuwa katika oparesheni ya kudhibiti maandamano ya wananchi walioandamana katika kituo cha polisi Lamadi, yaliyokuwa yanashinikiza serikali na jeshi la polisi kudhibiti matukio ya watoto kupotea.

Meshaki Daudi ni muhitimu wa kidato sita katika shule ya sekondari Loliondo, iliyopo mkoani Arusha mwaka huu umauti, umemfika pindi akiwa anasubiri kwenda chuo kikuu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi, amethibitisha kifo cha kijana huyo.


USSR
 
DUH! R.I.P. Policcm kwa kuua vijana wa chuo hawajambo
Namkumbuka Akwilina aliyekuwa anaenda kuripoti field,wajamaa wakampiga risasi
 
Nimeona hii habari ITV, inasikitisha sana, wanawake waliandamana kwa amani kuhusu hatma ya watoto kupotea majibu yao wamejibiwa kwa kuuliwa kijana mwingine mdogo, hii inamaanisha nini? Haki iko wapi ndani ya serikali inayojinasibu inasikiliza wanyonge? Amani iko wapi Tanzania!? Watoto wetu tuwafiche wapi?

R.I.P Kijana mzuri, waliokusababishia ndoto zako kuzimika watalipia wao na kizazi chao
 
Hivi ile style ya kumshukuru mama imeishia wapi?
Haya mitano tena kwa mama
 
Hivi hawa form four failure wana manawaza kwa kutumia makalio ama nini?watu wanaandamana kwa nini kutumia risasi za moto?
 
Hivi ile style ya kumshukuru mama imeishia wapi?
Haya mitano tena kwa mama
Naona hii serikali sasa kama imepoteza dira watu wanaadamana hawana silaha kwa nini police wabebe masilaha ,tuliona maandamano ya ubagu
zi uingereza lakini hakuuwawa hata mtu moja hapa serikali lazima ichukuwe hatua la kwanza masauni awajibike aidha awajibishwe na mkuu wa polisi awajibishwe pia madudu yamezidi jeshi la polisi.
 
Back
Top Bottom