Simiyu: Baadhi ya Wananchi Busega wadai Askari Polisi waliwaibia na kuwapiga Watu hata ambao hawakushiriki maandamano

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,631
6,294

Baadhi ya Wananchi Wakazi wa Kata ya Lamadi, Wilayani Busega wamedai baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi walishiriki kuwapiga na kuwapora fedha Watu wakati wa zoezi la kuwadhibiti Waandamanaji eneo hilo, Agosti 21, 2024.

Wamesema hayo Agosti 29, 2024 katika Mkutano wa Hadhara ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenan Kihongosi akilenga kusikiliza kero mbalimbali, ambapo wamedai Askari hao walivamia hata Watu ambao hawakuhusika katika Maandamano hayo wakawapiga na kuwapora fedha zao.

Akitoa tamko la Serikali, Kihongosi amesema “Changamoto kuhusiana na Jeshi la Polisi mlizozisema tutachukua hatua, hakuna aliye juu ya Sheria, kama kuna uzembe waliufanya Viongozi wetu tutachukua hatua bila kumuonea huruma Mtu wala hatutamlinda Mtu.”

Chanzo: ITV


RC KIHONGOSI: WANANCHI LAMADI MSIKUBALI KUTUMIKA KISIASA,DUMISHENI AMANI,PENDANENI KWA UTU WENU.

Busega,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenan Laban Kihongosi amewataka Wananchi wa Kijiji cha Lamadi Wilayani Busega kutokubali kutumika kisiasa na baadhi ya Wanasiasa wanaotanguliza maslahi yao binafsi na badala yake kujikita katika kulinda Amani na utulivu.

Mhe Kihongosi ametoa rai hiyo katika Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Lamadi aliouitisha kwa lengo la kusikiliza changamoto mbalimbali za Wananchi hao pamoja na kuwapa Elimu kuhusu umuhimu wa kulinda Amani.

"Pendaneni kwa utu wenu,mkifa hamtazikwa na Vyama vya Siasa ,mtazikwa na Wanalamadi hapa ndo kwenu,wee unatanguliza maslahi ya kisiasa mbele kuliko hata ukoo wako,Siasa tu."Alisema Mkuu wa Mkoa Kihongosi.

Amani na utulivu vimerejea katika eneo la Lamadi baada ya jitihada mbalimbali za Viongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa kumaliza sintofahamu iliyojitokeza siku chache zilizopita kufuatia baadhi ya Wananchi wa Eneo Hilo kufanya vurugu na kutishia kuvamia kituo cha Polisi.

GCO,
Simiyu -RS
28 Agosti ,2024.


Pia soma:
~ Simiyu: Mkuu wa Mkoa athibitisha kifo cha Mtu mmoja katika Maandamano ya Busega
~ Simiyu: Wananchi wavamia Kituo cha Polisi wakidai kuna matukio mengi ya Watoto kupotea
 
Back
Top Bottom