Similarities between CCM vs Zanu-PF and Magufuli vs Mugabe

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,808
48,968
Robert Gabriel Mugabe (1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU-PF. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe.

Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.

Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kulipiza kisasi kwa kuwaua na kuwatesa watu wa kabila la wa-Ndebele ambao mji wao mkubwa ni Bulawayo, mwanzo ilijulikana walikuwa wanauawa na watu wasiojulikana lakini baadaye yakawa mauaji ya halaiki ya wazi.

Tume ya kanisa katoliki kuhusu haki na amani ilitoa ripoti iliyodai kwamba zaidi ya watu 20,000 waliokuwa wanamuunga mkono Joshua Nkomo na wapinzani walipoteza maisha yao.

1983 Nkomo alikimbilia uhamishoni London baada ya wafuasi wake kumtuhumu kukiunganisha chama chake cha ZAPU na ZANU cha Mugabe na kuunda ZANU-PF, kama TANU na ASP zilivyoungana kuunda CCM.

Kuanzia enzi hizo hadi leo raisi Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu akitumia vyombo vya dola hasa jeshi la polisi ikiwezekana kufuta matokeo akiona anaelekea kushindwa.

Mabadiliko ya katiba ya mwaka 1998 yalisababisha kuanzishwa kwa chama kipya cha Movement for Democratic Change (MDC) chini ya kiongozi wake Morgan Tsvangirai na mwaka 2000 kilishiriki uchaguzi wa rais. Baada ya uchaguzi Tsvangirai alikamatwa kwa kosa la uhaini akituhumiwa kutaka kumuua Mugabe baadae 2004 aliachiwa kwa kukosekana ushahidi kama viongozi mbalimbali wa upinzani hapa wanavyokamatwa kwa uchochezi baadaye kuachiwa kwa kukosa ushahidi.

Baada ya uchaguzi huo wa 2000 uvunjaji wa haki za binadamu uliongezeka maradufu, mateso na manyanyaso dhidi ya wapinzani na wakosoaji wa serikali yamekuwa yakiripotiwa. Ni katika kipindi hicho Mugabe alianzisha mabadiliko ya sera ya Ardhi ambapo wazungu na wapinzani walinyang'anywa ardhi bila fidia kama inavyotokea leo Tanzania. Ilifikia hatua hadi ya nchi za Magharibi zikaiwekea Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi.

Mabadiliko hayo ya kiuchumi yaliyofanywa na Mugabe yaliishangaza dunia na kusababisha uchumi wa nchi hiyo kushuka hadi leo, hakusikia wala kujali ushauri wa kiuchumi alikuwa akipewa.

Watu walidhulumiwa mali zao, haki za binadamu zilikiukwa kwa kisingizio cha maendeleo, makampuni mengi hasa ya wazungu yalifunga biashara zao hali ambayo leo inaonekana hata Tanzania kwa makampuni kufunga biashara zao.

Katika kipindi hicho vifo vingi viliripotiwa na wapinzani kukamatwa mara kwa mara, mfano.

May 2003 ijumaa jioni Tsvangirai alikamatwa mara baada ya kufanya press conference, akituhumiwa kufanya uchochezi kwa serikali.

Tarehe 11 March 2007 Tsvangirai alikamatwa tena akielekea kanisani, iliripotiwa kuwa alipigwa sana na kuteswa na kikosi maalumu cha polisi. Aliumizwa kichwani machoni na hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kumuona zaidi ya mke wake. Mpiga picha wa Zimbabwe Edward Chikombo aliyefanikiwa kupata picha zake na kuzionyesha hadharani muda mfupi aliripotiwa kuvamiwa akiwa nyumbani kwake na kuuawa.
436262391_2f129b050a_m.jpg


Kwenye uchaguzi wa 2008 Iliripotiwa na vyombo mbalimbali kuwa Morgan Tsvangirai kutoka chama cha MDC-T alishinda kwa 47.8% huku Mugabe akipata 43.2% uchaguzi uliofutwa na kusababisha vurugu kubwa ambapo wafuasi zaidi ya 200 waliuawa.

Katika utawala wake matukio mbalimbali ya kukamatwa wapinzani na wakosoaji wa Mugabe yameripotiwa, watu walioonekana kusaidia upinzani walifunguliwa kesi na wengine ama kupotea au kufungwa jela.

March 2009 Tsvangirai alinisurika kifo baada ya gari lake kugongana uso kwa uso na gari jingine ambapo mke wake, Susan Tsvangirai, aliuawa kwa ajali iliyojulikana kama ya kupangwa.

Hadi tunakwenda hewani (leo) chama chake cha Zanu-PF kimemuomba Mugabe kuondoka mwenyewe (kujiuzulu) au chama kimuondoe kwa nguvu.
 
Natamani Tundu Lisu angekua Zimbabwe Ili ajifunze siasa za upinzani
 
Leo mtamfananisha na Mugabe,Kesho mtasema ni rafiki wa Kagame mtamfananisha naye tena,keshokutwa mtasema ni kama Museveni,wiki ijayo mtakuja na kusema yupo kama Raila Odinga kwa kuwa ni rafiki yake...

Mnabaki kufanya comparison tuu,hamtafuti the source ya kusolve the problem,tuacheni yao tufocus yetu. juzi mlijitoa ufahamu mkaangukia upande wa Kenyatta mkaampambaaa weeee leo kafanya nini??mulemule tuu kama wengine,msiridhishwe na wengine wamefanya nini wanasababu zao za kufanya hivyoo na nyie fanyeni kwa nafasi yenu kulingana na sababu zenu/situations zenu.
 
Natamani Tundu Lisu angekua Zimbabwe Ili ajifunze siasa za upinzani

Hapo mleta mada ameweka kisu kwenye mfupa, natabiri huu uzi kufutwa au kufikia page zaidi ya 20 kufikia kesho mchana. Na nyie mtalazimishwa kujibu mapigo ili kuhakikisha mnapoteza hoja kuu kwani hii post imekaa vibaya na imebeba mfanano mkubwa.
 
Yawezekana CCM na Zanu PF wanafanana kwasababu vyote ni vyama dola na vinaogopa mageuzi! Lakini Mugabe na Magufuli hawa ni watu tofauti kabisa! Mugabe akiwa msomi na exposure kubwa ameivuruga Zimbabwe ktk hali ya kutia aibu kwa misimamo ya kijinga jinga! Magufuli ni mtawala mwenye exposure sifuri na hajui siasa wala siyo mtawala. Haishangazi Tz inaanza kurudi nyuma!
 
Mugabe Hana Ukomo wa madaraka
Mbowe Hana Ukomo wa madaraka

Nguvu ya Grace ndani ya ZANU PF Ni sawa na Nguvu ya Madam Wema Sepetu ndani ya Chadema baada ya kumpiku Madam Joyce Mukya!

Umejitahidi kujibu kwa propaganda lakini post mama bado ina nguvu na kubeba uhalisia kwa 90%. Umejaribu mpaka kuleta mfano mfu ili kutoa watu kwenye uzi husika lakini ukweli uko wazi. Kajipange urudi jamaa amaongea ukweli ambao ni hatari hata kwake mwenyewe.
 
Umejitahidi kujibu kwa propaganda lakini post mama bado ina nguvu na kubeba uhalisia kwa 90%. Umejaribu mpaka kuleta mfano mfu ili kutoa watu kwenye uzi husika lakini ukweli uko wazi. Kajipange urudi jamaa amaongea ukweli ambao ni hatari hata kwake mwenyewe.
Usinpangie cha ku post
Ushamba ni kutaka Unavyowaza Wewe ndio
Wote tuwaze hivyo

Wapuuzi wenzio walihamasishana
Wahame humu JF wakahamia Mwanahalisi forums, unajua Kwanini ilikufa natural death? Jibu ni kuwa walikutana Wenye Mawazo yanayofanana ikakosa ladha!

Ladha ya JF ni haya Mawazo tofauti, hata Kama Wewe ni Mshamba wa Demokrasia ya Uhuru wa Mawazo jifunze kutambua uwepo wa Hali hiyo
 
Umesahau kitu.. Mwanzoni wakat uchumi unaanza kuporomoka Jamaa alikuwa akiwaambia wananch wa zimbabwe kwamba uchumi unakua na anapigana kulinda maslahi ya zimbabwe dhid ya mabepari mwisho wa siku mambo yakaja kuonekana hadharan sasa sijui iyo inaendana na huku kwetu au vp
 
Usinpangie cha ku post
Ushamba ni kutaka Unavyowaza Wewe ndio
Wote tuwaze hivyo

Wapuuzi wenzio walihamasishana
Wahame humu JF wakahamia Mwanahalisi forums, unajua Kwanini ilikufa natural death? Jibu ni kuwa walikutana Wenye Mawazo yanayofanana ikakosa ladha!

Ladha ya JF ni haya Mawazo tofauti, hata Kama Wewe ni Mshamba wa Demokrasia ya Uhuru wa Mawazo jifunze kutambua uwepo wa Hali hiyo

Sipingi mawazo yako kwani una hoja nzuri ila naziboresha, usisahau jazba nayo ni sehemu ya demokrasia. Hii kasi uliyokuja nayo niliitarajia sana. Ushauri wangu kwako, kaa tulia, kunywa maji kisha endelea na huu uzi usikie unayopenda na usiyopenda ila uvumilivu utakusaidia zaidi kwa uzi wa aina hii.
 
Sipingi mawazo yako kwani una hoja nzuri ila naziboresha, usisahau jazba nayo ni sehemu ya demokrasia. Hii kasi uliyokuja nayo niliitarajia sana. Ushauri wangu kwako, kaa tulia, kunywa maji kisha endelea na huu uzi usikie unayopenda na usiyopenda ila uvumilivu utakusaidia zaidi kwa uzi wa aina hii.

Hii ndio comment ya kidemokrasia sio kuzuia Watu Eti nataka kuharibu Uzi, kwani tupo hapa kupamba Mawazo ya alieleta mada?
Uachage Ushamba kila usichokikubali kukiita Propaganda au Mtu akiwaza tofauti Eti anataka kuharibu Uzi !
 
Hii ndio comment ya kidemokrasia sio kuzuia Watu Eti nataka kuharibu Uzi, kwani tupo hapa kupamba Mawazo ya alieleta mada?
Uachage Ushamba kila usichokikubali kukiita Propaganda au Mtu akiwaza tofauti Eti anataka kuharibu Uzi !

Yap hiyo dawa niliyokupa naona imepenya pazuri, naona sasa hata ile jazba imeshuka sana ndio maana umechangia bila yale maneno ya jazba na mihemko mara sijui wapuuzi wenzio, mara kuhamia mwanahalisi forum na lugha kama hizo. Karibu kwa mjadala.
 
Mh! naona kuna harufu ya ukweli apa.Ila chadema nao walibugi sana kumkaribisha lowasa kuwa mgombea leo wamenyanganywa sera pia dr slaa naye kabugi sna kuidhamisha ukawa bora angetulia maana leo ataushauri angeombwa nakuheshimika pia.
 
Back
Top Bottom