Daniel Mbega wewe ni muandishi mkongwe wa habari hususan habari za michezo na burudani, tukikufahamu ukiwa pale Business Times miaka mingi mpaka hata sasa sijui u wapi. Naamini una uzoefu na weledi wa kutosha katika kuandika habari, hata hivyo nachelea kusema habari uliyoiweka haijakaa kiweledi. Habari haiwezi kuanza kwa licha ya..... maana matokeo ya mechi ya Coastal Union na Azam hayafahamiki na hayatabiriki. Pili ungepiga hesabu zako utagundua Simba wana goal difference ya 24 na Azam wana goal difference ya 21, hivyo Azam watalazimika kushinda kwa zaidi ya tofauti ya magoli matatu ili waipiku Simba jambo ambalo uwezekano wake waujua moyoni mwako. Tatu Simba kwa sasa imeshinda mechi sita Mfululizo na sio tatu, Walishinda na Mtibwa 1-0, Ruvu JKT 0-2, African Sports 4-0, Mgambo JKT 5-1, Kagera Sugar 0-1 na Stand United 1-2.
Unaandika habari JF as if unataka kuuza gazeti kama kawaida ya title zenu zinazoboa na na za kinazi? Be professional banaa, wewe mkongwe sana katika tasnia yako.