Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 1,746
- 5,890
Nawapongeza Simba Kwa ushindi dhidi ya Stellenbosch wa goli moja Kwa bila. Sijui ni kutokuelewa matokeo ya Sola au ni ushabiki uliopitiliza.
Mashabiki wengi wa Simba ni kama hawajaridhika hivi Kwa goli moja bila na kosakosa kibao.
Lakini mchezo wa soka tunajua una matokeo ya kushangaza.
Ukweli mashabiki wa Simba walikuja na matokeo Yao vichwani,wengi waliamini na kusema mechi tuanimaliza hapahapa nyumbani kwa kushinda,wengine walisema mbili bila,wengine Tatu bila,wengine nne bila.
Lakini soka haliko hivyo.
Ndugu zangu mashabiki hua tuna matokeo yetu vichwani lakini Hali halisi hua haiko kama tutakavyo.
Wanasimba wenzangu kaeni mkijua michuano yoyote inapoingia kwenye hatua za fainali mara nyingi hua Kuna uhaba mkubwa wa magoli na kupelekea mechi kuamuliwa kwa njia za penati.
Hatua kuanzia robo fainali,nusu fainali na Fainali timu kufungwa magoli matatu manne na kuendelea ni nadra sana Kwa sababu timu zinazokutana kwenye hizo hatua za fainali hua ni timu Bora sana,yaani Kila timu moja inapopanda hatua ya juu hukutana na timu Bora pia,hivyo uwezekano wa kuifunga magoli mengi hua ni mdogo.
Hebu tuangalieni Dunia mzima,zipo mechi zilimalizika Kwa ushindi wa moja bila na timu zikatwaa mataji.
Zipo mechi zilimalizika Kwa bilabila na timu zikaingia kwenye penati,
Zipo mechi zilimalizika Kwa kufungana mabao yanayolingana na mechi zikaamuliwa kwa penati.
Sasa hebu tuangalie mifano michache TU ili kutetea hoja yangu.
Juzi kati hapa Yanga ilitolewa kwenye hatua ya makundi kwa kushindwa kuingia hata robo fainali kwa kushindwa hata kupata goli moja TU nyumbani.
Hebu tuangalie timu ya Zamalek ambayo ilishindwa kupata goli hata moja TU katika michezo yote miwili na bahati mbaya ikafungwa nyumbani kwao Misri na Stellenbosch..
Kosakosa za Kapombe na Ahua.
Jamani eeh mpira wa soka kukosa ni sehemu ya mchezo,kinachopelekea kukosa kosa ni kutokana nakukabwa sana na mabeki wa timu pinzani na kunyimwa nafasi ya kujiweka vizuri kwa ajili ya kufunga goli.
Kwa maana nyingine mabeki wa timu pinzani hua hawatoi nafasi kwa mshambuliaji kulenga goli vizuri,na hii wengi hatujui TU kua ni sehemu ya mafunzo ya mabeki.
Mara nyingi Ukiona mchezaji kakosa goli ni kutokana na shinikizo la kukabwa analopewa kutoka Kwa wachezaji wa timu pinzani ili asijiweke vizuri kulenga goli,hii ikiwa ni sehemu ya ulinzi.
Hata Stellenbosch nao wametukosakosa sana na wao huenda wanalaumina,lkn yote ni kutokana na mabeki wa Simba kitowapa nafasi ya kulenga vizuri goli.
Ukiondoa fitina nje ya uwanja,Simba anaenda kuitoa Stellenbosch huko kwao.
Katika soka la Sasa kucheza nyumbani wala sio kigezo Cha kushinda,rejea Zamalek na Stellenbosch huko Misri.
Tusiwalaumu wachezaji wanapokosa magoli.
Kumbuka hakuna mchezaji asiependa kufunga,kumbuka kufunga Kuna faida sana kwao ikiwa ni pamoja na ahadi za Hela,zawadi na heshima.
Ahua aliumia akaombq atolewe hata kukosa goli alijitahidi sana.
Amini nakuambieni Simba inatinga fainali.