Simba Tunataka Kurudia Makosa Yale Yale Ya Mwaka Jana Ya Kurundika Makipa!

G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,359
5,209
Tumeshindwa kuwa na Subira! Yaani kipa namba moja anaumia tu kdgo, unaingia sokoni kutafuta kipa mwingine, stori kama hii ilitutokea mwaka jana, alipopona Manula, tukajikuta tuna makipa watano!Sasa ni muda wa makipa waliobaki kuonesha umakini wao, siyo kusajili kipa mwingine, kwa nini hatutaki kuwapa nafasi makipa tulionao? Nawakilisha...
 
Unachosema ni sahihi kabisa.

Kipindi Moses Phiri amepona halafu Simba ikawa onasuasua kumpa nafasi, niliwahi kusema Simba inazingua sana na itaenda kuathiri upambanaji wa wachezaji wengine katika timu. Wachezaji wakiona kumbe tukiwa hii timu tukaumia, tunawekwa pembeni, wataanza kucheza kwa tahadhari kubwa. Tuliona jinsi upambanaji wa wachezaji wa Simba ulivyopungua sana kwa misimu miwili, watu hawajiulizi kwa kina sababu. Wakaja kuzingua tena kwa Kramo na sasa wanaenda kufanya kwa Ayoub.

Ndiyo maana wapambanaji kama kina Kibu wameona wakimbie kabla hayajawakuta na wao.
 
Munauhakika lakini kua Lakred kaumia?
Kumbukeni kocha alisha sema hawaitaji kikosini wachezaji hawa
Laikred
Ngoma
Fred
Onana.

Hivyo kuna uongo tunaongopewa hapo kuhusu Laikred.
Lakred hajaumia yuko fresh, sema kocha hajamuelewa.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Hawana subra...itakuwa team ya Namna gan kama mtu akiumia anatolewa kabisa..Waaminiwe waliopo mpaka atakaporudi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…