NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,572
- 13,399
Ni nyota njema kwa kocha Benchikha kwa kuanza vizuri katika ligi ya Nbcpl maana Simba sc toka walipochezea kichapo Cha goli tano dhidi ya mtaani haijawahi kushinda Tena Ila ushindi mkubwa ni droo katika mechi ya ndani na kimataifa pia.
Nimewatazama Simba sc dhidi ya Kagera Sugar FC, Kuna nafasi nyingi sana zilitengenezwa lakini umakini wa kumalizia nafasi za wazi bado upo chini sana Kuna papara nyingi kwa wafungaji.
Ikumbukwe Simba sc wanakibalua kigumu Cha kimataifa dhidi ya Wydad Casablanca, Endapo Benchi la ufundi wasipoyafanyia Yafanyia kazi hayo ni hatari sana kwa timu Kama Wydad Casablanca inayokuja kuwinda point tatu muhimu.
Kocha Benchikha alitoa sababu kuwa "hatukucheza mchezo wetu tuliozoea kwa sababu ya uwanja"
Kocha alizungumza kiufundi na kwa jicho la kawaida tu inaonekana molari ya Wachezaji imeanza kurejea na Mashabiki pia watavutwa uwanjani kwenda kushuhudia mchezo wa Simba sc vs Wydad baada kuona timu Yao imeanza kufufuka.
Maoni Yangu : uwanja mbovu usiwe sababu maana Kuna nafasi za wazi kabisa zilitengenezwa na Mchezaji alibaki na kipa lakini hakufunga, Benchi la ufundi litafute Mwarobaini wa kutibu hili Kama umekosa clear chance kwa Kagera Sugar FC usitegemee kupata nafasi nyingi kwa Wydad Casablanca (timu yenye wachezaji amkini) kwa timu kubwa Kama hii nafasi huwa zinapatikana chache tu.
Nawasilisha hoja.