Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 216
- 995
Klabu ya Simba inautaarifu Umma kuwa mchezaji wake, Kibu Denis Prosper hajaripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024/2025.
Tunapenda kuutarifu umma kuwa Simba tulimuongezea Kibu mkataba wa miaka miwili zaidi utakaoisha, Juni 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimkataba.
Hata hivyo, mchezaji huyu amekuwa akitoa sababu kadha wa kadha zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini.
Kutokana na utovu huu wa kinidhamu klabu itamchukulia hatua stahiki za kinidhamu na umma utapewa taarifa.
Imetolewa na:-
Idara ya Habari na Mawasiliano, Simba Sports Club.
Julai 23, 2024