Simba haikumsomesha Singano

ibuo

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
464
438
SIKU mbili baada ya Simba kudai imemsomesha mshambuliaji wake, Ramadhan Singano Messi, walimu wa shule aliyosoma ya Al-Farouq Islamic Seminary wameibuka na kukanusha madai hayo.

Mtandao huu umefika shuleni hapo na kukutana na mwalimu wa Singano, Abuu Rashid Laizer anayefundisha masomo ya Historia na Geografia pamoja na mlezi wake Hashimu Omary Poli.

Shule aliyosoma Singano

Mwalimu Laizer katika maelezo yake amesema: Ramadhan Singano amelelewa hapa kuanzia darasa la pili mpaka anamaliza kidato cha nne mwaka 2010.

Hapa alikuwa analelewa katika idara zote, tukiwa na maana katika malezi yake kama kijana, kielimu na mambo mengine yanayomuhusu. kwanza ni mtoto yatima, hana baba wala mama.

Shirika la Africa Muslim Agency lilichukua jukumu kutoka kwa ndugu zake kwa lengo la kumuwezesha kupata elimu. kama mnavyojua, unapomsaidia yatima kuna mafanikio ambayo mwenyezi Mungu atakuwezesha mbele ya safari. Moja ya sera ya shirika ni kusaidia yatima, Ramadhan ni miongoni mwao

Kuna vitu vingine watu wanazungumza labda kutokana na maslahi yao na wanajaribu kupotosha umma, lakini kiuhalisia huyu bwana (Singano) alikuwa hapa na patroni wake yupo.

Alikuwa anatokaje hapa mpaka alipoonana na Simba? Wengi wanadhani alitoka Simba B, lakini Simba walimuona akicheza shuleni kupitia kwa kocha wake aliyekuwa akiitwa kibonge na aliondoka mwaka 2007 wakati sisi tunaingia. Licha ya kuondoka, -kibonge bado alikuwa na ushirikiano na kijana wetu pamoja na kaka yake Ramadhan Hamis.

Kuna vitu vingine inabidi tuseme ili tusionekane kumbeba mtu fulani. Mwaka 2007 nikiwa mwalimu wa michezo nikimsaidia mwalimu anayeitwa Saleh Haruna, nilikuwa nahusika kutoa vibali kwa Singano kwenda kukutana na wachezaji wenzake wa Simba B

Ni muda mrefu, lakini imekuja kuonekana hivi juzi kuwa Singano ni moja ya wachezaji wanaoweza kuisaidia Simba.- Kuanzia 2009 mpaka 2011 timu kubwa iliona anaweza kufaa, lakini yeye ni yatima na wakati anasoma kila kitu kuanzia kula, kulala mpaka madaftari viligharamiwa na shirika

Vitu vyote walikuwa wanapewa na shirika pindi wakifungua shule. Hakuna mtu aliyekuwa akimlipia ada, mimi sijaona, labda kama mtu anazo risiti alizokuwa anamlipia alete tuzione na kuthibitisha.

Utaratibu wetu wa ada ya watoto yatima huwa inakatwa moja kwa moja Damam, Quwait, ambako ni makao makuu ya Idara ya elimu ya Africa Muslim Agency duniani, lakini kwa Tanzania kuna tawi -lake hapa Dar es salaam na Sheikh Kassim Mzee ndiye aliwatafuta akina Singano na wenzake.

Baada ya kuzungumza na mwalimu, tukapata fursa ya kuonana na mlezi wa watoto yatima shuleni hapo, Hashimu Omary Poli ambaye amefanya kazi toka mwaka 1997 mpaka leo.

Katika malezo yake Poli amefafanuwa kuwa:

Ramadhan Singano nilimpokea toka mwaka 2001 akiwa darasa la nne. Amesoma hapa mpaka alipomaliza kidato cha nne chini ya udhamini wa shirika la Africa Muslim Agency.

Kijana huyu toka alipokuwa mdogo kipaji chake kilidhihirika kwenye suala la michezo, alionesha uwezo mkubwa na kwa bahati nzuri kulikuwa na mwalimu Kibonge aliyekuwa karibu nao sana.- Mwalimu huyu alipewa fursa kubwa sana ya kuwa nao na kukuza vipaji vyao.

Nashukuru Mwenyezi Mungu mpaka anafika fomu foo alikuwa kijana anayependa sana mpira na akapata bahati ya kujiunga na Simba. Tukawa tunamsikia Ramadhani Yahya Singano ni mchezaji na alikuwa anakuja kuwasalimia wenzake na wakati mwingine anawaletea misaada.

Tunashukuru kwamba anakumbuka fadhila za Maustadh wake, anakumbuka jinsi alivyolelewa, aliishi na wenzake vizuri, -tunamuombea kila la kheri.

Ninachokifahamu mimi kama mlezi nilimpokea akiwa mdogo. Suala zima la kimalezi, udhamini wa kusomeshwa shule ilikuwa chini ya Shirika la Africa Muslim Agency.-Wao ndio waliomdhamini na walimpokea akiwa mdogo kama wanavyowapokea watoto wengine yatima. Amesema Poli.

Baadhi ya nyaraka za Singano katika shule aliyosoma

Mwanzoni mwa wiki hii Msemaji wa Simba, Hajji Sunday Manara alisema klabu hiyo imegharamia masomo ya Singano na wanashangaa kijana wao kukosa fadhila.

Manara alisema:- Hivi mnajua Messi tumemtoa wapi Simba? Unajua Ramadhan Singano amesomeshwa na klabu ya Simba? Mnafahamu hilo? Kasomeshwa -IT na klabu ya Simba, -Mnajua fadhila ambayo klabu ya Simba imemfanyia?

Hao wanaosema wazazi wake walikuwa wapi wakati klabu ya Simba inamsomesha? Nauliza, walikuwa wapi? Klabu ya Simba imegharimia haya. Ninyi waandishi ndio mnaandika vilabu havithamini wachezaji chipukizi. Sisi ndio klabu pekee yenye wachezaji zaidi ya asilimia 75 tuliowatoa kwenye mpango wetu wa soka la vijana. Hawa tunawakuza na bado tunawapa ofa ya usajili

Singano ameingia kwenye mgogoro na klabu yake akidai imeghushi mkataba wake.

Simba ina mkataba wa miaka mitatu uliosainiwa mei 1, 2013 na unatakiwa kumalizika julai 1, 2016, wakati Singano ana nakala ya mkataba wa miaka miwili aliosaini mei 1, 2013 na unamalizika julai 1, 2015.

Nakala ya mkataba wa miaka mitatu waliyonayo Simba pia ipo TFF, lakini Singano anadai hakusaini mkataba huo na anautambua wa miaka miwili.

Licha ya suala hilo la mkataba, bado Singano hajatimiziwa baadhi ya stahiki zake katika mkataba wake miaka miwili ikiwemo suala la kodi ya nyumba.

Muonekano wa shule aliyosoma Messi
 
sasa yule albino anaetukana watu na kujigamba maana yake nini.
naona kaburu ametoroka na timu ya taifa
 
Simba mwachieni Singano aondoke, mbona mmemkomalia hivyo dogo...
 
Watu wakishagundua huna watetezi basi wanataka kukutumia tu kwa maslahi yao
 
Katika hii makala amemnukuu Hajji Manara akisema kuwa Simba Sc imemsomesha Singano IT, na si elimu ya msingi wala sekondari.

Najiuliza lengo hasa la kufunga safari hadi sekondari aliposoma Singano ni nini hasa?
Kwanini asingeenda chuo alichosomea hiyo IT, na kuuliza nani hasa akimlipia ada ya masomo?

Sasa nimeamini maneno ya Baba Kiki kua huyu Shaffih kuna jambo analitafuta katika uongozi uliopo.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kitu kinaendelea kati ya singano, simba na shafi dauda + luambano a.k.a wazee fursa. Kituhicho kitajulikana tu baada ya sakata la singano kwisha. Haiwezekani wakalikomalia hili suala kuliko singano mwenyewe. Kwa kifupi wao kama watangazaji (tena wa chombo makini cha habari) walipaswa wawe neutral mpaka hapo tff na vyombo vingine vya usalama vitakapotoa hukumu ni nani mkweli kati ya simba na singano kwani suala hili tayari lipo tff na polisi. Na mwenye makosa aadhibiwe kwa mujibu wa sheria bila kujali ni aveva, kaburu, hanspope au singano mwenyewe.
 
hata kama simba wamemsomesha hakustahiri kufanyiwa uhuni kama huo na huwezi kumkandamiza mtu ambae umemsaidia tabia hiyo ya kinyama
 
Haji Manara wamesema Simba imemsomesha IT course Shaffih anaenda Al_farouk shuleni??
Dah. Mbona za chini ya kapeti Singano kampigia simu Matola wanamaliza hili tatizo na uongozi. Tusubiri tuone
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom