Sikutegemea kama Mtwara ina fursa kiasi hiki

ormystatus

Senior Member
Nov 3, 2019
108
222
Nimepata fursa ya kufika eneo la MAGHALANI -MTWARA. Eh bwana eeh nilichokishuhudia imenifanya nijiulize mara mara mbili mbili kwa nini MTWARA mpaka sasa ipo nyuma kimaendeleo namna hii.

Yani maghala yamejaa magunia ya korosho na bandari ipo bize usiku na mchana. Order za watu zinasubiri meli zisepe, sawa tufanye hilo sio suala vipi kuhusu magari ya makaa ya mawe na Saruji yanayoingia na kutoka maghalani 24/7 mwaka mzima?.

Nadhani Serikali inapaswa kuongeza nguvu MTWARA ili kuharakisha maendeleo ukizingatia mikoa ya kusini ipo nyuma kimaendeleo.

MAPENDEKEZO.
SEREKALI IJENGE KIWANDA KIKUBWA CHA MAGUNIA.

Kuna maeneo yametengwa mtwara kwa ajiri ya Viwanda, hivyo basi kama Sekta binafsi zimeshindwa kufanya uwekezaji Serikali ijikakamue ijenge hata kiwanda kikubwa kimoja cha magunia (hasahasa ya katani) kwa sababu pesa nyingi tunapoteza kuagiza magunia ULAYA na ASIA.

Serikali itaweza hata kufanya ubinafsishaji mbele kwa mbele wakati huo uzalishaji ushaanza kama kuna muwekezaji atatokea. Na uzuri wake eneo la uzalishaji halitokuwa mbali na itakapotumika hiyo bidhaa ya magunia.

SERA NZURI ZA KUFUFUA ZAO LA MKONGE MTWARA ZIWEKWE.
Kwa kujenga kiwanda cha magunia tutapiga ndege wawili kwa jiwe moja, tutaongeza zao lingine la biashara tofauti na Korosho ambalo ni Mkonge na ndo litakalolisha kiwanda cha magunia.

KUJENGA VIWANDA VIDOGO VYA KAMBA .
 
Tatizo la kule ni dini isiyokuwa na tija kwa wananchi, ni kama Tanga au Bagamoyo tu. Mtu anaamka asubuhi kavaa shuka aliyolalia jana na kwenda kushinda msikitini hata mswaki hajapiga. Hana wazo la kwenda shambani kufanya kazi wala nini, anataka kukaa tu na wenzake wakisengenya waendao makazini kuwa wanaringa na kutishia maisha yao.
 
Mtizamo wa Kipumbavu! Usiamini Kila unayosikia!

Vipi kuhusu Rombo ambao wao ni kupiga ulabu tu mpaka wanshindwa kutembea!
 
Yakiwekwa mazingira mazuri kama ilivokuwa kwenye mapendekezo yangu bhasi hakika wageni watamiminika kuchangamkia fursa kwasababu wenye mji wamelala. Kwa miezi hii ya msimu wa korosho watu wa kaskazini na kanda ya ziwa wamejaa sana hapa Mtwara.
 
Kwhy hizo korosho zilizojaa hapo bandarin mpaka magunia hayatoshi kalima shemeji Yako huyo unaekaa kwake?
 
Hapo ndipo nakuona kama wewe ni mtu wa ajabu sasa wenyeji wamelala vipi wakati hizo korosho wanazobeba hao wasukuma zimelimwa na sisi wenyeji?mtaongea mengi mno ila mwisho wa siku mtakiri wenyewe tu
 
Kwhy hizo korosho zilizojaa hapo bandarin mpaka magunia hayatoshi kalima shemeji Yako huyo unaekaa kwake?
Huwa nawashangaa sana watu wa bara sisi huku mtwara tunalima mazao maarufu nchini kuanzia korosho,mbaazi na ufuta sasa huwa nashangaa mno tunapoitwa sisi ni wavivu...au kipimo cha uvivu ni kutokuwa wachukuzi wa magunia kama wasukuma?
 
Hapo ndipo nakuona kama wewe ni mtu wa ajabu sasa wenyeji wamelala vipi wakati hizo korosho wanazobeba hao wasukuma zimelimwa na sisi wenyeji?mtaongea mengi mno ila mwisho wa siku mtakiri wenyewe tu
Isiishie kwenye kulima korosho tu, ufanyike na uwekezaji mwingine .
 
Huwa nawashangaa sana watu wa bara sisi huku mtwara tunalima mazao maarufu nchini kuanzia korosho,mbaazi na ufuta sasa huwa nashangaa mno tunapoitwa sisi ni wavivu...au kipimo cha uvivu ni kutokuwa wachukuzi wa magunia kama wasukuma?
Kuna watu wanapenda vitu vya kusikia kuliko kutaka kuujua uhalisia wa kitu, utasikia tu wanasema watu wa kusini wavivu hasa watu wa bara
 
Hizi korosho na mbaazi unawalimia wewe? Usipende kuongea stori za vijiweni Kaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…