Sikutarajia watu kuumia sana kiasi cha kutoficha hisia zao baada ya mashabiki wa Simba kuchangia pesa ya adhabu

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,879
5,080
Katika hali ya kushangaza sana nimeona hata baadhi ya wachambuzi wa mpira wanaongea kwa uchungu sana baada ya kuona mashabiki wa Simba wameamua kuchangia timu yao baada ya kuadhibiwa na CAF.

Mmoja wao anayejiita chuma cha mjerumani anasema eti mashabiki kuchangia wanadhihirisha wao ni waharibifu kweli na huo ni ushamba.

Kwa maoni yake mashabiki hawakupaswa kuchangia ili wathibitishe wao hawakufanya kitendo kile!

Soma Pia: Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Mimi nalaani mashabiki wa aina ya mchome ambao walifanya hivyo ili kuichafua Simba.Mashabiki aina ya mchome wanaovaa jezi za Simba wapo wengi wamepandikizwa na wanalipwa kuharibu brand ya Simba.

Lakini pamoja na hayo hakuna namna yoyote ile adhabu lazima itekelezwe.

Nawauliza wanaoumia mashabiki wa Simba kuchangia timu yao,wanataka nani ailipe pesa hiyo?

Nini kinawaumiza wakati hawatoi pesa wao?Kwa nini wanateseka hivi au ni WIVU tu?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kuna kozi ya uchambuzi wa mpira siku hizi?
 
Back
Top Bottom