Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina yaorodheshwa na UN kwenye mali za urithi za kiutamaduni za binadamu

Yoyo Zhou

Senior Member
Jun 16, 2020
117
206
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) hivi karibuni liliamua kuorodhesha Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina kwenye mali za urithi za kiutamduni za bindamu. Uamuzi huo utasaidia kuhimiza ongezeko la ushawishi wa utamaduni wa jadi wa Kichina duniani.

Historia ya Wachina kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa ni ya zaidi ya miaka 3,000. Sikukuu hiyo pia ni sikukuu muhimu zaidi ya jadi ya watu wote wenye asili ya China. Wakati wa sikukuu hiyo, watu hununua vitu vingi vipya, kula chakula pamoja wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya, kusalimiana na kutakia heri ya mwaka mpya, kucheza ngoma za dragon na simba, kufanya ibada, na kutembelea marafiki.

Shughuli hizo zote zinaonesha utamaduni mkubwa wa Kichina. Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina hudumisha na kuimarisha uhusiano kati ya watu binafsi, familia na taifa, kurithi dhana ya ustaarabu wa China kuhusu maisha matulivu, masikilizano na amani.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ilianzishwa nchini China, lakini tayari imeenea duniani kote. Hadi sasa takriban asilimia 20 ya watu duniani wanasherehekea sikukuu hiyo, na hata baadhi ya nchi zimechukulia sikukuu hiyo kama sikukuu ya kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa utamaduni wa Kichina, licha ya watu wenye asili ya China, watu wengine wengi wenye ustaarabu na rangi tofauti wameanza kusherehekea sikukuu hiyo.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kutambuliwa na watu duniani kote pia kunatokana na juhudi za China katika kueneza na kuendeleza utamaduni wake kwa njia ya kivumbuzi. Miaka 10 iliyopita, China ilitengeneza filamu ya muziki kuhusu sikukuu hiyo, na kuionesha katika nchi mbalimbali, ili kuwasaidia watu duniani kufahamu utamaduni wa China.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kutambuliwa na watu duniani kote pia kumethibitisha tena wazo la China la kuishi kwa pamoja kwa staarabu tofauti duniani. Katika mchakato wa urithi na maendeleo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, mila nyingi za kiutamaduni za Kichina zimerithishwa.

Wakati huo huo, wakati sikukuu hiyo inapoingia kwenye jukwaa la kiutamaduni duniani, imerekebishwa na watu wa nchi nyingine kulingana na utamaduni wao, hali ambayo inaonesha kuwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China si ya Wachina tu, bali pia ni ya binadamu wote duniani.
 
Back
Top Bottom