Siku zote hesabu baraka zako

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
5,867
13,673
Kuna mwamba ambaye alipotea baharini akiwa safarini kwa mda wa mwezi mmoja,alipoulizwa ni kitu gani ambacho ulikihitaji sana wakati wa changamoto yako ya kupotea,alijibu ni maji na chakula

Naam,wakati mwingine huwezi jua baraka zako mpaka pale zinapokupotea,ndo unajua khe kumbe maji nayo baraka kubwa au chakula nacho kumbe ni baraka kubwa.

Tulio wengi wetu hatuhesabu baraka zetu ambazo tumejaaliwa na muumba wetu,huwa tunaangalia sana mambo ambayo huwa hatuna na kutamani tuwe nayo,na hii hupelekea kutozithamini baraka ambazo tunazo siku zote

Mfano mtu anapopata shida ya kupumua na kutumia gas ili aweze kusavaivi,hapo ndipo atakapo ona eeh kumbe kupumua nako ni baraka kubwa. Lakini akiwa mzima anaona kupumua kama jambo rahisi hivi na la mchezo mchezo lakini subiri shida hiyo impate ndio atajua hakika hiyo ni baraka kubwa mno.

Siku zote za maisha yetu tuzikumbuke baraka mbali mbali ambazo tumejaaliwa na mola wetu na tushukuru kwa kila jambo,usihuzunike kwa kukosa jambo fulani kwani tambua nawe una jambo ambalo wengine wanatamani wawe nalo.

Always remember to count baraka zako.

Ni hayo tu!
 
Sijasoma ulichoandika ila Kwenye mapenzi ukipigwa chini mda wa mchana hamna shida kampan plus ubize tatizo ni mida kama hii usiku upo mwenyewe kimya kimya unaugulia maumivu
 
Back
Top Bottom