Mohamedex121
JF-Expert Member
- Jan 27, 2022
- 1,733
- 3,294
Baada ya kujichangachanga kama laki 2 na nusu, nikapanga niende pangani tanga kumsaka mtaalamu (mganga wa kienyeji) kwaajili ya tiba ya maradhi yaliokuwa yakinisumbua pamoja na kuweka mambo yangu sawa.
Safari niliianza nikitokea Dar kwa basi la kampuni ya hood, nauli ikiwa 22000, na majira ya saa 8 mchana nikawa nimeshafika tanga mjini karibu na ngamiani stand (hii ndio mara yangu ya kwanza kufika tanga nikiwa sina ndugu wala mwenyeji wangu)
Nikashangazwa na watu watanga kunipokea kama ndugu yao hasa mabodaboda, makonda na madereva wa mabasi yanayoenda pangani, mama ntilie, Abiria wenzangu Nk. Nikakumbuka ule msemo wa kuwa watu wa tanga ni wakarimu sana. Nimelifurahia sana hilo nilipokuwa apo tanga.
Nauli kutoka tanga mjini mpaka pangani ni 4000 na mida ya saa 11 jioni nikawa nipo pangani stendi, muda ulikuwa umeenda nikaona bora nitafute lodge nilale kwanza kisha asubuhi ya kesho nianze kumsaka huyo mtaalamu
NITAENDELEA KWENYE KOMENTI BAADAE KWASASA NINAKAZI NAIFANYA APA HIVO TUVUMILIANE.