Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 54,142
- 122,588
Wanabodi,
Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, hivyo hizi ni salaam zangu za Siku ya Wanawake Duniani kwa wanawake wote wa Tanzania. Kwa Tanzania, Maadhimisho rasmi ya kitaifa yanafanyikia Uwanja wa Sheikh Amri Abedi, jijini Arusha, mgeni Rasmi akiwa ni Rais Samia.
Hili ni bandiko la swali, kwa maoni yangu nafasi za upendeleo kwa wanawake vikiwemo viti maalum, vinawadumaza wanawake na kuwafanya wabweteke, hivyo kwanza nawashauri Wanawake wote wa Tanzania, Acheni Kubwetekea Kubebwa bebwa ikiwemo Viti Maalumu, kwa jinsi Rais Samia alivyojibeba, sasa wanawake wengi wanaamka na kujibeba, bado kuna haja ya kuendelea kuwepo viti maalum au tuvifute na wanawake mjibebe?, aukwa vile kubebwa ni uroda, wanawake mnapenda uroda, hivyo mnalazimika kubebwa, tuvifute viti maalum mjibebe, au tuviache muendelee kula uroda kwa kubebwa?.
Nikimuangalia na kumsikiliza Rais Samia, tangu ameshika urais wa Tanzania, kiukweli ameutendea haki kustahili kupewa maua yake!, ameleta mwamko na msisimko mkubwa wa ajabu wa ukombozi wa mwamke, wanawake wengi wa Tanzania, sasa sio tuu wanajituma, na wana jibeba, bali sasa wanawake wanajiamini, wanajitambua, wanatembea vifua mbele, tena kuna baadhi wa mababa ndani ya nyumba zetu, tunakoma ila hatusemi tuu, samani tulikuwa kwa vile ni sisi tunanunua chakula, na tumekilipia bei ya jumla, tulikuwa tukitaka kula, tunajilia tuu tunavyotaka, sasa hivi sio hivyo tena, ukitaka kula sio unajichukulia na kujilia, sasa ni lazima uombe chakula, upakuliwe ndipo ule!.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Hivyo hiyo mitano tena ikikamilika, hapo October, 2025, kutakuwa hakuna sababu kabisa ya wanawake wa Tanzania kuendelea kubebwa kwa viti maalum, wengi wanabweteka!, Rais Samia hakubebwa, ifike mahali wanawake wote muache kubwetekea kubebwa bebwa, sasa mjibebe kama Rais Samia!.
Kwa miongo kadhaa, wanawake wamekuwa wakinyanyaswa, kubaguliwa, kudhalilishwa na kudharauriwa kwasababu tuu ya jinsia yao, lakini urais wa Rais Samia kama Rais Mwanamke wa kwanza, umeleta ukombozi mkubwa kwa wanawake wa Tanzania.
Ili kuwatendea haki wanawake kupata haki sawa na wanaume, ukabuniwa utaratibu maalum wa upendeleo kwa wanawake, unaoitwa kwa jina la kizungu, affirmative action, hivyo mkutano wa kimataifa wa wanawake duniani, uliofanyinyika jijini Beijing nchini China, ukatangaza ili kuleta usawa wa kijinsia duniani, nafasi za wanawake kwenye uongozi lazima zifikie 50/50 kwa wanawake na wanaume.
Ili kufikia lengo hilo, Tanzania, tukaanzisha nafasi za upendeleo la wanawake katika maeneo mengi, vikiwemo nafasi za viti maalum Bungeni na kwenye udiwani.
Miongoni mwa nafasi ambazo hazikuwahi kufikiriwa kushikwa na mwanamke ni nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia CCM. Japo CCM ilimteua Rais Samia kuwa makamo wa rais, hakuna mtu yeyote aliyewahi kufikiria kuwa kuna siku rais wa JMT anaweza kufariki akiwa madarakani, hivyo ilipotokea Rais JPM kufariki akiwa madarakani, na kwa mujibu wa katiba makamo wa rais, ndie anapaswa kuapishwa kuwa rais, tukio lilipotokea, kwa vile makamo wa rais ni mwanamke, kulitokea kizungumkuti ambacho hakikutangazwa, na watu kujiuliza sasa itakuwaje?.
Tarehe 13 Machi, saa 12 jioni, Mtanzania fulani wa idara nyeti, aliposti video ya jambo fulani kwenye mtandao wa YouTube akitokea Uingereza, (Video hiyo tembelea Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?)
Kesho yake Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, alifuta shughuli zote za kawaida ikiwemo kufuta shughuli zote za umma za rais wa Zanzibar bila kutoa maelezo yoyote!.
Kesho yake huku Tanzania bara, shughuli zinaendelea kama kawaida as if nothing happened!. Baada ya kupostiwa ile video, minong’ono ya mahali JPM alipo ikaanza, Waziri Mkuu ili kuzima hiyo minongono, akatangaza JPM yuko fiti bukheri wa afya, yuko ofisini anachapa kazi!, au mlitaka aende Kariakoo?.
Kesho yake, Makamo wa Rais akaanza ziara ya Tanga, hiyo inamaanisha ametumwa na JPM. Ni wakati akiwa ziarani Tanga, Tarehe 17 Machi, 2021, ndipo Rais Samia akatangaza msiba wa Taifa kuwa JPM amefariki baada ya kuugua!, na kuonyesha, hata hiyo tarehe 12 Machi, Waziri Mkuu hakuambiwa hali ya afya ya JPM, alifichwa!. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni? Makamo wa Rais alipopangiwa ziara ya Tanga, kuonyesha alipangiwa na JPM, naye pia alifichwa!, ina maana kuna mtu alimpangia kazi Makamu, kujifanya kapangiwa na JPM, ili kumzuga!.
Hiki kizungumkuti kilitokea kwasababu Makamo alikuwa ni mwanamke, watu wakiulizana ilikuwaje!. Za chini ya kapeti zinasema, taarifa ilipomfikia Mkuu wa Majeshi, CDF, Mabeyo, ndipo akawaamuru wahusika katiba ifuatwe, ndipo Makamo Rais Samia, akapelekewa taarifa na kutangazia huko huko Tanga. Uthibitisho wa kizungumkuti hiki, ni baada tuu ya Rais Samia kuapishwa kuwa Rais wa JMT, kazi ya kwanza ni pangua pangua ya Ikulu!.
Hii inamaanisha, kama lisingetokea lile tukio la Mach 17, Tanzania isingepata rais Mwanamke!. Naomba niwaibie jambo jingine kuhusu urais wa mwanamke, lisingetokea lile tukio la Machi 17, yaani JPM angeendelea mpaka 2025, amimi nakuambia, CCM isingemsimamisha mgombea mwanamke kwenye urais!.
Hivyo nikisema Tanzania tumepata rais Mwanamke kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, lakini baada ya Rais Samia kuwa rais wa JMT, akashauri uchaguzi wa 2025, twende na mwanamke, na Watanzania tumchague rais mwanamke na kukamilisha usawa wa kijinsia, na miminilitoa wito humu Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Kwa vile uchaguzi wa 2025, Watanzania tunakwenda kumchagua rais mwanamke,
naomba tutangaze mwaka huu 2025 uwe ni mwaka wa ukombozi wa mwanamke. Wanawake wenye sifa kutoka vyama vyote, wajitokeze kwa wingi kugombea kumuunga mkono Rais Samia, na vyama viteue wagombea wanawake kwa wingi kwenye majimbo yote ya ubunge, udiwani, uwakilishi na shehia, kisha Watanzania tuwapigie kampeni ya nguvu, tuwachague hata kupitiliza hiyo 50/50.
Na baada ya kufanikiwa kuchagua rais mwanamke, wabunge, wawakilishi na madiwani wa kutosha kupitiliza hata hiyo 50/50, najua kazi ya kwanza ya Bunge jipya ni kufanya mabadiliko madogo ya katiba kwa hati ya dharura, kuiingiza Dira ya Maendeleo 2550, kama haitaingizwa Bunge la Aprili, hivyo tuitumie fursa hiyo kuvifuta rasmi viti maalum, kwasababu usawa wa kijinsia utakuwa umekamilika kwa Rais Samia kuwawezesha wanawake kujibeba, hakuna tena sababu ya kuendelea kubebwa bebwa na mbeleko ya viti maalum, maana kuendelea kuwepo kwa viti hivi, kunapelekea wanawake kuendelea kubweteka.
Maadam Rais Samia ni mwanamke na ameweza kuwa rais wa Tanzania kwa kujibeba, Urais wa Samia 2025, uwe ni ukombozi wa mwanamke, hakuna tena tena kubebwa, wanawake mjibebe!. Je, Wabunge Viti Maalum ni wa kubebwa? Mnaonaje iwe ni awamu moja tuu kisha waendeni jimboni, kupisha wengine, au waendelee kubebwa tu?
Heri ya Siku ya Wanawake.
Paskali.