Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,594
Siku ya Ugonjwa wa Kisukari Duniani inatoa fursa ya kuongeza uelewa wa ugonjwa wa kisukari kama suala la afya ya umma duniani na nini kifanyike, kwa pamoja na kibinafsi, kwa ajili ya kuzuia, kutambua na udhibiti bora wa Ugonjwa huo
Ugonjwa wa Kisukari ni hali ya Kiwango cha Sukari kuzidi kwenye damu kutokana na tezi za kongosho kushindwa kuzalisha vichocheo vya kutosha vya insulin, au mwili kupoteza sifa na uwezo wa kuvitumia vichocheo vya insulin vyenye kazi ya kudhibiti kiwango cha Sukari mwilini.
=====
Kisukari ni ugonjwa unaoambatana na hali ya uwepo wa sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu.
Hutokea baada ya tezi za kongosho kushindwa kuzalisha vichocheo vya kutosha vya insulin, au mwili ukipoteza sifa na uwezo wa kuvitumia vichocheo vya insulin vinavyo zalishwa hivyo kufanya ongezeko kubwa la sukari litokee kuliko kiwango cha kawaida kinachotakiwa.
Insulin ndiyo vichocheo vinavyotumiwa na mwili katika kudhibiti ongezeko la sukari.
Aina Zake
Kuna aina nyingi za kisukari, lakini wataalam hupenda kuugawa ugonjwa huu kwenye aina kuu tatu ambazo ni kisukari aina ya kwanza, kisukari aina ya pili pamoja na kisukari cha ujauzito.
Vihatarishi
Baadhi ya mambo huongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa kisukari. Miongoni mwake ni-
Dalili za kisukari husababishwa na uwepo wa sukari nyingi mwilini ambazo huufanya mwili uanze kuonesha tabia hasi. Baadhi ya dalili hizo ni
Athari
Kisukari ni mojawapo ya magonjwa yanayo ongoza kwa kuua watu wengi duniani kila mwaka pamoja na kusababisha ulemavu na utegemezi wa kudumu.
Pia, huchangia kwa kiasi kikubwa upofu, magonjwa ya moyo, maambukizi makali mwilini yanayoweza kusababisha vidonda visivyopona, maumivu ya kudumu ya miguu, ugonjwa wa figo, kiharusi, kudumaa kwa afya ya uzazi kwa jinsia zote, kujifungua kabla ya wakati pamoja na kifafa cha ujauzito.
Kati ya mwaka 2000 – 2016, kulikuwa na ongezeko la asilimia 5 la vifo vya mapema duniani vilivyo sababishwa na kisukari.
Mwaka 2019, ugonjwa wa kisukari ulishika namba 9 duniani katika kusababisha vifo ambapo takriban watu 1.5 M walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huu.
Matibabu na Ushauri
Matibabu ya kisukari huhusisha mazoezi, lishe, kudhibiti uzito pamoja na matumizi ya dawa.
Kutokana na aina husika ya kisukari, mhudumu wa afya atatoa dawa pamoja na ushauri wa namna bora ya kutumia dawa hizo. Mfano wa dawa hizo ni Metformin, glibenclamide, insulin n.k

- Aina ya kwanza ya kisukari hutokea baada ya mwili kukosa sifa na uwezo wa kuzalisha vichocheo vya insulin. Mara nyingi husababishwa na mwili wenyewe kuzishambulia seli zinazozalisha vichocheo hivi. Walau asilimia 10 ya wagonjwa wote wa kisukari huwa wapo kwenye kundi hili. Hufahamika pia kama kisukari kinachotegemea insulin
- Aina ya pili ya kisukari hutokea kwa watu ambao miili yao huzalisha vichocheo vya insulin, lakini huwa sugu kiasi cha kushindwa kuvitumia kikamilifu katika kudhibiti sukari. Walau asilimia 90 ya wagonjwa wote wa kisukari huwa wapo kwenye kundi hili. Hufahamika pia kama Kisukari kisichotegemea insulini
- Kisukari cha ujauzito hutokea wakati wa ujauzito pekee. Husababishwa na baadhi ya vichocheo ambavyo mwili wa mwanamke huvitengeneza ili kumlinda mtoto. Aina hii ya kisukari mara nyingi huisha baada ya kujifungua
Vihatarishi
Baadhi ya mambo huongeza nafasi ya kuugua ugonjwa wa kisukari. Miongoni mwake ni-
- Kutoka kwenye familia yenye historia ya uwepo wa ugonjwa huu
- Kuwa na uzito mkubwa
- Umri wa zaidi ya miaka 45
- Kutokufanya kazi yoyote au mazoezi yanayoongeza utimamu wa mwili
- Kuwa na shinikizo kubwa la damu na mafuta mengi
- Kuwa na ujauzito
- Uwepo wa changamoto kwenye mfumo wa taarifa za mfumo wa kinga za mwili unaoweza kushambulia tezi za kongosho
- Kuwa mvutaji wa sigara
Dalili za kisukari husababishwa na uwepo wa sukari nyingi mwilini ambazo huufanya mwili uanze kuonesha tabia hasi. Baadhi ya dalili hizo ni
- Kuhisi njaa kila mara
- Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole.
- Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara
- Kuhisi kiu mara kwa mara
- Kupungua uzito wa mwili na kukonda
- Kupatwa na vidonda visivyo pona kirahisi
- Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati
- Kupungua kwa uwezo wa macho katika kuona
- Kupungua kwa hamu na uwezo wa mwanamme kwenye kushiriki tendo la ndoa
- Maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa mkojo, miwasho sehemu za siri na fangasi wa mara kwa mara
Athari
Kisukari ni mojawapo ya magonjwa yanayo ongoza kwa kuua watu wengi duniani kila mwaka pamoja na kusababisha ulemavu na utegemezi wa kudumu.
Pia, huchangia kwa kiasi kikubwa upofu, magonjwa ya moyo, maambukizi makali mwilini yanayoweza kusababisha vidonda visivyopona, maumivu ya kudumu ya miguu, ugonjwa wa figo, kiharusi, kudumaa kwa afya ya uzazi kwa jinsia zote, kujifungua kabla ya wakati pamoja na kifafa cha ujauzito.
Kati ya mwaka 2000 – 2016, kulikuwa na ongezeko la asilimia 5 la vifo vya mapema duniani vilivyo sababishwa na kisukari.
Mwaka 2019, ugonjwa wa kisukari ulishika namba 9 duniani katika kusababisha vifo ambapo takriban watu 1.5 M walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huu.
Matibabu na Ushauri
Matibabu ya kisukari huhusisha mazoezi, lishe, kudhibiti uzito pamoja na matumizi ya dawa.
Kutokana na aina husika ya kisukari, mhudumu wa afya atatoa dawa pamoja na ushauri wa namna bora ya kutumia dawa hizo. Mfano wa dawa hizo ni Metformin, glibenclamide, insulin n.k
- Shiriki mazoezi, husaidia kuunguza nishati pamoja na kupunguza usugu wa mwili katika kutumia vichocheo vya insulin.
- Lishe huchukua sehemu kubwa ya matibabu kwa kuwa karibia kila chakula hugeuzwa kuwa sukari mwilini. Uchaguzi wa vyakula vyenye kiasi kidogo cha mafuta na wanga, nafaka nzima, nyuzi lishe nyingi, matunda pamoja na mboga za majani hushauriwa.
- Ni muhimu kudhibiti ongezeko la uzito wa mwili. Ukubwa wa athari za kisukari mara nyingi huenda sambamba na kiasi cha uzito alio nao mgonjwa.
- Usivute sigara
- Punguza matumizi ya pombe
- Punguza matumizi ya chumvi hadi kijiko kimoja kwa siku