Siku mtu mwenye mali zake mkazi wa Dar aliyeugua maradhi yasiyojulikana alivyoletwa kutibiwa kwa mganga wa kienyeji huko Lindi

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,673
31,372
Mnakumbuka miaka kadhaa iliyo pita niliwahi kuanzisha Uzi kwamba nataka kufanya utafiti kuhusu uganga na uchawi?

Basi moja Kati ya sehemu nilizo kwenda ni Kwa mganga mmoja babu wa miaka themanini na ushee huko mkoani Lindi vijijini Alie sifika Kwa kuwa Na uwezo mkubwa WA kushindana Na wachawi Na kuwa opoa watu walio tupiwa magonjwa ya kichawi na Magonjwa Mtambuka

Tukio Hilo lilitokea mwaka 2018.

Boss huyo mwenye majumba , magari na Mali nyingi jijini Dar ES salaam na mikoani plus mkwanja wa kutosha kwenye benki aliletwa kilingeni Kwa babu huyo ambae sasa hivi ni marehemu (I mean huyo babu ameshafariki now)

Aliletwa na familia yake ikiongozwa na mke wake baadhi ya watoto zake na baadhi ya ndugu wa mwanaume.

Pamoja nao alikuwepo pia mama mzazi wa mgonjwa.

Case ya jamaa ni kwamba alikuwa amepooza Kwa Zaidi ya miaka mitatu pamoja na kusumbuliwa na vitu vingine visivyo eleweka kama vile kusikia vitu vinatembea mwilini, kusikia sauti zisizo eleweka n.k

Walipeleka hospitali ugonjwa hauonekani.

Walizunguka hospital nyingi, wakahamia Kwa wachungaji, Kisha ma ostaz na waganga wa kienyeji but kote in vain.

Kote huko mke wa jamaa alikuwa mstari wa mbele ' katika kuhakikisha mume wake anapata nafuu ya haraka '

Kesi inamfikia mganga babu wa Lindi.

Babu baada ya kuchekecha mambo yake aka enda porini akaja na miti kadha wa kadha akaagiza itwangwe pamoja na baadhi ya Dawa zilizokuwa pale kilingeni zikachemshwa Kisha mgonjwa akanyweshwa.

Dakika kadhaa baada ya mgonjwa kunyweshwa Ile dawa alitapika vitu vingi sana vya ajabu ambavyo vingeweza kujaa kwenye ndoo.

Kitu cha ajabu Zaidi mgonjwa huyo ambae alikuwa kwenye wheelchair Kwa Zaidi ya miaka mitatu akasimama na akawa mzima kabisa Yani kana kwamba hakuwa yeye aliyekuwa hajiwezi Kwa Zaidi ya miaka mitatu..

Ilikuwa Ni furaha ya ajabu sana Kwa wanafamilia.

Furaha ilikuwa kubwa Zaidi Kwa mke wa jamaa. Alionyesha furaha ya ajabu sana Na alishukuru Mungu Kwa namna ya ajabu Na ya kipekee. It was a a moment of happiness.

MGANGA ANATOA MAELEKEZO NA MASHARTI KWA MGONJWA

Baada ya tukio Hilo, babu alitoa Dawa akaelekeza Dawa hizo mgonjwa atatakiwa kuzitumia Kwa Muda wa siku ishirini Na Moja. Ndani ya siku hizo 21 hatotakiwa kuonana na mtu yoyote Yule isipokuwa mama yake mzazi au binti yake . Akaagiza pia zoezi la kumuhudumia mgonjwa chakula lifanywe Na mama Ake mzazi au binti yake Na wakati chakula kinaandaliwa asiwepo MTU mwingine yoyote Yule isipokuwa mama mzazi wa jamaa au binti wa jamaa.

(Jamaa alikuwa in his late 40s mama Ake alikuwa in her early 70s na binti yake wa Kwanza alikuwa in her early 20s mke wake alikuwa in her early 40. I just guessed there age by just looking at them. I have that intelligence).

Babu ali elekeza kwamba baada ya siku 21 jamaa atarejea kilingeni Kwa ajili ya huduma itakayo fuata.

Waliondoka na mgonjwa akiwa anatembea vizuri kabisa.. 3 days later babu anatuambia vijana wake kitu cha ajabu.

Siku ya tatu baada ya tukio Hilo mganga akatuambia "nyie wajukuu zangu hivi mnawajua wanawake vizuri" tukamjibu tunawajua kiasi chake babu. Akatuambia basi ninyi bado hamuwajui wanawake vizuri. Akatuambia siku ya Kesho atakuja yule mke wa yule kijana aliye tibiwa hapa juzi. Mwanamke huyo atakuja kuniambia Jambo mbele yenu ambalo litawafungua macho yenu kuhusu mwanamke ni kiumbe wa aina Gani.

MKE WA JAMAA ANAKUJA KILINGENI KWA BABU

To cut the story short, mke WA JAMAA alimwambia babu hivi.

BABU NAKUOMBA NIPO CHINI YA MIGUU YAKO. NINAKUOMBA UFANYE JUU CHINI UMZUIE MUME WANGU KUTUMIA DAWA ULIZO MPA NA IKIWEZEKANA UMREJESHE KATIKA HALI ALIYO KUWA NAYO AWALI.

MKE anaendelea Ku confess. Hayo maradhi yanayo msumbua Mimi ndio muhusika nilienda kumroga Kwa mganga nikapewa sumu ya kichawi nimlishe. Huyo mganga alinithibitishia kwamba Kwa uchawi Huo Hakuna MTU yoyote ataweza kumuopoa mume wangu Na kwamba sumu hiyo ya kichawi ingemtesa Kwa miaka minne Na baada ya hapo angepoteza Maisha yake. MGANGA aliniambia katika kipindi chote hicho cha mateso ya mume wangu ninatakiwa kumuonyesha upendo wa Hali ya juu Sana na kuionyesha familia Na ukoo kwamba ninapambana Kwa Hali Na Mali mume wangu apone ili ikitokea atakapo kufa basi nisi hisiwe ubaya wowote.

Sasa naona kwako dawa zako zimemuopoa kabisa Ni wazi kuwa mume wangu atapona. Kwa hiyo Mimi nipo tayari kukupa Pesa ( anataja mamilioni ya Pesa) Na kitu kingine chochote unacho kitaka ili ujitoe kwenye kumtibu mume wangu.

Alipoulizwa kwanini anataka kumuua mume wake Na kwamba amemfanyia kosa Gani Hadi amuue Yule mwanamke akasema hajafanyiwa kosa lolote Na mume wake isipokuwa anacho kitaka Ni Mali zake na mamilioni ya Pesa zilizopo benki.

AS TO WHETHER BABU ALIKUBALI OFFER YA MWANAMKE YULE MCHAWI, I HAVE VERY LITTLE TO SAY ABOUT IT BUT NINACHO TAKA KUKWAMBIA NI KWAMBA DUNIANI HAKUNA MTU ASIE PENDA PESA.

NYUMBA ZA IBADA WANATAKA PESA . KILA SEHEMU NI PESA TU. HATA WAZAZI WAKO . WALIKUWA WANAWAPENDA WEWE NA NDUGU ZAKO KWA USAWA PINDI MLIPOKUWA WADOGO LAKINI MKISHA ANZA KUJITEGEMEA, ATAKAE KUWA ANATOA PESA KWA WAZAZI NDIO ATAKAE KUWA ANAPENDWA.

Sasa Kwa kesi kama ya mwanamke huyo kama angekuwa mganga kijana, it could be very easy, Ange chukua Pesa na mpira ungerudishwa Kati..

Huyu mwanamke ana wawakilisha wanawake wengi WA kitanzania na Afrika Kwa ujumla. Kama una Mali Na umeoa Hasa Hasa ndoa ya mke mmoja, ukipatwa Na maradhi yanayo hatarisha uhai wako basi jua ya kwamba mke wako anataka wewe ufe ili arithi Mali yeye

Na wewe ndugu au rafiki WA mume ambae amepatwa Na maradhi ya namna hiyo Na unamfahamu mtu anaeweza kumtibu jamaa huyo uwe makini sana pale unapo jaribu kumuunganisha jamaa Kwa mtaalamu anae weza kumtibu shida yake Kwa Sababu mke wake akijua unaweza kuanza kufa wewe Kwa Sababu unataka kumcheleweshea kumiliki Mali ZA mume wake.
 
Back
Top Bottom