Siku Maalum ya Usafi na utekelezaji wake

Mkurya mweupe

JF-Expert Member
Aug 10, 2023
237
783
Nishawahi kutembelea maeneo mengi nakuta kuna siku maalumu ya usafi, mfano mkoa wa Geita huwa wana utaratibu wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi, ambapo wiki hii imeamuliwa ifanyike siku ya Jumamosi

Jambo linalonishangaza ni kwamba siku ya usafi maduka huwa yanafunguliwa na saa nne, yaani wafanyabiashara huwa wanakaa nyumbani au nje ya maduka yao wakisubiri muda wa usafi uishe na kufungua, huwa sioni logic ya hiki kitu, maana huwa hakuna usafi unaofanyika labda kitu ambacho huwa kinafanyika ni wafanyabiashara kuchelewa kufungua wakiwa wamesimama tu madukani au majumbani kwao na muda wa kufungua ukifika wanakuja kufungua.

Je, hii ndo huwa maana ya usafi?
 
Back
Top Bottom