Nafikiri kama kuna kitu kinawanyima raha WatanZania wengi ni ukweli kwamba nchi ya Kenya ina Uchumi mkubwa klk TanZania, hili swala linawasumbua watu sana ingawaje upande wa Kenya wala siyo ishu kivile!
Sasa huwa najiuliza kulingana na jinsi takwimu za Kichumi zinaovyo onyesha ni swala la muda tu na wala siyo swala la kama inawezekana au la kabla TZ haijawa na Uchumi mkubwa klk Kenya, sasa hiyo siku ikifika Watanzania watafanya nini? Je watafanya iwe siku ya mapumziko na kusherehekea, watacheza brn. kugonga mvinyo au itakuwaje?
Binafsi sioni kama ni ishu hata ya kunifanya nishtuke ila nitashuka siku kama TZ ikiwa na Uchumi sawa au kuzidi AK hapo ndipo nitakapo sherehekea lkn kuizidi Kenya si ni bado ni third world tu?
Na kama alivyosema Raisi Magufuli uwezo wa kuifikia AK na hata kuipita upo na uko ndani yetu tuna mazingira mazuri zaidi klk AK, kwamba sisi tuko Kiutamaduni, kisiasa stable zaidi klk AK, nchi yetu ni ya watu wa aina moja zaidi ya asilimia 98 (98%) ya WatanZania ni wabantu hilo limetupunguzia magomvi ya kiethnic kama yanayotokea Kenya, AK au Uganda na Nigeria, tuna Lugha inayotuunganisha wote ambapo wengine hawana hivyo tuna kila sababu ya kuwa power house ya Afrika, hapa kwetu hakuna Boko Haram, hakuna Alshabab au sijui Kony aliyejificha msituni na mwisho na muhimu klk yote sisi tuna CCM imara ambayo pmj na mapungufu yake yote lkn ni muhimu kwa mustakabali ya nchi yetu!