Sijui mkombozi wa elim atatoka wap

abdukarim

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
476
593
Naamini watanzania mungu anazidi kuwapigania katika harakati za kila siku.Hakuna jambo linalonisikitisha kwa kuona elimu ya Tz inakufa alafu na sisi tunawaaminisha watanzania kuwa tunawasaidia.Katika jiji letu tumeanza mitiani ya kuwapima watoto wetu kwa mitiani ya kata,wilaya na mkoa .Lakini cha ajabu tulivyozoea kuwapima watoto wetu kwa kuwachapia mitiani na kusimamiwa na waalimu wengne toka shule zingne ili tahimini yetu iwe nienye uhakika.

Sasa hv hayo mambo hayapo tena halimashauri inasema haina pesa mitihani yote iwe ya kata, wilaya au mkoa walim wenyeji mnaletewa na kuandika ubaoni kwa kuwa hakuna pesa halimashauri.Kumbuka wakurugenzi wanawaapisha kiapo wakuu eti wafaulishe vyovyote vile wajuavyo halafu wanawapa mithani wasimamie wao na kusahihisha wao ,kwenye halomashuri kunapelekwa tathimini tu.Sasa waalim now wao wanasimamia na kuchakachua na kupeleka tathimini yenye maendeleo mazuri wakati watoto hakuna walichokifanya.

Ukiwauliza wilayani au manispaa wao wanasema hatuna hela pesa yote inapelekwa serikali kuu na serikali kuu haturudishii angalau pesa kidogo sasa sisi tufanyeje nynyi fanya mtakvyoweza ili wakubwa wafurahi hilo lipite.

Kwakweli hii inaniuma sana bora tungwrudisha michango wazazi wakachangia make elim ndoo future y baadae .Wazazi wangeweza hata kitoa miambili mitihani ingechapwa na watoto wangefanya vizuri kwa kuwapima speed na kujitegemea.

Sasa unaandika ubaoni maswali hamsini wakati kuna mtoto mwingne haoni vizuri ubaoni na mwingne anaadika taratibu sana na wewe unataka kufuta angalau utumie masaa machache lakini unashindwa.Kumbuka mtihani wamwisho anapewa karatasi yake binafsi je kama hakujengewa hayo mazingira itakuwaje?

Ukienda kwa upande wa waalim walioshushwa toka secondari ni mtihani sana,wanafundisha utafikiri wanafundisha secondary, wanafunzi wanaleta mashitaka kuwa hawawaelewi wanavyo wafundisha .Mm naskitika sana kwann tunawadanganya watanzania kwa kuwauwa watoto wao kielim ili wasiweze kuwasaidia wazazi wao na wao kujitambua kwa ujumla.?

Sisi ni waalim tunazidi kuwaambia wazazi na ambao wanatarajiwa kuwa wazazi elim inakufa mwanao akmaliza atakuwa ni wakuuza machungwa kwa kuwa wanasema tufanye njia yoyote ili mradi tuwape matokeo mazuri ya kuwadanganya wazazi kumbe hamna kitu.Mungu iokowe Tz na watu wake pamoja na kizazi chake.
 
Back
Top Bottom