Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,624
- 47,250
Hii simulizi, kwa namna moja au nyingine, ina link na simulizi yangu ya kwanza kabisa hapa jukwaani Naitwa Analyse, na hii ndio safari yangu ya maisha...
Maswali mengi ambayo hamkuyapatia majibu kwenye simulizi ile, basi mtayapata kwenye hii ya sasa. Na mengine ambayo hamtoyapata humu, pengine mtayapata kwenye simulizi zijazo.
Unaweza kuielewa simulizi hii ya sasa, bila hata kusoma hiyo iliyopo kwenye link hapo juu. Nimeweka link kwa ajili ya follow up, kwa atakayetaka.
Twende Kazi.
****** ***** ***** ***** *****
1st Portion:
Kama ilivyo kwa wazazi wengine, wazazi wangu pia walikuwa wanatamani sana kijana wao nisome shule. Kile kitendo cha kuishia njiani, kwa upande wao hakikuleta taswira nzuri. Pamoja na mengi yaliyokuwa yamejitokeza, Bado tamanio lao la kuona naenda shule liliendelea kuwepo. Kitendo cha kukaa nje ya mfumo wa elimu, nilijiona kama vile regular education ishanitupa mkono, sana sana nilikuwa nafikiria kama nitaenda kusoma, basi walau iwe mafunzo ya ufundi, sikutaka kukaa darasani tena.
Ila kwa upande wa wazazi, hasa Mshua, yeye alikuwa anatamani niendelee na advance, maana sikuwa nimefeli O level, na yeye hakushindwa kuniendeleza, ni ile kiburi cha kitoto ndio kilitibua mambo. Ilifikia hatua nikiwasiliana na mshua, pakitokea quarrel ya aina yoyote, lazima swala la elimu liingiziwe, hata kama mada aihusiani. At last niliamua ngoja nirudi shule tu. Nilivyowafikishia ile taarifa Mshua aliipokea neutral, haoneshi kama kafurahi au la. Ila alikubaliana nayo.
Tokea nimalize form 4, ulikuwa umepita muda kiasi, Mshua alipata tabu kunipatia usajili katika shule ya serikali. Nakumbuka Mshua alikuwa muda wote ni kuongea na simu tu, mara kapiga huku, mara kule, mara kaenda kukutana na mtu huyu au yule. Maana mfumo wa government ulikuwa unanikataa. Option ya kwenda shule za private ilikuwepo, ila sikuelewa kwanini Mshua alikuwa analazimisha nisome shule ya serikali. Alifosi sana anavyojua yeye, hatimae nikafanikiwa kupenyezwa kwenye shule ya serikali, japo nilianza kwa kuchelewa takriban miezi mitatu.
Binafsi nilikuwa sitaki kusoma nje ya Dar, wakati mshua yeye alikuwa anaamini, nikipata shule Dar sitosoma. Kwahiyo aliniwahi na kauli moja, kama sitokubali kwenda kwenye shule itakayopatikana, basi nitarudi kwenda kusomea kule kijijini walipo. Sikuwa na namna. Hatimae nikabahatika kusajiliwa katika shule iliyokuwa pale mkoani Tanga.
Changamoto na Mzee wangu Bado ikarudi pale pale, kwenye swala la combination. Mzee yeye anasema nisome zile za Arts, binafsi sikuwa na mpango nazo. Tena kuonesha Yuko serious, kabla ya kwenda rasmi shule, alininunulia vitabu kadhaa vya language na Kiswahili. Mshua yeye alikuwa anaamini kwavile napenda kusoma vitabu, basi njia sahihi kwangu ni Arts. Ila kwa upande wangu, kusoma vitabu ni hobby tu. Sikutaka kubisha, nikavipokea, nikaenda shule rasmi shule.
Kitu cha kwanza nilichofanya baada ya kupokelewa pale shuleni, ilikuwa ni kutaka kujua combi zinazotolewa pale. Palikuwa na PCB, PCM, CBG na HKL tu. Nikaanza mchakato wa kuomba kubadilishiwa combination . Baada ya kuzungushwa sana, mwishowe nikauvagaa mziki wa PCM. Nilivyompa taarifa mshua, kwa mara ya kwanza Mshua akanitukana, kisha akaniambia "Hivi unajua nimepoteza hela kiasi gani mpaka wewe umepata hiyo nafasi, au unadhani nina hela za kuchezea?". Kila nikijaribu kujitetea, ananicrash, mwisho wa siku akaniambia "Unatumia nguvu sana kutaka kuniletea aibu kwenye familia, sasa Sikia ukipata zero nisikuone tena hapa kwangu"
Tukaishiana hivyo.
****************
Nilipata tabu sana pale shuleni, sana yani. Ile miezi 3 ya mwanzo ilikuwa kama miaka mitatu. Kila walim wakitangaza kuna test, nakosa amani kabisa, maana kama sijawa wa mwisho, basi ni wapili kutokea mwisho. Kuna jamaa alikuwa anaitwa Athuman au Ochu, huyo ndiye tuliyekuwa tunapokezana nafasi mbili za mwisho, akidoji test ya namba, basi ujue mkiani nitakuwa Mimi. Hapo kipindi Mimi shule naiona kama gereza, kuna wadau wanafanya solving kwenye nekta ya form 6, na maswali yanawatii. Kuna jamaa mmoja nikamganda sana awe ananikatia mapindi, maana kidogo alikuwa njema. Alivyojua Sina topic yoyote ambayo nimeshasoma, alinishangaa sana, akaniambia "Dogo hii ni PCM, hatuji shule kichwa kichwa". Huyu jamaa ndio alikuja kunionesha mchikichini, na hapo ndio nilikutana na watu (walimu) ambao walinibadilisha kabisa, walioniondolea aibu na fedhea darasani (mmoja kwasasa ni marehemu, Mungu amlaze pema).
Nilipoingia form 6, nishakuwa mwenyeji sasa pale Tanga, hakuna ratiba ya baikoko ambayo nilikuwa siijui. Hakuna malaya wa Chichi na La Cassa ambae nilikuwa simjui. Wamama hao ndio usiseme, Ijumaa mpaka Jumapili nilikuwa sionekani kabisa maeno ya hostel. Na baadhi ya Jumatatu, nilikuwa naenda shule kutokea nyumbani kwa Mama Mariam.
Nilijikuta nahitaji sana hela, ili kuweza kukeep up na movements zangu. Nilikuwa na jamaa yangu mmoja wa karibu sana, yeye alikuwa ni mzawa wa kule kule, aliitwa Ochu. Jamaa alichoresha mchoro, tuibe mahindi kwenye store ya shule, walau yatupatie vihela kadhaa tukiyauza.
Lile deal lilienda vizuri, maana tulikuwa tunahamisha mahindi kidogo kidogo, then tunaenda kuyahifadhi kwa bi mkubwa ambae mumewe ndio tulipatana tumletee gunia moja. Bahati mbaya, yule Mama akajikuta raia mwema, akavujisha ile issue kwa Mwalim. Siku hiyo kama kawaida tumejaza mahindi kwenye mabegi tunapeleka kwa jamaa, tunakuta Mwalim anatusubiria. Akatulaza kituoni, then kesho yake kesi ikasomwa assembly.
Tukala stick mbele ya umati. Kisha tukapewa suspension ya miezi 3, tukirudi tuje na wazazi pamoja na hela ya fine.
Issue inaanza, ni mzazi gani nitamuita? Mama hawezi kuja, Mshua yuko mbali sana na pale, lakini hata ingekuwa karibu nisingeweza kumwambia ule ujinga. Kwa upande wa mwanangu Ochu, wiki kama 2 zilizopita alikuwa na msala home kwao, kwahiyo alikuwa kwenye kipindi cha tahadhari, so hakuweza kuwaambia home kwao, japo yeye ni mzawa wa pale. Mwisho wa siku tukaadhimia tuite wazazi wa kukodi, japo mwana yeye lile wazo hakuliafiki hata kidogo. Hostel za ile shule niliyokuwa nasoma, zilizopo nje ya shule, zilikuwa opposite na vijumba fulani vya mbao, vimechoka sana, walikuwa wanaviita Kijiji Cha 21 (kama sijakosea), sasa mwanangu Ochu ndio akaenda kuchukua Mzee mmoja pale, aende akaigize kama baba ake mdogo. Siku ambayo Ochu alienda na baba ake mdogo feki, na Mimi nilienda kwa dhumuni la kuomba niendelee na masomo, mzazi wangu yupo njiani anakuja. So wakati tumesima pale, Mwalim wa nidham akamuuliza yule baba mdogo feki wa Ochu amekuja pale kwa dhumuni la nani? Yule dingi akasema yeye amekuja kusikiliza kesi ya Ochu, Mimi hanifahamu.
Mwalim: "Mzee umekuja kwa ajili ya nani hapa? Au wote?"
Mzee : "Nimekuja kwa ajili ya huyu (akimnyooshea kidole Ochu"
Mwalim: "Mwanao anaitwa nani?
Mzee: "Ochu.... , Athuman"
Mwalim: "Athuman nani?"
Mzee : Akawa Kimya. Mwalim akarudia tena swali, ila Mzee kimya.
Mwalim: "Una uhusiano nae gani?"
Mzee: "Mtoto wa kaka angu"
Mwalim: "Huyo kaka ako anaitwa nani?"
Mzee: (kimya)
Mwalim (akamnyooshea Ochu kidole) : "Haya, wewe na baba ako, ondokeni mkaje na baba enu"
Kisha akanigeukia na Mimi, wewe pia ondoka, bila mzazi nisikuone hapa.
Nikatangulia Mimi kutoka, wakanifata kina Ochua, hao tukaenda nje ya shule. Hapo tayari nishaingia ubaridi, maana sioni namna naweza kumwambia mshua aje.
Baada ya kama wiki hivi ya kuzurura zurura pale mjini, nikaenda sehemu moja inaitwa Nguvu Mali, kule kulikuwa na jamaa yangu anasoma Galanosi. Nilivyomuelezea msala wangu, akasema atanikutanisha na jamaa mmoja hivi, mchaga, ambae alikuwa na biashara yake karibia na maeneo ya shuleni kwao. Huyo mchaga, alikuwa anatumiwa sana na wanafunzi wa Tanga Tech kwenye misala kama hiyo. Kwa ufupi alikuwa mbobezi (kwa maelezo aliyonipa jamaa yangu)
Basi alivyonikutanisha nae, ikabidi nimpange issue ilivyo, kwamba kuna kesi ya uongo na kweli nimepewa huko shuleni, akaniuliza maswali mawili matatu, pia nikamuelezea jinsi Ochu alivyoumbuka ofisini, yule jamaa akacheka tu. Akasema hayo mambo madogo, kesho kutwa ntakuja. Wakati nataka kuondoka, akaomba advance 10k, maana tulipatana 25k.
Endelea hapa: Sijawahi kujutia kwenye maisha yangu. Mpaka siku niliyokutana na yule Mzee