Siielewi hii kampeni: Mtoto wa leo ni Samia wa Kesho

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
20,189
29,663
Kuna kampeni ya Leo imezinduliwa mkoani Tanga na Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko inayoitwa Mtoto wa Leo ni Samiah wa Kesho. Hii Kampeni nimeshindwa kuuelewa kusudi lake. Je ni kweli kwamba kila mtoto wa Leo atakuwa Samiah wa Kesho?.

Je, ni kweli kila mtoto anataka kuwa Kama Samiah? Je wawe Kama Samiah kimatendo au kicheo?. Yani wanakuwaje Kama Samiah.

1. Samiah ni Rais, je kila mtoto ana ndoto ya kuwa Rais?.

2. Samiah ni mwanasiasa, je kila mtoto ana Nia ya kuwa mwanasiasa au kuwa Mwenyekiti wa chama?.

3. Samiah ni mwanamke , je watoto wa kiume Wanavutiwa kuwa kama yeye?

4. Samiah amemteua mkwe wake kuwa Waziri kwenye serikali yake , je kila mtoto kesho awe Kama yeye a teue wakwe kwenye serikali.

5. Samiah elimu yake ya kuunga unga, je watoto wa Leo na wao wawe na elimu ya kuunga unga?

6. Samiah amekopa Deni la nje kuliko Marais wote waliopita, he watoto wa Leo wawe Kama Samiah?

Nadhani waliokuja na kampeni hii mashuleni walikuwa na lengo la uchawa ndani yake. Ingekuwa Bora pale ambapo wangesema " Mtoto wa Leo ni Rais wa Kesho" ingekuwa vizuri, lakini kuandika jina la mtu Kwenye kampeni kubwa Kama hiyo ni uchawa.
 
Samia or Samiyah (Arabic: سامية sāmiyah), also spelt Samiya, Sameea, is an Arabic female given name meaning “elevated, exalted, lofty”, “high of prominence, eminence, glory, distinction”, “aspiring to the highest distinction, honour, sublime, proud, noble-minded of ethics and morals
 
Kuna kampeni ya Leo imezinduliwa mkoani Tanga na Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko inayoitwa Mtoto wa Leo ni Samiah wa Kesho. Hii Kampeni nimeshindwa kuuelewa kusudi lake. Je ni kweli kwamba kila mtoto wa Leo atakuwa Samiah wa Kesho?...
Wivu ndio unakusumbua sidhani kama kuna jingine.

Basi mtoto wa Leo ni economist wa kesho 😂😂
 
Kuna kampeni ya Leo imezinduliwa mkoani Tanga na Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko inayoitwa Mtoto wa Leo ni Samiah wa Kesho. Hii Kampeni nimeshindwa kuuelewa kusudi lake. Je ni kweli kwamba kila mtoto wa Leo atakuwa Samiah wa Kesho?...
Shida nini mkuu?
 
Kama ni hivyo basi bora wangu nimpe sumu leo usiku afie huko
Nyumbu mmekwama aisee, dah!!!

Mumchukiae huyo Sasa.......hata habari na nyie Hana, anapiga Kazi tu. Kweli kama alivyosema Dr Janabi; 'haters wa mama Samia hatarini kujifungua kabla ya wakati'
 
Wanafikiri kuwa rais ndio jambo kubwa na bora zaidi duniani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…