Sifa za wasio na elimu ya halali hasa wanapokuwa wanasiasa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,859
Wapo wanasiasa ambao hawana elimu ya halali yao au hawana kabisa elimu. Wanasiasa hawa wengine wamebahatika hata kupenya na kushika nyadhifa kubwa kwenye Serikali au kwenye vyama vyao. Hawa ni wale ambao walisoma na kufeli au wale wanaotumia veti vya magumashi/vyeti vya watu wengine.

Wanasiasa wa aina hii wao huwa na silaha mbalimbali katika kubaki walipo au hata kupanda zaidi. Wanasiasa hawa huwa wanajipambanua kwa kujikomba, kunyenyekea kupita kiasi, kusifu kila analofanya mkuu wake na kuigiza mara kwa mara kuwa anatekeleza kila ambalo mkuu wake atakuwa akilisema au kulifanya.

Kiufupi, wanasiasa walio na ukakasi kwenye elimu zao huwa ni waoga na wasiotaka kuwaudhi wakuu wao. Wanasiasa hawa wanajazwa hofu na elimu yao ya magumashi. Wanasiasa hawa vyamani na serikalini hutenda kazi zao kiujanjaujanja kwa kuwatumia watu wengine ambao huwalipa sirini ili kuwafanyia kazi zao.

Wanasiasa hawa wenye elimu za mashaka hawataki kabisa majadiliano ya uelewa ya ana kwa ana kwakuwa yaweza kuonyesha upungufu wao wa uelewa juu ya mambo hata yale ambayo ndiyo wanayoyasimamia kila siku katika nafasi walizonazo.Yanapotokea majadiliano ya aina hiyo, ya ana kwa ana, wanasiasa hawa kutuma wawakilishi wao wenye weledi kuhusu mambo hayo.

Wanasiasa hawa huishi kwa sanaa na usanii kwelikweli. Wanasiasa hawa si wa kuwaamini kwakuwa ndio informers and puppets for others. kazi yao huwa ni kujilinda wasiumbuke na kuhakikisha wakuu wao wanaendelea kuwaamini kupitia kujikomba kwao na kuwachengea wengine.
 
km mkuu fulani vile zenj nae ana kiromoromo kweli,huyo jamaa ni kada kwelikweli wa yanga elimu yk std 4,mkuu wa fitna Zanzibar jina lk linaanzia heruf V
 

Umenena vyema. Na kwa kuongezea hapo watu wa aina hiyo huogopa kabisa kuongelea kuhusu ufaulu wa wanafunzi katika maeneo yao hasa unapokuwa wa chini. Watafanya kila njia kuhakikisha mijadala inayohusiana na ufaulu inapotezwa kiaina.
 
Nisaidie kuweka mfano kama unao Mkuu
Mkuu hapo kwenye bold ......... jaribu kurekebisha ili uendane na heading yako.

Watu waliofail na watu wanaotumia vyeti vya wengine ni tofauti kabisa. Kafail kunaweza kuwa katika level fulani (let say form six) halafu baada ya kuafail mtu akaendelea na maisha yake na mihangaiko yake mpaka akafanikiwa, mfano anaweza kuwa John, Jacob, Ole!!

Kutumia vyeti vya watu ni tofauti kwa kuwa ni wizi wa kiaina. Hapa mtu anafail darasa la saba, form four halafu anatumia cheti cha mtu mwingine kujiendeleza mpaka anafanikiwa bila probably bila kugundulika, mfano anweza kuwa Daudi, Innocence au Petro!!
 
Mmoja wako RC wa DSM.

Kwa jinsi alivyokua anaiendesha ile vita ya madawa ilibidi nijiulize akili yake ipoje.
 
Akibahatika yeye ndio akawa mwenyekiti wa chama kwa mfano anakuwaje, enhheee hebu tupe tufaidike!
 
U
umenikumbusha mjadala wa Hamad Rashid vs Freeman Mbowe, Serena Hotel, ilibidi lissu awe pembeni kuokoa jahazi. Kweli waliofeli huongoza kijanja kijanja
 
Hivi Mh. Mbowe angelikuwa na vyeti vya kugushi miaka yote hii si vingelikuwa vimechapishwa!? Nawaza tu kwa sauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…