Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 286
- 595
Utangulizi
Nimekua nikisoma habari mbalimbali katika mitandao ya kijamii, katika Jambo ambalo linanipa maswali ni mabadiliko ya vigezo vya kuoa au kuolewa
Wakati nikiwa kijana mdogo kuna maswali yalinisumbua sana, mana mtaa ambao nilikuwa naishi ulikuwa na nyumba za watumishi WA umma (magorofa ya TBA) na kwa sehemu kubwa walikuwepo wanasheria na watumishi WA idara zingine za serikali
Marafiki zangu Kwa sehemu kubwa Baba Zao walikuwa wanasheria na mama Zao walikuwa walimu na wachache walikuwa mama WA nyumbani.
Wakati nikiwa katika harakati za kuoa maswali mengi yalikuwa kichwani mwangu juu ya wale wazazi wa rafiki zangu na wazazi wengine ambao nilikuwa nawafahamu.
Kwakweli Kwa sehemu kubwa kulikuwa na ufanano na ndoa hizo sina uhakika Sana juu ya migogoro iliyokuwako kwenye hizo ndoa , nachojua zilitulea na kutufikisha hapa tulipo.
Wakati nataka kuoa niliwaza Sana ni kigezo gani kiwe cha Kwanza na muhimu kwa binti ambaye atakuwa mke wangu?
Kigezo cha Kwanza ambacho kilikuwa moyoni mwangu ni
A. Mwenye Hofu ya Mungu 60%
Kuna tofauti ya kwenda kusali na kuwa na Hofu ya Mungu , kipindi cha kuoa au kuolewa kila mmoja anakwenda kanisani Kwa tumaini la kumpata mweza ndio maana lazime UWE makini, sio kila MTU anayekwenda kanisani ana Hofu ya Mungu
Biblia inasema MTU Mwenye Hofu ya Mungu ni Yule anayeskia neno la Mungu na kutetemeka , unashangaa uko kwenye mahusiano na binti tena ni MTU wa ibada Sana lakini haigopi uzinzi ! Ujue huyo MTU Hana Hofu ya Mungu.
Umesoma habari ya Yusufu alipolazimishwa na mke wa potifa kufanya nae mapenzi ,akakataa akiogopa kumtenda Mungu dhambi.
Leo hii vijana wanapotaka kuoana wanataka Kwanza kufanya ngono Kwanza wajuane Kwanza , ndio maana ndoa nyingi za Leo zina pata shida
B. Mama wa Watoto wangu 30%
Nilijiuliza maswali Huyu binti ambaye nakwenda kumwoa ndiye atakaye kuwa mama wa Watoto wangu?
Kuna kitu ambacho watu wengi Hawajui , tumbo la mwanamke limewekwa na Mungu kupitisha agano la Mungu Kwa mwanadamu
Mungu alisema na Ibrahimu akamwambia utapata mtoto wakiume Kwa Sarah Kwa sababu kwenye tumbo la Sarah Ndiko kuna agano ambalo Mungu alifunga na Ibrahimu ndio maana licha ya Ibrahimu kuwa na watoto wengi lakini ni Isack Tu ndiye aliyepewa urithi wakiagano na Mungu
Kwa hiyo unapochagua binti wakuoa ni lazima ujue anafaa kuwa mama wa Watoto wako?
Kuna tofauti ya kuwa na binti kama girlfriend na binti kama mama WA familia
C. Mwenye kujishughulisha
Ni kweli biblia inatoa maagizo kwamba Baba ndiye ataleta chakula Kwa ajili ya familia, lakini biblia hiyo hiyo inasema mke Mwema ni Yule anayejishughulisha Kwa kazi ya mikono
Leo hii mabinti wengi wanafanya kazi nzuri Tu lakini bado wanategemea fedha Zao kuzitumia Kwa matumizi ya mapambo na hanasa za Dunia lakini za mume ndio zitumuke kwenye familia
D. Na vigezo vingine ambavyo 10%
Vigezo vya Karne ya 21
A. Mwenye Shape au Elimu na fedha 60%
Kitu ambacho kinanisikitisha ni habari za ndoa za SASA watu kuachana hata mwezi hawajafikisha? Umetumia gharama zote za sherehe kubwa lakini ndoa hazidumu Kwa sababu umeangalia kitu kidogo Sana , shape inakwisha, Elimu sio maarifa na fedha zinamabawa Leo ziko kesho haziko, vitu vya nje haviwezi kutunza ndoa