Siasa za Zanzibar na hatma ya Muungano

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,226
3,290
Muungano huu umepita katika majaribu kadhaa, miaka ya 1980 ulipata dhoruba ya kilichoitwa kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar.

Muungano ulitumia rungu la chama (CCM) kumuondowa rais aliyechaguliwa na wazanzibari kule Dodoma kwa mwenyekiti wa chama na wenzake kufanya maamuzi ya kumtimua rais Jumbe ambaye NI RAISI HALALI.

Wazanzibari wazalendo na wasomi wameendesha jitihada nyingi za kutaka Muundo ubadilike ili kuipa mamlaka Zanzibar kufanya maamuzi yake kwa maslahi ya Uchumi na maendeleo bado hazijafanikiwa.

Kuja kwa vyama vingi kuliamsha ari mpya. Wazalendo wamejaribu mara kadhaa kutumia mbinu mbali mbali kuanzia bungeni , mijadala na hata kuunga mkono upinzani ili kujaribu kusikilizwa lakini bado.

Miaka ya 1990, wakati wa uongozi wa Dr Salmini alichukuwa hatua kadhaa za kujitutumuwa ikiwamo kujiunga na OIC na kuifanya bandari ya Zanzibvar kuwa huru. Kwa mara nyengine muungano ulitumika kudhoofisha jitihada hizi kwa Zanzibar kulazimishwa kujiondoa OIC na aidha kuanzishwa TRA inayopanga viasi vya kodi na kukusanya kodi Zanzibar -Hali bado imebana.

Mwaka 2013-2014 ikaja Katiba mpya, wazanzibari kwa umoja wao kupitia maoni ya wananchi kwa Tume ya warioba Wazanzibari walitaka muungano wa serikali tatu. Mawazo yaliyotokana na kutaka muungano wa Mkataba hapo awali.
Bunge la Katiba (Chombo cha muungano) kilitumika tena kupora maamuzi ya wazanmzibari kwa kufanywa vitimbi wakati wa kupiga kura na kugeuza maoni ya weazanzibari ya kutounga mkono serikali mbili zilizopendekezwa. Kwa mara nyengine hapa siasa za muungano zilitumika na kupora fursa ya kurekebisha muungano wetu kwa njia za maelewano.

Mwaka 2015 wanaharakati na wazalendo kwa umoja wao waliunga mkono upinzani (CUF )kama njia muafaka ya kubadilisha viongozi na wakaichagua CUF kusimamioa mambo yao wakiamini wataweza kuipeleka ajenda ya Muungano wa usawa pale panapostahili kwenye uchaguzi wa Oktoba 2015. Jeshi la wananchi chombo cha muungano kwa kushirikiana na polisi na usalama wa taifa kwa mara nyengine tena waliotumika kupora haki ya Wazanzibari kwa kufanikisha kuzingira(Bwawani undersiege by Military Force ) hapo tarehe 28 0ktoba, 2015 na hatimae Jecha kufuta uchaguzi halali.

Kama haitoshi Jeshi la Polisi na vyombo vyengine vya usalama vya muungano bila kujali uhalali au uharamu vilitumika kutii uongozi ulio nje ya katiba wa kujiongezea muda visivyo halali na vilitumika kupambana na jitihada za wananchi kutaka haki itendeke.

Aidha ni jeshi la polisi hilo hilo na vyombo vyengine vya muungano vilitumika kulinda Uchaguzi haramu uliofuta kinyume cha taratibu matakwa ya wananchi ya tarehe 25 oktoba,2015. Bila kujificha Amir jeshi mkuu kutumia neno fyokofyoko kulinda maslahi yake dhidi ya Wazanzibari.
Jeshi la wananchi na polisi lilipelekwa hadi vichochoroni kule Zanzibar na kutisha wananchi na kukamata watu waliodhaniwa wengeleta fyokofyoko.

Hatimae Vyombo vya Muungano vimetumika kumuapisha na kumpa ulinzi dr Shein bila kujali uhalali wa kilichofanyika kama kiina uhalali.


Hali hii inaleta taswira kuwa siku zote vyombo vya muungano hutumika kudhoofisha ama kufuta haki za wazanzibari na hutumika kulinda maslahi ya wahafidhina wachache na kuacha maslahi ya wengi.

Bila ya kujificha vyombo vya dola vya Muungano vimejidhihirisha kuibeba (CCM) kule Zanzibar na wameacha sintofahamu ya kiutawala ikiendelea katika ule unaoitwa uchaguzi wa marudio.


Mara hii kupitia uchaguzi wa 2015 jumuiya ya kimataifa imejitutumuwa kwa Tanzania walau kwa hatua za awali kupinga uchaguzi wa marudio na kuchukuwa hatua angalau kwa MCC kusitisha msaada wao.

Picha hio tuipeleke kwenye hatima ya Muungano wetu. Jee hali hii itaubakisha salama? na jee kwa jitihada hizi za viongozi wa muungano kutumika kufanya haya dhidi ya maamuzi ya wazanzibari walio wengi ndio kusema tunaimarisha muungano na hivyo ndiyo utaendelea kudumu?

Nini kitafuata baada ya sakata la Zanzibar juu ya huu muungano? na role ya vyombo vya Muungano kufanikisha kilichotokea zanzibar?

Muungano' muungano' muungano'

Acha tuone muda utasema.
 
snitch underways tena ya hali ya Juu / kulikuwa na ubaya gani seif kuachiwa Zanzibar?/ magufuli anamaadui wengi sana! wengine wakijifanya kumpa ushauri! wa ndivyosivyo for their special targets.
wiser 1 na hapa vipi?
 
Mapinduzi hayakuletwa kwa kalamu na karatasi, hivyo nasi hatutawapeni kwa kalamu na karatasi. Asha Bakari. Swali ni kuwa; hizo pesa zinazotumika kuandaa karatasi na wino na maigizo yoote ya kupiga kura zingelitumika vizuri si zingeleta maendeleo Zenj??
Tunatumia mabillion kutengeneza filamu ya masaa 12 tu halaf inapotea mpaka tena baada ya miaka 5? Ni Tz tu
 

Hata jumuiya ya kimataifa mara hii imejiridhisha jinsi Muungano ulivyotumika kupora maamuzi ya wazanzibari na ndio maana kwa mara ya kwanza Tanzania kama Tanzania imekutana na changanmoto hio na sio Zanzibar pekee .

Hivi sheria za kimataifa katika hili la Zanzibar zinasemaje? wazungu kwenye maslahi yao hawashindwi kufanya fitina

Isije ikatumika hii kuleta chokochoko ya muungano hasa ikizingatiwa waingereza ndio walikuwa koloni la Zanzibar

wenye kujuwa tuelekezeni
 
Tatizo la siasa za Tanzania ni Tanganyika kutojua kula na kipofu. Ukila na kipofu jitahidi usimguse mkono, kwani atajua kama anakula na mtu mwengine.

Ni siasa chafu za udini wa kikatoloki uliowavaa hususan viongozi wa CCM wa bara kuliridhia kanisa hilo kuupanua ukatoliki wao Zanzibar kwa hila na vitisho. Jambo hilo ndio liliowashtua masheikh wa Uamsho na kuanza kampeni za kuwaamsha wazanzibari. Na wameamshika kweli. Pamoja na kuwa wako kizuizini matokeo makubwa yaliotokea yanadhihirisha kuwa wazanzibari wameshaamshwa na kuamshika.

Vipofu Zanzibar ni watu wepesi kuwatawala kama hutagusa desturi zao, imani, silka na mila zao. Wazanzibari u unaweza kuwatawala kwa kuawatisha kwa mtutu wa bunduki na vifaru lakini huwezi kuzimiliki nafasi zao daima.

Mreno alijaribu kwa karne kadhaa na akashindwa. Rai za akina Lukuvi na Sitta pia hazitafua dafu! CCM bara msome alama za nyakati.

Mjiulize kuna Rais gani mzanzibari wa kuzaliwa aliemaliza muda wake wa miaka 10 hajageuka kuwa mpinzani wa muungano? RAIS Jumbe alipinduliwa Dodoma kupinga muungano,Komandoo alidiriki kumtolea uvivu Nyerere na kumwambia asimjaribu kiberiti chake kimejaa, Karume ndio huyo anaongoza mapambano mpaka CCM BARA/KISONGE wanamuundia vikundi vya kumzomea kwenye sherehe za chama; Sheikh Idrissa yeye hakutaka hata kuongeza kipindi cha pili kwa kukataa kuburuzwa na bara.

TUWACHENI TUPUMUWE
 

KISHADA;
Mkoloni Mwingereza ametokea wapi na kuufuta uchaguzi uliofanyika chini ya uongozi wa Jecha?? Jamani Mnyonge haya mnyongeni ila haki yake mpeni. Usimwonee Muingereza wala Shetwani. Mwambieni Jecha, tumemkubali. Hakuna awezaye kumpinga ila historia itamsuta. Muungano haupo kwenye hili la kurudiwa kura kabisaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…