Katikati ya ukimya unaomezwa na hasira zilizojificha kuna mwangwi mkubwa wa kishindo cha ukimya wa visasi ulioipowa, ni kana kwamba unasubiri wakati ufike tu ulipuke.
Watu wana hasira ndani ya ukimya na wanameza hasira hizo. Kitu kimoja kiko wazi kule Zanzibar.
Ingawa watu wanaendelea na maisha bado wanaamini haki yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015 itapatikana, sijui ni kwa nini? Maisha yako juu na kila kitu kibaya watu wa kule wanakiita zombe au Jecha.
Nilipata taarifa kuwa wawakilishi wapya na madiwani na hata rais wamebatizwa majina ya Wawakilishi Mazombi na madiwani mazombi.
Mtu akikosea anaitwa zombi au jecha ilimradi kila kitu ni Zombi au Jecha
Lengine liko wazi jamii imekatika vipande hasa kule kisiwani Pemba. Jambo hili naamini linawakosesha raha viongozi na watawala.
Habari ya kinachoendelea Pemba sio nzuri. Kuna taarifa za watawala na viongozi wakuu kushindwa kutembelea Pemba. sijui kwa shughuli nyingi au wanatishwa na kivuli cha Mazombi.
Kuna taarifa ambazo zinafichwa kwamba kabla ya uchaguzi wa marudio hadi sasa viongozi wa kitaifa walikuwa wakisusiwa misikiti na sehemu za ibada na shughuli za kijamii.
Ukimya wa Zanzibar unaashiria jambo na kule kila kitu ni Zombi au Jecha.
Taifa linakwenda wapi?