Si kila tukio ni la watu wasiyojulikana mengine kama la Dodoma yanahusisha wivu wa mapenzi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,581
117,723
Watu watatu wameuawa, huku mama mwenye nyumba akijeruhiwa na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Segubwawani, Kata Nala jijini Dodoma.

Waliouawa ni watoto wawili wa familia moja ambao miili yao imekutwa imeungua motor, huku mfanyakazi wa ndani akikutwa na majeraha kichwani.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Anania Amo akizungumza na Mwananchi usiku wa leo Jumatatu Septemba 16, 2024 amesema watu watatu walikutwa wamefariki dunia.

Amesema mmoja ambaye ni mama mwenye nyumba alikutwa amejeruhiwa na amepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

“Huyo aliyewahishwa hospitali anaonekana ana jeraha kichwani na watatu tuliendelea kuangalia hali ya majeraha waliyoyapata kabla hawajafariki. Hawa wawili (watoto), walikutwa wameungua isipokuwa mmoja ndiyo amejeruhiwa hajaunguzwa,” amesema.

Amesema hakuna jirani aliyesikia kelele, bali mtoto aliyetumwa kwenda katika familia hiyo ndio alirudisha habari kuwa hakupata ushirikiano.

“Majirani waliposogea katika nyumba hiyo, mtoto wa miaka sita ambaye alikuwa katika nyumba hiyo, lakini hajajeruhiwa ndiye alipiga kelele akiomba kufunguliwa maana milango ilikuwa imefungwa. Ndio baadaye waligundua kuna mauaji yamefanyika,” amesema.

Tukio hilo ni mwendelezo wa matukio ya mauaji mkoani Dodoma ambayo yamekuwa wakitokea katika siku za hivi karibuni. Mengine yamekuwa wakihusishwa na visasi.

Chanzo: mwananchi_official

Pia soma: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Na kwa Uzoefu wangu Tukuka GENTAMYCINE hapa kinachoonekana huyu Mama Marehemu alimbambikia Mume au Mwanaume wake Watoto na baadae Jamaa akaja kujua kuwa analea Mabao (Mbegu) za Mwanaume / Wanaume Mwingine / Wengine.

Wanawake wa Kitanzania narudia tena Kuwaambieni leo kuwa msipobadilika hasa katika Suala la Tamaa, Uwongo na Usaliti mtakufa mno kwani Wanaume wanaumia Kupambana kutafuta Hela ili wawatunze na nyie mnawafanya Madunduka (Wajinga) na Mapopoma (Wapumbavu)
 
Kulaumu wanaumr wamo lakini DNA aaaaaahhh. Wanaharamu Sana. Anyway jamaa kama story ninkweli hakupaswa kuwapatia adhabu hao viumbe wasio na hatia. All in all wanawake wanacheat Sana ndio maana wanahakikisha wanaume tunaendelea kujiita social father's kwanujinga wetu ila ukiwaambia tupime DNA mapema anaruka kimanga au lawama kibao oooh hauniamini blah blah
 
Umesikia sakata lililotokea huko Lamadi nasikia kuna hadi tuhuma ubakaji na uporaji zimefanywa na vijana wa utii wa sheria bila shuruti
 
Kusalitiwa kunauma sana. Mtu unaumiza kichwa upataje fedha ulee familia yako vizuri. Kumbe unalea watoto wasio wako!!???
Kwenye sheria ya ndoa tuonggeza kifungu kinachosema: ndoa hii Watoto watapimwa DNA au ndoa hii Watoto hawatapimwa DNA. Wnandoa waamue mapema cheti chanye kirai kipi watasain na kuchukua.
 
Hapo unaweza kukuta mwanamke anakwambia hv .....

"mwanaume mwenyewe huna huna uwezo wa kuzalisha wenzako wamegusa tu wamenipa mimba nimezaa watoto wangu ww huna watoto hapa......."

Hii kauli hata kama ulikuwa ni katekista lazima ubebe upanga
 
Back
Top Bottom