Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,616
- 13,301
Bismillahir Rahmanir Rahiim
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
WARAKA WA IDD ADH-HA 1445 - JUNI 17, 2024
UTANGULIZI
Awali ya yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutupa fadhila nyingi. Tunamuomba Azidi kuturehemu kwa hayo na mengine.
Kwa hakika ili tuishi kwa hadhi ya Binadamu kama Aliyotukusudia Aliyetuumba, tunahitaji uongozi bora. Hili ni hitajio kubwa la maisha ya binadamu tukiwemo Watanzania.
Kwa muktadha huo tunahitaji uongozi na serikali bora. Tunahitaji serikali ya namna hiyo iliyopatikana kwa ridhaa ya wananchi na inayo wajibika kwa watu wa taifa lake.
Serikali inayo tambua na kuheshimu uhuru wa watu wake katika nyanja zote za maisha. Serikali inayoheshimu sheria na mipaka ndani ya msonge wa Taifa.
MAISHA YETU
Kutokana na yale tulioyazungumza katika utangulizi tunaihitaji utawala unaoleta nafuu na maendeleo kwa watu wake. Moja ya vipimo vikubwa vya mafanikio ya utawala ni kuleta nafuu katika maisha ya watu.
Hapa kwetu Tanzania toka tupate uhuru (1961), sifa hiyo ni sawa na kusema imeshindikana. Sera za kila awamu yake kwa kiasi kikubwa zina zalisha matatizo na kurithishana matatizo hayo. Waathirika wakubwa wakiwa ni raia wa kawida.
Kwamfano unaweza kuona jinsi bei ya bidhaa muhimu zilivyo kuwa juu katika awamu moja na kuongezeka awamu inayofuata.
Awamu ya Tano: Unga wa Dona ulikuwa 1kg, Sh. 880.
Awamu ya Sita: Unga wa Dona ni 1kg, Sh. 920.
Awamu ya Tano: Unga wa Ngano ulikuwa 1kg, Sh. 920.
Awamu ya Sita: Unga wa Ngano sasa ni 1kg, Sh. 1,600.
Awamu ya Tano: Mchele ulikuwa 1kg, Sh. 1,500.
Awamu ya Sita: Mchele ni 1kg. Sh, 2,000.
Awamu ya Tano: Sukari ilikuwa1kg, Sh. 1,800.
Awamu ya Sita: Sukari sasa ni1kg, Sh. 3000.
Awamu ya Tano: Nyama ilikuwa 1kg, Sh. 7,000.
Awamu ya Sita: Nyama ni 1kg, Sh. 10,000.
Awamu ya Tano: Mbatata gunia 1, ilikuwa Sh. 70,000.
Awamu ya Sita: Mbatata gunia 1, sasa ni Sh. 120,000.
Awamu ya Tano: Mafuta ya kula lita 10, ilikuwa Sh. 35,000.
Awamu ya Sita: Mafuta ya kula lita 10, sasa ni Sh. 58,000.
Awamu ya Tano: Nyanya tenga 1, ilikuwa Sh. 12,000.
Awamu ya Sita: Nyanya tenga 1, sasa ni Sh. 36,000.
Awamu ya Tano: Vitunguu gunia 1, ilikuwa Sh. 50,000.
Awamu ya Sita: Vitunguu gunia1, sasa ni Sh. 100,000.
Awamu ya Tano: Saruji 50kg, ilikuwa Sh. 12,000.
Awamu ya Sita: Saruji 50kg, sasa ni Sh. 15,000.
Awamu ya Tano: Mafuta ya Dizeli, 1lt ilikuwa Sh. 2,350. Petroli 1lt ilikuwa Sh. 2,400.
Awamu ya Sita: Mafuta ya Dizeli, 1lt sasa ni Sh. 3,500. Petroli 1lt sasa niSh. 3,500.
Lingine ambalo huenda sambamba na hali hiyo ni viwango vikubwa vya kodi na idadi kubwa ya kodi katika vyanzo vya kawaida vya mapato ya raia. Lingine ni kodi hizo kuwa mrejesho duni sana wa huduma kwa wananchi hao.
Udhaifu wa sera zetu umejenga taifa tegemezi la mataifa mengine kiasi cha kuwa mtumwa wa madeni. Anaye beba mzigo wa madeni hayo ni huyo ambaye gharama zake za maisha zinapanda kila siku sambamba na mzigo mkubwa wa kodi.
Tunaambiwa 40% ya pato la taifa linatumika kulipa deni hilo. Kwa ufupi serikali zetu zimeshindwa kuleta nafuu kwa maisha ya watu, huku wananchi wakiwa hawaoni nia na uwezo wa serikali zao wa kutatua shida zao.
Hali hiyo imesababisha madhara mengi kama vile, njaa, ukosefu wa elimu, kushindwa kulipa gharama za matibabu, wizi, ujambazi, ukahaba kwa wanafunzi na mengine mengi.
USALAMA WA TAIFA
Taifa likifilisika Usalama wake na raia wake huwa hatarini. Moja ya sababu za kufilisika mataifa mengi hasa barani Afrika ni Ufisadi. Mataifa yaliyo salimika ni yale ambaye ndani ye serikali zao hamna mafisadi.
Tanzania inaonekana ufisadi ndani ya serikali si tatizo kubwa. Tunasema hivyo kwa sababu, Ripoti za Mkaguzi Mkuu wa mahesabu wa serikali (CAG), 2021, 2023, 2023, zimetaja mafisadi na ufisadi mkubwa waliotenda viongozi wa serikali lakini serikali haijachukua hatua dhidi yao.
Tarehe 22.04.2024, katika mkutano wa hadhara mjini Dodoma, ambao makamu wa Rais Dokta Philip Mpango, alikuwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda, alihoji kwanini watu hao hawajakamatwa. Makamu wa Rais alijibu kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati ya kushughulikia jambo hilo.
Majibu hayo yalikua ya kisiasa kwa sababu kwa mujibu wa mfumo wa sheria wa nchi, watuhumiwa wote wa ufisadi hushughulikiwa na Mahakama za Uhujumu Uchumi.
Wakati watuhumiwa wa ufisadi wa serikali wakipewa heshma ya kuogopwa, watuhumiwa raia wa kawaida, wao kwanza hupewa majina mabaya kama vile Panyarodi, majambazi na kadhalika kisha husakwa na kukamatwa na vyombo vya dola na baadhi yao hupigwa risasi hadharani na kuuwawa.
Nasaha zetu katika maadhimisho haya ya sikukuu ya Idd watu wote wachukuliwe sawa katika mizani ya sheria. Tunashauri watuhumiwa waliotajwa katika uchunguzi wa Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa serikali (CAG), na wengine, sheria ifanye kazi kama ilivyo kwa raia wa kawaida.
ONGEZEKO LA MADHARA KATIKA SHERIA
Tafiti zilizofanywa na wataalamu wa sheria zimeonesha katika mfumo wa sheria Tanzania kuna sheria nyingi dhidi ya haki na uhuru wa ubinadamu. Serikali imeshauriwa kuzifuta sheria hizo lakini imekataa kwa kutotekeleza ushauri huo.
Baya zaidi ni kuwepo na utungwaji wa sheria zenye matokeo ya kupoka uhuru na Haki kwa wananchi. Moja ya sheria hizo ni sheria ya Ugaidi. Sheria hii inaruhusu watu wa usalama kumuuwa raia bila ya kumfikisha Mahakamani.
Inaruhusu watu hao kumtuhumu raia na kuchukua mali yake (ukiwemo utajiri wake), bila kumfikisha Mahakamani. Inaruhusu Mahakama kumuhukumu raia adhabu ya kifungo chochote au kifo bila kumuona shahidi aliyethibitisha tuhuma dhidi yake Mahakani.
Sheria nyingine yenye mwelekeo wa kuondoa uhuru na haki kwa rai ni ile Na. 258/2023, ya vyama vya siasa. Sheria hii inamruhusu kiongozi wa serikali kufuta chama cha siasa chenye wanacha mamilioni bila ya wanchama hao kupata haki ya kujitetea.
Sheria hiyo iliyosheheni mambo mengi ya mfano hayo, imepingwa na asilimia kubwa ya makundi ya kijamii vikiwemo vyama vyama vya sheria na vya siasa.
Kuendele kuwepo kwa sheria za ukandamizaji katika mfumo wa sheria na kuongezwa kwa sheria za namna hiyo kuna madhara makubwa kwa watu na mfumo wenyewe wa sheria.
Kwa mfano Waislamu wamekua wakikamatwa kama Waislamu na kutiwa hatiani na sheria makhsusi (ya Ugaidi), kwa kiwango cha kuonesha Tanzania imetunga sheria elekezi kwaajili ya dini ya Kiislamu.
Moja ya vipengele vinavyokazia dhana hiyo ni pale Waislamu waposhinda shauri na kuachiwa huru na Mahakama, hawaruhusiwi kuondoka mikononi mwa vyombo vya dola ila kwa kudhaminiwa na ndugu zao. Dhamana hiyo huwa haifahamiki ni kwa tuhuma au shauri gani.
Mfano wa pili wa madhara ya utungwaji wa sheria zinazo ondoa uhuru na haki katika taifa letu ni mchakato wa uchaguzi wa kupata viongozi wa serikali za Mtaa, Vitongoji na Vijiji unaoendelea hivi sasa.
Bunge limefuta sheria inayoelekeza uchaguzi huo kusimamiwa na TAMISEMI. Katiba ya nchi imeelekeza uchaguzi huo usimamiwe na Tume ya Uchaguzi ya Taifa. Hata hivyo Tume hiyo haijapewa (kutungiwa), sheria inayowawezesha kusimamia uchaguzi huo.
Ikiwa uchaguzi utaendelea kwa mchakato mwingine wowote kinyume na Tume, bilashaka taifa litakua na viongozi wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji waliopatikana kinyume cha sheria.
Kwa ufupi katika mfumo wetu wa sheria kuna sheria nyingi zinazoondoa uhuru na haki kwa raia lakini tatizo kubwa zaidi ni watawala wetu kuwa na dhamira za kutunga sheria za namna hiyo na kuzilinda zile zilizopo.
Tunaishauri serikali yetu itimize ipasavyo ahadi zake ikiwemo ile ya maridhiano. Iheshimu na kutekeleza makubaliano ya vikao vya pamoja na makundi ya uwakilishi vilivyokwisha fanyika huko nyuma.
TUNAWATAKIA IDD NJEMA WATANZANIA WOTE