Shule za serikali kuagiza majembe, reki na makwanja kila mwaka huwa wanayapeleka wapi?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,304
4,592
Kila mwaka shule za Serikali huagiza wanafunzi wapya wanaoanza kujiunga na shule hizo kwenda na majembe, makwanja, reki, mafagio nk kama sehemu ya mahitaji ya vifaa vya kukamilisha wanaporipoti shuleni.

Swali langu ni kuwa huwa wanayapeleka wapi kila mwaka wanapokea mapya, angalau hata mafagio tunaweza sema wameyatumia yakaisha je, majembe reki na makwanja ambayo yanakuwa hayaishi kwa haraka maana ukizingatia matumizi ya usafi wa kupalilia shule tu hayawezi kuisha ndani ya miaka 2, 3 au 4 sasa kila mwaka wanayoagiza wanayapeleka wapi au ni mradi wa walimu pia?

Maana pamoja na kuletwa vipya kila mwaka ila unaweza kuta shule inaupungufu wa vifaa vya usafi mpaka unashangaa vimekwenda wapi?

Nadhani kutakuwa na ka mchezo kachafu kanafanywa na shule za Serikali kuhusu vifaa hivyo wanavyoagiza wanafunzi.
 
Kumbe Kuna shule za wakulima kwa maana mimi ni mtoto wa kishua shule nimesoma INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA ada kwa mwaka ni milioni 65. 😃😃😃😃
 
Watoto wenu huwa wanayaiba na kwenda kuyauza kwa mama ntilie,
Fundisheni watoto wenu waache wizi sio tu kutoa lawama kwa serikal na waalimu wakuu
 
Back
Top Bottom