Shule ya Lucky Vicent yafungwa, Lema afika kutoa pole

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Shule ya Lucky Vicent imefungwa kwa siku saba kufuatia vifo vya wanafunzi wake 32 vilivyotokea kwenye ajali ya gari jana Karatu.

Kutokana na ajali hiyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na wabunge wengine wa Chadema wamefika shuleni hapo kutoa pole.

Lema kwa niaba wabunge wameeleza kusikitishwa na msiba huu na amewapa pole wafiwa lakini akatoa angalizo kusiingizwe siasa katika msiba huu mkubwa.

Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro ameeleza kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako watafika jioni kuzungumza na wafiwa.

Kesho Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa niaba ya Rais John Magufuli ataongoza kazi kuaga miili ya wanafunzi hao Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mkuu wa shule hiyo, Ephraem Jackson hadi sasa vifo ni 36 na wanafunzi wawili bado wamelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Wanafunzi hao ni Sadiely Ismail na Wilson Tarimo.

Chanzo: Mwananchi
 
Huu ni msiba wa Taifa Viongozi tujiepushe na tofauti zenu za itikadi zenu msituletee kwenye huu msiba.

Sio kila kitu siasa tumepoteza Watoto wa kitanzania Watoto wadogo malaika hawa jamani MUNGU atusaidie tuwasitiri kila mmoja kwa imani yake kwa kadri MUNGU atakavyotupa nguvu hiyo kesho.

Sitegemei Viongozi kuonyesha tofauti zao ktk msiba huu haitapendeza kabisa.Malumbano ya Bungeni yabaki huko huko Bungeni
 
Atakayeleta siasa ni dhahir hayupo na sisi atafute nchi wanayofanya siasa wakati wa majonzi!!
 
Uyo n mshamba wa maisha yeye akl yake anazani kunenepa ndo afya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…