Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 528
- 1,254
Wakuu,
Niliweka uzi majuzi wa shimo lililokuwa linazidi kuchimbika kutokana na bomba kuwa na hitilafu na hivyo kutiririsha maji na kufanya ardhi eneo hilo kubonyea kirahisi na kuharibika (zaidi soma hapa: Serikali mnasubiri mpaka sehemu hii ya barabara iwe handaki? Ni kero kubwa kwa wakazi wa Mbezi Beach), tatizo hilo limeshughulikiwa baada ya DAWASA kutuma fundi wao na kuweka mambo yote vizuri. Angalia picha na kavideo kafupi hapa chini;
Hivi ndivyo palivyo sasa (kama haka kamvua kalipita na huko kutakuwa full uji sasa hivi)
Sasa kero yangu imebaki kwa TARURA, kama mnavyoona hapo kwenye picha Wakuu huo uji (tope) mpaka kule mwisho ni kamvua kaduchu tu kalinyesha juzi, pata picha imemwagika mvua ya maana hiyo changamoto yake tunapata wakazi wa maeneo haya.
Barabara ni mbovu kuanzia Makonde kule, kuja mpaka kwa Dr. Hiza mpaka hiki kipande kinachoedna kuunganika na sehemu ya lami inayotokea supermarket ya Shopaz. Chimba chimba ya DAWASA wengine wanasema ni Wachina imetuacha na njia mbovu sana. Maji yalikuwa hayatuami ovyo lakini sasa hivi kamvua kadogo tu ni kero kubwa.
TARURA, lini mtakuja kutuweka lami au zege wakazi wa Mbezi Mbeach, na nyie mnaosema tujitolee mtulie tuli, tunakatwa kodi kwanini huduma bado ni mbovu? Ukimpa fundi hela akushonee nguo yako akiharibu au kuchelewesha pesa yako utamkaba mpaka acheue pesa uliyomlipa, sasa kwanini tuache hawa ambao wanachukua pesa ndefu kutoka kwetu? Yaani tuhangaike wao wazivuje tu kirahisi hivyo?
TARURA tunasubiri majibu yenu.