Nimeitoa hii facebook group ya Kyela. Imeandikwa na George Mwakalinga. Inasikitisha sana.
Wandugu.
Leo nimeshutushwa sana na jinsi kijana wetu Siwale Chiristopher alivyosindikizwa mpaka kuzikwa kule kijijini Katumba.
Kila sehemu nimesoma watu wote wakiwaita hawa vijana mashujaa. Nilitegemea kabisa hata kusindikizwa kwao kwenda safari yao ya mwisho kungelikuwa na mwelekeo huo wa mashujaa wetu.
Lakini naongea na Katumba naambiwa hakukuwa na kiongozi yeyote wa wilaya. Wala hakukuwa na kiongozi yeyote wa mkoa. Kulikuwa na police tu kutokea Morogoro wakishirikiana na wenzao wa Kyela.
Rambi rambi zenyewe, ukiachia milioni moja aliyotoa mkuu wa police na laki tano aliyotoa mkuu wa police wa mkoa wa Morogoro ambazo zote wameambiwa zitaingizwa kwenye account ya mke wake, hakuna rambirambi yoyote nyingine ya maana kwa familia.
Familia ya huyu kijana ni wazee sana na ambao hawajiwezi. Walikuwa wanamtegemea kijana wao.
Hivi tunawatuma hawa vijana kwenye mapambano ambayo wanaweza kupoteza uhai wao. Wakifa tunashindwa kuwajali wao na familia zao. Tunategemea wawe na uzalendo gani? Kelele za mashujaa wetu hapo zina maana gani?
Mimi nimewashangaa mpaka hata Kyela FM. Nawauliza mlikuwa na program yoyote ya kushiriki kumsindikiza huyo kijana? Naambiwa hapana. Hata walioenda, walienda tu kwasababu ni kijana mwenzao wa Katumba.
Niwaambie ndugu zangu, huko nyuma wale mashujaa wetu kama waliofia Kagera vita na Idi Amin walikuwa mashujaa kweli kweli na kuzikwa kwao mkoa mzima ulikuwa unasimama. Mimi naona hapa Uingereza, police akifa akiwa kazini. Mazishi yake huwa hakuna hata sehemu ya kukanyaga. Kikubwa familia yake hukakikishiwa huduma zote. Juzi kuna askari aliyechomwa kisu na gaidi aliyeua watu kwa gari London. Watu wamechanga kulipia nyumba na kila kitu mpaka ada za watoto wake wakienda vyuoni.
Inakuwaje sisi tunaimba mashujaa wetu huku tunawaacha wenyewe wakati wa shida? Tunataka wafe wakitulinda huku wakifa tunatekeleza familia zao?
Kulikuwa na ugumu gani mkuu wa mkoa kushiriki mazishi ya huyu kijana? Kulikuwa na ugumu gani vipongozi wa wilaya kushiriki mazishi ya huyu kijana?
Mimi nashauri wote tusaidiane kuisaidia familia ya huyu kijana kupitia michango ,mbalimbali. Kama viongozi wamemtelekeza, sisi wananchi na ndugu zake hatuwezi kumtelekeza.
Kama umeguswa na kifo cha huyu kijana basi onyesha kuguswa kwako kwa kutoa mchango ili mzee wake angalau apate rambirambi anayostahili. Yule mzee ni mgonjwa na hana uwezo. Kapoteza mwanawe kisha anaambulia sh. kama elfu 50 zilizochangwa na wanakijiji wenzake. Hilo sio sawa kabisa.
Naomba tumtumie Maisha Ambangile, meneja wa Kyela FM ili kukusanya michango na kisha mtaamua nani wakaifikishe kwa familia.
Kijana mwenyewe ni huyu hapa chini. Anaitwa Siwale Christopher.
mheshimiwa Mwigulu, chukua hatua kuwasaidia hawa watoto wa maskini.