Shughuli ni pale unapogundua hujui kiingereza wala kiswahili

The Mastermind

Senior Member
Dec 3, 2012
107
50
wakati Nasoma Shahada yangu ya kwanza, tulitumia diski tepetevu, kicharazio, kirudufu, kinukuzi na kiteuzi. Ilikuwa nadra sana kukuta mwanafunzi anatumia nywila kwenye kipakatarishi. Hata vitu kama mdaki, diski mweko, mtaliga, kadi sakima na kadiwia/mkamimo havikuwepo kabisa. Ila kwa sasa mambo yamebadilika. Wanafunzi wanakula vibanzi na sharubati, wanapata mishiko haraka kutoka kiotomotela...wanatumia kadihela, Aaah mambo Saaaafi!


Shughuli ni pale unapogundua hujui kingereza wala kiswahili
 
Kiswahili kimeharibiwa kwa makusudi kabisa. Kinatolewa kabisa ladha ya matamshi.

Tanzania hakuna chema tulichokikuta ambacho hatujakiharibu kwa ujinga wa wachache.
 
Mtu akiongea kiswahili kama hicho sitapendana naye hata kidogo. Kiotomotela ndio nini! Diski tepetevu!! Kicharazio!!!
 
Tufunze Kiswahili basi kwa kutupa maana za hayo maneno!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…