Naamini kbs jamii forums ni gwiji wa ushauri ,,
Miaka kadhaa iliopita Nilikua Tanga kwa mapumziko kwasababu ndo nyumbani sasa ktk pitapita zangu nikakutana na kijana ambae tunafahamiana tukasalimiana pale lkn alivyoona simu yangu akaniuliza vp kaka simu yako INA WhatsApp nikamjibu ndio.
Akaniambia naomba kuna mtu niingize Namba yake nimcheki kaniambia yupo WhatsApp nawasiliana nae lkn sjawahi kumuona,,
Nikampa akaingiza namba akamuona Mara akamtumia msg lkn hakua online kwahio hakujibu
Nikamuuliza huyo mbona ni mtu mzima ni Nani wako akacheka tu hakunijibu,, basi akafuta namba akanipa sim yangu nikaondoka,
Yule mama alivyowasha data akakuta ule ujumbe akanipigia nikajaribu kumuelewesha ilivyokua
Tatizo likaanza hapo kila siku ananitumia sms za kunisifu kua mimi ni kijana mzuri na mambo kibao mimi nikawa simjibu ,
Akapiga nikapokea akaniuliza vp mbona hujibu sms zangu au huna vocha nikamjibu ndio akanitumia vocha 5000
Siku zilivyozidi kusonga mbele ndo tukazidi kuzoeana na akaniambia yeye yupo mkoani yani nimbali nauli kama 70000 nikitaka kwenda atanitumia,,, akaniambia nikiwa na shida nimuambie atanisaidia..
Siku moja nikamjaribu kua nina shida ya laki mbili akanitumia kwakweli sjaamini nikaenda kutoa fasta duh nikajua hapa nimempata .
Maisha yalienda hivyo kuhusu laki au laki mbili nilikua natumiwa. Na alidai ananipenda haswa na ni mtu mzima ana watoto wa tano
Mwezi uliopita nilimpigia simu nikamueleza shida yangu kua ninashida ya laki NNE akanitumia
Sasa hapo ndo shida ilipoanza kumbe ile pesa alichukua dukani kwa mume wake na mume wake mahesabu aliyaweka vzr ,,wiki iliopita akanipigia anataka nimrudishie ile hela nikamuambia sina kitu pesa yote nimemaliza labda nikutaftie au subiri mwisho wa mwezi akaniambia ukweli kua pesa alizokua ananitumia alikua anachukua dukani sasa safari hii imejulikana kwaio kamwambia mumewe kua kuna mtu kamkopesha kwahio sasa pesa ya watu inasubiriwa na tarehe ndo hizi zimefika ,,na usawa huu wa magu laki NNE ni ndefu jamani tangu Jana ananipigia na ukweli ni kua hatujawahi kuonana
Nipeni ushauri wadau nimpotezee au kwasababu pesa za kurudisha sina na imekua ghafla
Natumaini hamtanipotosha
Asanteni