Shirikisho la riadha Tanzania - RT latangaza kamati mbalimbali, yupo Ikangaa, Simbu na Gidabuday

Melubo Letema

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
413
410
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limetangaza Kamati mbalimbali kwa lengo la kuboresha utendaji wa shirikisho hilo.
Kamati hizo zimetangazwa na Rais wa RT, Silas Isangi, mbele ya waandishi wa habari jijini Mwanza, Mei 9.

Isangi, alisema Kamati hizo zimetangazwa kwa mujibu wa katiba ya shirikisho hilo na zitadumu kwa miaka miwili, 2023-2024.

Katika kamati hizo, kumesheheni magwiji wa taaluma mbalimbali, zikiwemo sheria, mawasiliano, fedha, uchumi, masoko, madaktari, wawakilishi wa wachezaji nk.

Kwenye kamati hizo, Kamati iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ni ya mabadiliko ya katiba, kutokana na kilio cha wadau wengi, ambapo Mkutano Mkuu wa RT ulioketi Novemba mwaka jana jijini Dodoma ilikazia, ambapo Rais Isangi, amemtangaza Wakili msomi Farida Jawewa kuwa Mwenyekiti huku Katibu wake akiwa ni Katibu wa zamani wa shirikisho hilo, Wilhelm Gidabuday.

Wajumbe ni Kanali mstaafu Juma Ikangaa, Allen Allex, Charles Maguzu kutoka BMT, Katibu Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha Rogart John Steven Akhwari, Mwenyekiti Riadha Morogoro Angelius Likwembe, Boniface Tamba, wawakilishi wa wachezaji Mariam Said na Alphonce Simbu.

Kamati ya Nidhamu inaundwa na Wakili msomi Baraka Sulus ambaye ni Mwenyekiti huku Katibu ni Catherine Nyamko ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Dar es Salaam huku Wajumbe ni Gidamis Shahanga, Allen Alex na Marcelina Gwandu.

IMG_1470.jpg

IMG_1465.jpg

IMG_1466.jpg

IMG_1467.jpg

IMG_1468.jpg

IMG_1464.jpg
 
Nakumbuka enzi za Nyambui ilikuwa Gidabuday akihojiwa basi ni kuponda uongozi wa Nyambui sasa sijui uko kwenye riadha kuna pesa
 
Chama cha riadha kinahitaji marekebisho makubwa sana. Haiwezekani pamoja na hizi marathon zilizotapakaa kila sehemu hapa Tanzania ila bado kimataifa majina ni yaleyale kila siku, Geay, Simbu, Failuna na Giniki.

Ni uwendawazimu nchi kuwakilishwa na wanariadha wanne tu wanaofanya vizuri. Mtu kama Geay kimataifa ni mkubwa kuliko mwanamichezo yeyote yule hapa Tanzania akiwemo Samatta lakini endorsements alizo nazo ni chache sana kulinganisha na jina lake.

Yule kijana tulitarajia hadi muda huu awe anapiga noti nyingi kwenye makampuni ila RT imelala haioni pesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom