peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,942
Richard Nzumbe mkazi wa mtaa wa Butengwa Manispaa ya Shinyanga amefariki dunia akidaiwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakati anaingia nyumbani kwake.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 1 usiku wakati akitoka kazini kwake alipofika nyumbani kwake ndipo alishambuliwa na watu hao wanaodaiwa kutaka kumpora fedha.
Akieleza undani wa tukio hilo leo Desemba 19, 2022 Shemeji wa marehemu, Salome Dady amesema majira ya saa 1 usiku walikuwa ndani yeye na watoto wa dada yake, ndipo waliposikia gari la shemeji yake likiwa limefika getini.
Amesema, mmoja wa mtoto alitoka nje kumlaki baba yake na ndipo aliposukumwa na watu hao waliomfuata marehemu kisha kumfanyia unyama huo.
"Mtoto wa dada alikwenda kufungua mlango ndipo nikasikia kelele nje ikabidi nitoke nikaone kuna nini nikakuta watu wawili wanampiga risasi shemeji ikabidi nichukue stuli nikampiga mmoja akaanguka, ndipo wakachukuana wakaondoka," amesema Salome Dady.
Naye Mwenyekiti wa mtaa wa Butengwa, Onesmo Mayenda akizungumzia tukio hilo, amesema majira ya saa 1 usiku alipewa taarifa na wakazi wa mtaa huo na alipofika eneo hilo alikuta washambuliaji hao wameshatoweka.
“Kwa kweli tukio hili ni la kikatili sana na tunalilaani kwa sababu majambazi hawa wametoa uhai wa mtu, ambapo ni kosa la jinai, hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi kuwakamata waliohusika,” amesema Mayenda.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Jeshi la polisi linaendelea na msako wa kina kuwabainisha waliohusika na tukio hilo.
Chanzo: Mwananchi