The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 296
- 545
Mwanaume anayejulikana kwa jina Peter Mayala (45) mkazi wa Kijiji cha Mwamagunguli, Manispaa ya Shinyanga, amejiua kwa kujinyonga ndani ya chumba chake cha kulala baada ya kujaribu kumuua mtoto wake wa kike anayeitwa Anna Peter (6) huku chanzo cha tukio kikidaiwa kuwa ni ugomvi wa familia kati yake na mke wake.
Mashuhuda wa tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo, wamesema mke wa marehemu alitoka kwenda kuwaita majirani na kuwaambia mume wake amemfukuza asilale chumbani na aliporudi na baadhi yao wakakuta mtoto wake wa kike anayeitwa Anna Peter amechinjwa na kisha mwanaume huyo kujinyonga kwa kamba hadi kufa.
Soma pia: Baba ajinyonga baada ya kumuua mwanaye
Aidha, majirani akiwemo Mwenyekiti wa kijiji hicho wamesema tukio hilo limewasikitisha kwa kuwa kijana huyo, alikuwa hana ugomvi na mtu yeyote mtaani na wala hawajawahi kusikia wana ugomvi ndani ya nyumba yao.