DOKEZO Shimo linalojazwa taka ni hatari kwa Wakazi wa Vijibweni - Dar es Salaam, Viongozi wa Mtaa wanachukulia poa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

MeVSMe

JF-Expert Member
Mar 25, 2024
270
425
Katika mizunguko yangu, nilipita katika eneo la Kigamboni, Kata ya Vijibweni, Mtaa wa Mkwajuni ambapo nilikutana na shimo kubwa lililozungukwa na makazi ya watu, eneo hilo ambalo limejaa takataka, linafanana na jalala lililoachwa wazi.


Kwa kuwa nilikuwa mgeni, nilidhani pengine ni sehemu iliyotengwa rasmi kwa ajili ya kutupia taka. Hata hivyo, nilipouliza baadhi ya wenyeji, walinieleza kuwa shimo hilo limekuwepo kwa miaka kadhaa, likizidi kutanuka na kuleta madhara kwa wakazi wa maeneo jirani.

Wakazi waliniambia kwamba, mvua zinaponyesha, shimo hili hujaa maji na kusababisha mafuriko yanayoingia katika nyumba zao, hali ambayo imefanya baadhi ya nyumba kulegea kwenye misingi, na baadhi kubomoka.

Nilipozungumza na wakazi wa eneo hilo kuhusu jinsi wanavyokabiliana na tatizo hili, walieleza kuwa baadhi yao wameamua kujenga upya misingi ya nyumba zao kwa kuimarisha kuta zinazozunguka nyumba ili kuzuia athari zitokazo na maji kutuama katika shimo hilo.

Wakazi walijaribu kuziba shimo hili kwa kutupa takataka ndani yake ili kuzuia mafuriko, lakini walikataliwa na serikali ya mtaa na halmashauri kwa madai kuwa kuweka takataka kwenye shimo hilo ni hatari kwa afya zao.

Kwa sababu ya tatizo hili kuwa kubwa, mnamo tarehe 9 mwezi wa 8, 2024 viongozi walikubaliana na Diwani wa kata hiyo kuleta vifusi ili kuziba shimo hilo kwa haraka iwezekanavyo. Wananchi walifurahi wakiamini kuwa suluhisho la kudumu limepatikana.

Wananchi wanasema walishtushwa baada ya siku kadhaa walipokuta pembezoni mwa shimo hilo kumejaa lundo la takataka badala ya vifusi walivyoahidiwa. Wakazi walipohoji kuhusu ujio wa takataka hizo, waliambiwa kuwa diwani alileta takataka hizo kwa ajili ya kujaza shimo.


Picha ikionesha takataka zilizomwagwa pembezoni mwa shimo

Wakazi wa Vijibweni wanasema wameshangazwa na hatua hiyo kwani awali waliambiwa kuwa kuweka takataka kwenye shimo ni hatari kwa afya, lakini sasa diwani ameamua kutupia takataka hizo akidai ni kwa ajili ya kuziba shimo hilo. Wananchi wanajiuliza, "Je, takataka hizi zilizoletwa na diwani si hatari kwa afya zetu?"

Katika uchunguzi wangu, nimebaini kuwa baada ya takataka kumwagwa, baadhi ya wananchi wamegeuza eneo hilo kuwa jalala rasmi, wakiamini kuwa ni rahisi kumwaga taka hapo kuliko kulipia gharama za magari ya kuzolea taka. Hali hii inazidi kuweka mazingira hatarishi kwa wakazi wa Vijibweni na kuongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa.


Kwa kuwa suala hili lilifikishwa kwa viongozi, nilimtafuta diwani wa eneo hilo ili kujua kwa nini ahadi ya kuleta vifusi na kuziba shimo haijatimizwa, na badala yake takataka ndizo zimewekwa. Diwani alinijibu kuwa anahitaji muda zaidi kulizungumzia suala hili kwa kina.

Wakazi wa eneo hili wanalalamikia sana uwepo wa shimo hili, hasa kwa sababu ya kuongezeka kwa mbu wanaoeneza malaria.

Ni kawaida kwa wakazi hao kwenda hospitali mara kwa mara kupima malaria kutokana na hofu ya kuambukizwa maradhi hayo. Ni wazi kuwa shimo hili limekuwa chanzo cha hatari kwa afya na maisha ya watu wa eneo hili.

Mimi kama mwananchi, natoa wito kwa uongozi wa Wilaya ya Kigamboni kuchukua hatua mara moja kushughulikia tatizo hili.

Afya na usalama wa Wananchi uko hatarini, na ni jukumu la viongozi kuhakikisha kuwa maisha ya watu hayapo kwenye hatari kama hii.

Je, Serikali iko tayari kuendelea kushuhudia madhara makubwa zaidi kwa wakazi wa Vijibweni?
 

Attachments

  • IMG_20241112_085542_304.jpg
    340.7 KB · Views: 6
Diwani WA Kata ya vijibweni ni Balaa, na nasikia bado anataka kugombea
 
Kama wameshapokea mshiko msitegemee wafanye kitu hapo.. Dawa pekee ni kuwatafuta NEMC
 
Kwanini waliwakataza wananchi kutupa taka? Lakini Diwani kazileta?
 
Kwa jina lingine Shimo la Udongo, hili shimo ni kubwa mno labda ni picha tu zina shindwa kuonyesha ila kiuhalisia kujaza hilo shimo ni story za kusadikika. Hakuna serikali wala mtu ana weza ingia garama za kujaza hilo shimo ni kubwa mno mno mno wanao fahamu lilipo wanaweza ongea ukweli hapa. Kinacho takiwa kuweka mikakati ya kuzuia takataka kuto tupwa humu ila lina tisha ni kubwa sana.
 
Sasa mdau Hilo Shimo, ukifuatilia limesababisha makazi ya watu yameharibika, na wamekataza kumwagwa taka, ni sawa! Lakini kwanini Diwani alete taka? Lakini hili suala kama linaathiri makazi ya watu, kwanini lisichukuliwe hatua????
 
Hili Shimo ni kubwa, ni vile tu picha haioneshi uhalisia vizuri, lakini ni Shimo refu na kubwa
 
Sasa mdau Hilo Shimo, ukifuatilia limesababisha makazi ya watu yameharibika, na wamekataza kumwagwa taka, ni sawa! Lakini kwanini Diwani alete taka? Lakini hili suala kama linaathiri makazi ya watu, kwanini lisichukuliwe hatua????
Mkuu na kuelewa sana Na Diwani wa eneo ni jirani yangu ni mtu janja janja sana, ukifwatilia historia ya hilo shimo makazi ya watu yamelikuta, lilikuwa lina chimbwa mchango miaka ya nyuma serikali ikaja sitisha zoezi baada ya watu kuanza hamia. maanake kwa lugha ya siasa ni kwamba makazi kuzunguka hilo shimo wamejenga shimo likiwepo je wali lazimishwa kujenga eneo hilo? Mbili diwani ana tumia ujinga na umbumbumbu wa watu waeneo lake kama mtaji, hii ni kwa kuwalaghai kuwa ata lijaza kitu ambacho ana juwa hawezi wala hiyo hela hana. So na ungana na wewe diwani ana zingua hataki sema ukweli kz tarehe za kupambania kiti zimekaribia ila ukwel kujaza hilo shimo hata Mama Samia hawezi kubali.
 
Je, ni zipi sababu za uwepo wa hilo korongo?

Njia ya asili ya maji?
Shughuli za kuchimba mchanga?
 
Heeee, hii kubwa aisee
 
Hili Shimo ni kubwa, ni vile tu picha haioneshi uhalisia vizuri, lakini ni Shimo refu na kubwa
Hapa na kuunga mkono Mkuu ila kiuhalisia unadhani lina weza kujazwa? Kz kwa maoni yangu Diwani ana danganya garama ya kujaza shimo lilikuwa lina chimbwa mchanga leo urudishe pawe flat uhalisia uko wapi? ahahaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…