Shikamoo Malaria, aiseeh! Sijawahi kuumwa hivi. Siku tatu kama mwaka.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
29,028
69,696
Mabibi na Mabwana hamjambo!

Pasaka iliisha vizuri Kabisa. Siku hiyo tulikutana ndugu wote maeneo ya Msasani beach Club.

Kama mnavyojua Taikon Hana gari, sasa ndugu zangu wale kidogo wengi wao walikuja na Magari Yao. Nami kujilizajiliza nipande Magari ya watu kidogo naonaga shida kidogo. Ni kweli ni ndugu zangu na wananipenda Sana. Hivyo kunipa lifti au hata kuniazima gari kwao sio tatizo. Tatizo lipo kwangu na mitazamo yangu. Sijajua mtazamo wangu ni mbaya au mzuri. Lakini angalau nipo comfortable nao.

Sasa bhana kama mjuavyo pasaka ya mwaka huu jiji la Dar lilikuwa na Mvua. Hivyo wakati wa kwenda Moto uliniwakia. Nikamkumbuka Binti Kimoso alivyonishinikiza ninunue gari. Oooh! Unatia aibu, oooh! Tunateseka hapa nyumbani tuu bure! Nikasema mmmh! Binti Kimoso yupo Sahihi hii ni shida Sana.

Kama mjuavyo asiye na gari asingoje mpaka mwisho wa shughuli/sherehe.
Nikasema hapa acha nitafute kaupenyo niwatoroke kimazingara.
Yaani hawakuniona nikija na hawataniona nikiondoka. Lakini shida yote ya nini hii lakini. Yaani Kisa gari tuu! Basi ndio hivyo.

Taikon nikawa nasoma rada na mwenendo wa program ili nipate upenyo. Hatimaye, program ya Muziki na kucheza. Nikasema hapahapa. Huyooooo!

Kisa hiko nimekisimulia nikiamini kinaujumbe kwa ambao wataamua kupata ujumbe.
Watu watafute pesa ili wawe comfortable.
Pili, unaweza ukawa na jina lakini usiwe na Pesa zinazolingana na jina Lako.
Hata hivyo ishu kubwa na tatizo kubwa la Taikon na watu aina yangu hatupendi kutiatia huruma. Tupo radhi tufe na tai shingoni. Hasara ya mtazamo huo ni unaweza kukosa Msaada ambao ungepatikana.

Nimerudi home nashangaa mwili wote unauma, viungo vinakatika. Heee! Nini tena.
Sijakaa Sawa kichwa nacho kinagonga. Nikamwambia shemeji yenu najihisi sipo Sawa.
Tukaenda usiku huohuo hospital, napimwa naambiwa ninamalaria ya Kufa Muda wowote. Mamaaa! KWELI. Sijakaa Sawa nahisi ubaridi Mkali unaingia mwilini. Nikajiambia Buriani Taikon kuzimu inakuita.
Najitania mwenyewe akilini hapo.

Tukarudi nyumbani ingawaje nilitamani nibebwe na ambulance. Nilikuwa nimechoka Sana. Nilikuwa Hoi. Ndio kwanza Nina masaa machache tangu ugonjwa unianze ila Moto unawaka.
Taikon Acha kudeka bhana! Wenzako wanaugua Miaka nenda Rudi wewe hata hajamaliza masaa 24 unalialia. Nikajiambia. Sasa itabidi nijikaze.

Usiku sikulala, chakula hakipanda, Maji hayashuki, Dawa kunywa zinapanda. Dadeki! Nakufa jamani! Nakufa! KWELI nikasema hapa nikileta Mchezo nitavuta hapa.

Sasa nikaanza kuwaza nitakavyokufa nini kitaendelea Duniani. Aaaa! Aaaahh! Machozi yakanitoka nilipomtazama mtoto wangu, nilipomuangalia Mke wangu, haaa! Mungu usinifanyie hivyo. Nikasema. Machozi yananitoka Mke anachanganyikiwa anahisi ugonjwa umekuwa Mkali Sana. Kumbe Mimi nawaza jinsi nikifa.

Sasa nitazikwa Wapi? Jamani! Jamani!
Ninakufa sijajipanga. Ninakufa sijajipanga. Nani atagharamia Usafiri wa mwili wangu upelekwe kwetu Makanya mahali nilipozaliwa. Sikutaka nikifa nizikwe Dar.
Mungu sijajipanga, usinifanyie hivyo.

Nikafikiri wee! Nikasema ugonjwa ukizidi Sana itabidi nimwambie Mke wangu nisafiri kurudi Makanya. Nikaugulie nyumbani. Huku agenda ya Siri ikiwa ikitokea nimekufa nisiwape watu usumbufu wa kusafirisha mwili wangu.

Ogopa unaumwa Mpaka unaona maruerue unaona watu waliovaa Kazi nyeupe wanakuja na kuzunguka kitanda chako alafu wanaondoka.

Kulala shida,kwani utaota mandoto Mabaya Sana. Ukiamka shida kwani unahisi maumivu. Sasa nifanyeje?

Sijui niandike Wosia, nikawa namtazama Mke wangu alivyomrembo, nikamkumbuka mdau wa JF aitwaye Nikifa MkeWangu Asiolewe au niandike Wosia kuwa nikifa mke wangu asiolewe.
Lakini nikakatazama kabinti kawatu, bado ni kadogo, hata Miaka thelasini hakajaikaribia. Nitakuwa nimekaonea.
Basi machozi ya Wivu yakaanza kunitoka.

Nimekufa zangu, Mke wangu namuona anaolewa tena kwa harusi kubwa.. amebebwa juujuu na lile limwanaume ambalo niliamua Niliite lijinga. Linamkiss mbele za watu kwenye hiyo harusi Yao.
Namwona Mke wangu Akiwa ameshanisahau na anafurahia mwanzo mpya katika mahusiano na ndoa mpya. Doooh!

Mungu usinifanyie hivi. Sitaki! Sitaki Kufa Mimi!
Basi nikisema hivyo kimoyomoyo wale watu wenye mavazi meupe wanakuja kwenye kitanda na kuanza kunisumbua,napiga makelele, Mke wangu anakuja kumbe yeye hawaoni. Nawaambia niacheni! Niacheni! Sitaki kwenda!
Basi hapo Mke wangu anajua safari imekwiva.

Sasa nikaingia huko mtandaoni sasa, ni masaa machache Tangazo la Kifo cha Taikon limetangazwa. Mtandaoni huko nikaona wengine wakilia, wengine wakinipost, wengine wakifurahia Kifo changu kwa Sababu hawakunipenda kutokana na Msimamo na mitazamo yangu.

Mungu usinifanyie hivi!

Ugonjwa umenipeleka kwa usiku mitatu. Hatimaye Mungu akasema Dogo amka Acha Mawazo ya kijinga.
Hutakufa.
Nikaamka zangu Leo nipo vizuri.

Nilipamiss Sana JF siku Tatu mfululizo kutokuwa JF kwangu sio kawaida.

Shikamoo Malaria

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
 
Pole sana ila nilikisubiri nikuulize wewe na Manfried ni ndugu ? Ni ID yako maana ameweka picha zako na za huyo shemeji hakika mmeendana ila nikataka kuuliza shemeji hana mdogo wake na mimi nioe mwenzio ?

Kubwa zaidi nashukuru kwa msaada wako ikiwa uliyewekwa kwenye picha ndiyo wewe basi tambua kuna askari mpumbavu katika kumbukumbu zako jitahidi kukumbuka na ujue ulinisaidia wewe dogo .

Pamoja sana aisee 🖐️
 
Manfred kwa kweli simfahamu na hiyo sio mara ya Kwanza kufanya hivyo. Ingawaje round hii kaweka picha. Nafikiri ni kijana anayenikubali.

Binti Kimoso hana ndugu wakike aliyebaki. Wote wameolewa

Kubwa zaidi nashukuru kwa msaada wako ikiwa uliyewekwa kwenye picha ndiyo wewe basi tambua kuna askari mpumbavu katika kumbukumbu zako jitahidi kukumbuka na ujue ulinisaidia wewe dogo .

Pamoja sana aisee 🖐️
Mmmh! Hatari Sana
 
Mabibi na Mabwana hamjambo!

Pasaka iliisha vizuri Kabisa. Siku hiyo tulikutana ndugu wote maeneo ya Msasani beach Club.

Kama mnavyojua Taikon Hana gari, sasa ndugu zangu wale kidogo wengi wao walikuja na Magari Yao. Nami kujilizajiliza nipande Magari ya watu kidogo naonaga shida kidogo. Ni kweli ni ndugu zangu na wananipenda Sana. Hivyo kunipa lifti au hata kuniazima gari kwao sio tatizo. Tatizo lipo kwangu na mitazamo yangu. Sijajua mtazamo wangu ni mbaya au mzuri. Lakini angalau nipo comfortable nao.

Sasa bhana kama mjuavyo pasaka ya mwaka huu jiji la Dar lilikuwa na Mvua. Hivyo wakati wa kwenda Moto uliniwakia. Nikamkumbuka Binti Kimoso alivyonishinikiza ninunue gari. Oooh! Unatia aibu, oooh! Tunateseka hapa nyumbani tuu bure! Nikasema mmmh! Binti Kimoso yupo Sahihi hii ni shida Sana.

Kama mjuavyo asiye na gari asingoje mpaka mwisho wa shughuli/sherehe.
Nikasema hapa acha nitafute kaupenyo niwatoroke kimazingara.
Yaani hawakuniona nikija na hawataniona nikiondoka. Lakini shida yote ya nini hii lakini. Yaani Kisa gari tuu! Basi ndio hivyo.

Taikon nikawa nasoma rada na mwenendo wa program ili nipate upenyo. Hatimaye, program ya Muziki na kucheza. Nikasema hapahapa. Huyooooo!

Kisa hiko nimekisimulia nikiamini kinaujumbe kwa ambao wataamua kupata ujumbe.
Watu watafute pesa ili wawe comfortable.
Pili, unaweza ukawa na jina lakini usiwe na Pesa zinazolingana na jina Lako.
Hata hivyo ishu kubwa na tatizo kubwa la Taikon na watu aina yangu hatupendi kutiatia huruma. Tupo radhi tufe na tai shingoni. Hasara ya mtazamo huo ni unaweza kukosa Msaada ambao ungepatikana.

Nimerudi home nashangaa mwili wote unauma, viungo vinakatika. Heee! Nini tena.
Sijakaa Sawa kichwa nacho kinagonga. Nikamwambia shemeji yenu najihisi sipo Sawa.
Tukaenda usiku huohuo hospital, napimwa naambiwa ninamalaria ya Kufa Muda wowote. Mamaaa! KWELI. Sijakaa Sawa nahisi ubaridi Mkali unaingia mwilini. Nikajiambia Buriani Taikon kuzimu inakuita.
Najitania mwenyewe akilini hapo.

Tukarudi nyumbani ingawaje nilitamani nibebwe na ambulance. Nilikuwa nimechoka Sana. Nilikuwa Hoi. Ndio kwanza Nina masaa machache tangu ugonjwa unianze ila Moto unawaka.
Taikon Acha kudeka bhana! Wenzako wanaugua Miaka nenda Rudi wewe hata hajamaliza masaa 24 unalialia. Nikajiambia. Sasa itabidi nijikaze.

Usiku sikulala, chakula hakipanda, Maji hayashuki, Dawa kunywa zinapanda. Dadeki! Nakufa jamani! Nakufa! KWELI nikasema hapa nikileta Mchezo nitavuta hapa.

Sasa nikaanza kuwaza nitakavyokufa nini kitaendelea Duniani. Aaaa! Aaaahh! Machozi yakanitoka nilipomtazama mtoto wangu, nilipomuangalia Mke wangu, haaa! Mungu usinifanyie hivyo. Nikasema. Machozi yananitoka Mke anachanganyikiwa anahisi ugonjwa umekuwa Mkali Sana. Kumbe Mimi nawaza jinsi nikifa.

Sasa nitazikwa Wapi? Jamani! Jamani!
Ninakufa sijajipanga. Ninakufa sijajipanga. Nani atagharamia Usafiri wa mwili wangu upelekwe kwetu Makanya mahali nilipozaliwa. Sikutaka nikifa nizikwe Dar.
Mungu sijajipanga, usinifanyie hivyo.

Nikafikiri wee! Nikasema ugonjwa ukizidi Sana itabidi nimwambie Mke wangu nisafiri kurudi Makanya. Nikaugulie nyumbani. Huku agenda ya Siri ikiwa ikitokea nimekufa nisiwape watu usumbufu wa kusafirisha mwili wangu.

Ogopa unaumwa Mpaka unaona maruerue unaona watu waliovaa Kazi nyeupe wanakuja na kuzunguka kitanda chako alafu wanaondoka.

Kulala shida,kwani utaota mandoto Mabaya Sana. Ukiamka shida kwani unahisi maumivu. Sasa nifanyeje?

Sijui niandike Wosia, nikawa namtazama Mke wangu alivyomrembo, nikamkumbuka mdau wa JF aitwaye Nikifa MkeWangu Asiolewe au niandike Wosia kuwa nikifa mke wangu asiolewe.
Lakini nikakatazama kabinti kawatu, bado ni kadogo, hata Miaka thelasini hakajaikaribia. Nitakuwa nimekaonea.
Basi machozi ya Wivu yakaanza kunitoka.

Nimekufa zangu, Mke wangu namuona anaolewa tena kwa harusi kubwa.. amebebwa juujuu na lile limwanaume ambalo niliamua Niliite lijinga. Linamkiss mbele za watu kwenye hiyo harusi Yao.
Namwona Mke wangu Akiwa ameshanisahau na anafurahia mwanzo mpya katika mahusiano na ndoa mpya. Doooh!

Mungu usinifanyie hivi. Sitaki! Sitaki Kufa Mimi!
Basi nikisema hivyo kimoyomoyo wale watu wenye mavazi meupe wanakuja kwenye kitanda na kuanza kunisumbua,napiga makelele, Mke wangu anakuja kumbe yeye hawaoni. Nawaambia niacheni! Niacheni! Sitaki kwenda!
Basi hapo Mke wangu anajua safari imekwiva.

Sasa nikaingia huko mtandaoni sasa, ni masaa machache Tangazo la Kifo cha Taikon limetangazwa. Mtandaoni huko nikaona wengine wakilia, wengine wakinipost, wengine wakifurahia Kifo changu kwa Sababu hawakunipenda kutokana na Msimamo na mitazamo yangu.

Mungu usinifanyie hivi!

Ugonjwa umenipeleka kwa usiku mitatu. Hatimaye Mungu akasema Dogo amka Acha Mawazo ya kijinga.
Hutakufa.
Nikaamka zangu Leo nipo vizuri.

Nilipamiss Sana JF siku Tatu mfululizo kutokuwa JF kwangu sio kawaida.

Shikamoo Malaria

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Marahaba mgonjwa
 
Ni zake mkuu kwani ulikuwaga humjui Robert..ni verified member
Basi ni litoto lidogo lenye manufaa makubwa kwa nchi yake .
Vipi mradi wetu wa kuku unaendaje kaka ?
Mbona mimi wakiatamia hawamalizi muda wanayakimbia mayai ?

Je pumba kwa wingi kumlisha mbuzi zinapelekea kuharisha kwa mbuzi ?

Nje ya topic ila nimekukamata hapa najua ukichomoka sikupati tena
 
Mkuu aisee hio changamoto hata Mimi kw sasa naipitia nadhani labda ni kaupepo sio kazuri..me wangu hata kutaga wamegoma kbs ila nahisi labda kwa sababu sijawapa pumba ile mchanganyiko nimefulia naishia KUWAPA mtama tu na vipumba kidogo..aisee wa kienyeji nimekuja kugundua faida yake ni kula nyama tu maana hata vifaranga vya miezi miwili ukiviona hadi huruma yaani vdg sana mkuu.mbuzi Sina uzoefu nao kbs bado sijajaribu..ila Nina sungura na njiwa na wenyewe bado wadogo hawajaanza kutaga
 
Back
Top Bottom