Shida ya maji yaanza tena kama ilivyo ada katika miezi hii ya September, October na November

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
14,364
53,814
Kama ilivyo kawaida, inapofika miezi ya 9, 10 na 11 Shida ya maji huwa kubwa katika jiji la Dar es salaam. Cha ajabu jili jambo lipo kwa miaka nenda rudi, lakini Serikali hii dhaifu ya CCM, isiyojielewa, iliyoshindwa kusolve ishu za msingi kama maji halafu inadhani bado ina legitimacy mbele ya macho ya wananchi bado inavimba na kuogea kwa kejeli eti "Wapinzani hawajakomaa"

Serikali dhaifu, isiyojielewa, kibogoyo ya CCM imeshindwa kwenye masuala ya huduma za msingi kama kupanga miji, nishati ya kupikia, umeme nafuu, barabara bora, shule bora. Yaani kila kitu chini ya serikali hii ya CCM ni kulipualipua tu hakuna ilichoweza kukifanikisha vizuri.

Vidara vya Serikali vimechoka, ukienda hata kwenye VYOO makazini huko kwenye idara za Serikali ni choka mbaya. Yaani hata kumaintain vyoo huko makazini wanafeli watawezaje kuendesha nchi?

Kiufupi tumekuwa ni kituko cha dunia. Miaka zaidi ya 60 ya kutawaliwa na CCM lakini CCM imeshindwa kusolve ishu ya maji safi na salama katika mji mkubwa kama Dar es salaam.

Huu ni ujinga, na Watanzania kubaki kimya wakati watu wanafuja mihela kwa kuzipeleka kwenye mambo yasiyo na tija ni ujinga zaidi.

LINI CCM iaweza kuwa na Tija, iweze kutatua masuala ya msingi kama maji kwa ufanisi?
 
Back
Top Bottom