Shida ni nchi ya kisekula kutengenezwa katika Ukristo na Uislam hili ni kosa kubwa lilifanyika na linaendelea kufanyika

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,683
14,051
Nitazidi kupiga kelele kadiri niwezavyo na kutoa tahadhari kadiri niwezavyo katika moja ya makosa yaliyo fanyika Tanzania ni kutengeneza nchi kimaandishi ya kisekula lakini kivitendo ni ya Ukristo na Uislam pekee.

Watanzania wanajipongeza kwamba ni nchi isiyo ya kidini lakini ni nchi iliyo tengenezwa katika mzunguko wa dini mbili hizi Ukristo na Uislam.

Ni nchi chache sana duniani zinazoweza kujitambulisha kama nchi zisizo egemea dini yoyote ile kwa namna yoyote ile na katika nchi hizo Tanzania haipo kabisa.

Kosa ni kuwa serikali bado inaendelea kuzishikilia hizi dini mbili na kuziaminisha kwamba ndizo nguzo ya nchi.

Kazi kubwa sana inahitajika kuiweka hii nchi mbali na udini wa Ukristo na Uislam kama vile Tanzania imejengwa katika mzunguko wao pekee.

Jamii ambayo asilimia kubwa ya population yake inayatazama maamuzi ya serikali katika picha ya Ukristo na Uislam ina tatizo kubwa sana la udini wa kila dini moja kupambana mamlaka dhidi ya nyenzake.

Jamii ambayo viongozi wake wanafanya maamuzi kwa kutazama hizi dini mbili juu ya maamuzi yake ina tatizo kubwa sana la udini ndani yake.

WATANZANIA WANAZIPENDA SANA DINI ZAO UKRISTO NA UISLAM MPAKA KUATHIRI FIKRA ZAO KATIKA KUFIKIRI NA KUTAZAMA MAMBO KIMAPANA NA WATANZANIA WANA UDINI WA UKRISTO NA UISLAM HATA KAMA HAWAPO TAYARI KUKUBALI HILO.
 
Nitazidi kupiga kelele kadiri niwezavyo na kutoa tahadhari kadiri niwezavyo katika moja ya makosa yaliyo fanyika Tanzania ni kutengeneza nchi kimaandishi ya kisekula lakini kivitendo ni ya Ukristo na Uislam pekee...
Kuna siku ukiristo utakuwa hauna nguvu tena tanzania...nakupa 30yrs later...ukiristo utakuwa minority group tz..kama ilivyo Nigeria
 
Sioni future ya ukiristo kabisa....muislim wanafanya best move, non returnable...kuna uwezekano hata next prezidar atakuwa shehe tena....na itakuwa ngumu kurudisha ukiristo madarakani
 
Kwa nini umeamua kulitazama suala la uongozi katika picha ya Ukristo na Uislam na mbio za kutwaa madaraka ?
 
Sioni future ya ukiristo kabisa....muislim wanafanya best move, non returnable...kuna uwezekano hata next prezidar atakuwa shehe tena....na itakuwa ngumu kurudisha ukiristo madarakani
Mbona unajiongelesha mwenyewe na tena vitu ambavyo havitakuja kutokea kabisa kabisa.
Kiufupi hiyo ni future impossible tense,nyie jidanganyeni misikitini lakini uhalisia hautakuja uwe hivyo.
 
Kuna siku ukiristo utakuwa hauna nguvu tena tanzania...nakupa 30yrs later...ukiristo utakuwa minority group tz..kama ilivyo Nigeria
Kwa nini unalitazama hivyo taifa katika picha ya Nigeria ?

Wewe ni mfuasi wa imani moja kati ya hizo mbili ?
 
"maaskofu wa madhehebu yote tumeungana kupinga DPW " ---+Askofu Mwamakula wa Moravian Uamsho.
 
Nitazidi kupiga kelele kadiri niwezavyo na kutoa tahadhari kadiri niwezavyo katika moja ya makosa yaliyo fanyika Tanzania ni kutengeneza nchi kimaandishi ya kisekula lakini kivitendo ni ya Ukristo na Uislam pekee.

Watanzania wanajipongeza kwamba ni nchi isiyo ya kidini lakini ni nchi iliyo tengenezwa katika mzunguko wa dini mbili hizi Ukristo na Uislam.

Ni nchi chache sana duniani zinazoweza kujitambulisha kama nchi zisizo egemea dini yoyote ile kwa namna yoyote ile na katika nchi hizo Tanzania haipo kabisa.

Kosa ni kuwa serikali bado inaendelea kuzishikilia hizi dini mbili na kuziaminisha kwamba ndizo nguzo ya nchi.

Kazi kubwa sana inahitajika kuiweka hii nchi mbali na udini wa Ukristo na Uislam kama vile Tanzania imejengwa katika mzunguko wao pekee.

Jamii ambayo asilimia kubwa ya population yake inayatazama maamuzi ya serikali katika picha ya Ukristo na Uislam ina tatizo kubwa sana la udini wa kila dini moja kupambana mamlaka dhidi ya nyenzake.

Jamii ambayo viongozi wake wanafanya maamuzi kwa kutazama hizi dini mbili juu ya maamuzi yake ina tatizo kubwa sana la udini ndani yake.

WATANZANIA WANAZIPENDA SANA DINI ZAO UKRISTO NA UISLAM MPAKA KUATHIRI FIKRA ZAO KATIKA KUFIKIRI NA KUTAZAMA MAMBO KIMAPANA NA WATANZANIA WANA UDINI WA UKRISTO NA UISLAM HATA KAMA HAWAPO TAYARI KUKUBALI HILO.

Ukiambiwa nchi bado inadhibitiwa na ukoloni mamboleo sababu mojawapo ni pamoja na hizo Dini ulizotoa.
 
Sioni future ya ukiristo kabisa....muislim wanafanya best move, non returnable...kuna uwezekano hata next prezidar atakuwa shehe tena....na itakuwa ngumu kurudisha ukiristo madarakani
Mmmm mi nazani unakitu kama imani kali lakini kwa ma division zero tunayoyaona toka miaka 20 iliyopita na bado yanaendelea ktk matokeo ya masomo watalaam wa fani mbalimbali wa dini ya kiislam watakuwa adimu sana, fuatilia hata matokeo mwaka huu.,labda watalaam wa dini ya kiislam watakuwa wengi after even 20 yrs
 
Kuna siku ukiristo utakuwa hauna nguvu tena tanzania...nakupa 30yrs later...ukiristo utakuwa minority group tz..kama ilivyo Nigeria
Indeed.. COURT ya Naijeria inasema kesi za watu kubadili Majina toka ya Kikristo kwenda ya kiislam zimeongezeka mara dufu kuliko miongo miwili iliyopita.
Inward Nigeria ni Jamhuri ya kiislam kwasasa.. Waislam ndiyo wanaamua mstakabali wa Naijeria.
Tinubu hakutaka MUSLIM - MUSLIM TICKETS ila wenye Nchi wakamgomea, ikabidi akubali,akamchukua Shetimma(BOKO HARAMA ENABLER) sasa wapi Ikulu.
Cheti chako kikiwa na jina la Peter kupata Ajira ni shughuli ni Bora Uende mahakamani ubadili ili uendane na mfumo.
 
Kwa Tanzania haitakaa ije itokee.
 
Ukristo na Uislam kwa Mtanzania ni sawasawa mtu azaliwe na mwiko (birth mark); hauwezi ukauepuka kwa Karne hii na kwa uhalisia ya historia tuliyopitia

Kitu gani kinaweza kuunganisha makabila mbalimbali kama sio Imani ya aina Moja illyojengwa kwa UTAMADUNI imara ambao uko uniform across makabila yote; bila hizo Imani mbili ilikuwa patashika mashati kuchanika; Kuna makabila yangekuwa Bado yanaendelea na tamaduni za ajabu ambazo usikute hata zingehatarisha "cohesion" ya taifa zima

Kwelii sikatai tamaduni na Imani hazikuwa zetu ila zimefanya kazi kuumba hili taifa lako la Sasa
 
Sioni future ya ukiristo kabisa....muislim wanafanya best move, non returnable...kuna uwezekano hata next prezidar atakuwa shehe tena....na itakuwa ngumu kurudisha ukiristo madarakani
Kwa taarifa yako kwa sasa watu wameanza kuamka kwenye hizo dini za kuletwa na majahazi. Jaribu kufuatilia vizuri vijana wengi wamebaki na majina ya kidini, huku wakishi maisha ya kisasa zaidi kwenye kutafuta hela, kuliko kuzifia dini. Nitajie dini inayotoa hela Hadi ivutie vijana zaidi ya kukaririshana mistari ya vitabu visivyo na ushahidi wa kisayansi.

Ni kweli waisilamu wanaweza kuwa wengi kuliko wakristo maana Bado wanaendekeza imani za kukaririshwa, lakini wasiofuata dini yoyote watakuwa wengi kuliko huo utapeli uitwao dini.
 
Back
Top Bottom