Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,805
- 13,574
Sheria hii inaweka masharti ya kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, kufuta Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, 1979 na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo.
Kwa mujibu wa Sheria hii, Mtu yeyote ambaye ni raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na nane na ambaye hajapoteza sifa chini ya Sheria hii au sheria nyingine yoyote, atastahili kuandikishwa kuwa mpiga kura chini ya masharti ya Sheria hii.
Kila unapofanyika uchaguzi wa Rais, kila chama cha siasa kilichosajiliwa na kinachokusudia kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa Tume jina la mgombea wa kiti cha Rais na jina la mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa chama hicho, atapaswa kudhaminiwa kwa maandishi na wadhamini walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa madhumuni ya uchaguzi chini ya Sheria hii wasiopungua mia mbili kwa kila mkoa, angalau kwa mikoa kumi ya Jamhuri ya Muungano, kati ya hiyo angalau mikoa miwili kutoka Tanzania Zanzibar.
Endapo kutakuwa na mgombea mmoja halali wa kiti cha Rais aliyeteuliwa, Tume itamtangaza mgombea huyo kuwa mgombea pekee wa kiti cha Rais. Mgombea wa kiti cha Rais aliyetangazwa chini ya kifungu kidogo cha (1) atapigiwa kura ya ndio au hapana na atakuwa amechaguliwa kihalali kuwa Rais endapo atapata kura nyingi zaidi ya kura zote halali zilizopigwa.
Endapo mgombea pekee wa kiti cha Rais atashindwa kupata kura nyingi zaidi kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (2), Tume itatangaza siku nyingine ya uteuzi kwa ajili ya uchaguzi wa Rais kwa notisi itakayochapishwa katika Gazeti la Serikali.