Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,474
- 1,163
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu kimesema kitaendelea kuwatetea na kuwasimamia wachimbaji wadogo ambao wanaonzisha migodi midogomidogo ili waweze kunufaika kutokana na kuanzisha maeneo hayo.
Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Shemsa Mohammed kwenye mwendelezo wa ziara ya Tarafa kwa Tarafa iliyofanyika katika Tarafa ya Nkololo na Dutwa wilayani Bariadi kwa lengo la kukiimarisha na kujenga Uhai wa Chama Cha Mapinduzi.
Ameeleza kuwa CCM ilishatoa maelekezo kwa Afisa madini kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakigundua migodi ya madini na endapo wataendelea kunyang’anywa maeneo yao, Chama na Serikali kitawasimamia kuhakikiha haki inapatikana.
‘’Maelekezo ya Chama na Serikali, walioanza kuchimba awali katika eneo husika wapewe kipaumbele…labda leseni iwe imeombwa miaka mingi iliyopita, na kama mmengundua na leseni ikapatikana baadae ni haki yenu kuchimba eneo hilo.
Aidha, Shemsa amewataka wananchi kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi na serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ili iendelee kutekeleza miradi na kuwaletea wananchi maendeleo ambapo fedha nyingi zimeletwa vijijini.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amewataka watumishi wa serikali kuendelea kutoa huduma bora katika sekta za Afya, Elimu, Maji na Umeme ili wananchi waone tija ya miradi inayoletwa na serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Shema ameendelea na ziara ya Tarafa kwa Tarafa kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi huku akiongea na Wenyeviti wa vijiji na vitongoji, wajumbe na mabalozi wa mashina na matawi pamoja na viongozi wa dini.
MWISHO.