Sheikh Ponda ‘asakwa'

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, bado anatafutwa na mawakili wa serikali. Mawakili hao wanapinga hukumu yake iliyotolewa na Richard Kabate, Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro mwaka jana ya kumfutia makosa ikiwemo la uchochezi.

Jana katika Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Jaji, Edson Mkasimongwa, Bernard Kongola ambaye ni Wakili Mkuu Mwandamizi wa Serikali amesema kuwa, Jamhuri inapinga hukumu hiyo. Mwaka 2013 Sheikh Ponda alishitakiwa kwa makosa matatu; la kwanza alidaiwa kuwaambia waumini wa Dini ya Kiislam kwamba, wasikubaliane na uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti zilizoanzishwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania kwa madai ni vibaraka wa CCM na serikali.

Shitaka la pili lilihusu kuwa, Sheikh Ponda aliwaambia Waislamu kwamba serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi hao ni Waislamu.

Shitaka la tatu alidaiwa kulitendwa tarehe 10 Agosti mwaka 2013 kuwa, kauli yake katika shitaka la pili inadaiwa kuumiza imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu namba 35 cha mwaka 2002.

Wakili Kongola amesema, uamuzi uliotolewa na Hakimu Kabate haukuzingatia uzito wa ushahidi wa Kielekroniki uliofikishwa mbele ya mahakama yake. Wakili Kongola amesema kuwa, hakimu alikosea aliposema kuwa hati ya mashitakaa ina upungufu kisheria na kuwa Shekh Ponda hakuwa na nia ya kuwashawishi waumini kufanya kosa.

Amesema kuwa, hakimu alikosea pale aliposema upande wa mashitka haukuthibitisha mashitaka mahakamani. Rufaa hiyo imepangwa kuanza kusilizwa rasmi tarehe 30 Juni mwaka huu. Mwishoni mwa Novemba mwaka jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ilimuachia huru Sheikh Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama hiyo kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Awali Bernard Kongola, Mwanasheria Kiongozi wa Serikali mbele ya Richard Kabate, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro alidai kuwa, tarehe10 Agosti mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa Ndege, Manispaa ya Morogoro, Sheikh Ponda alifanya uchochezi jambo lililosababisha kufunguliwa mashitaka hayo matatu.

Na kwamba, awali katika agizo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa tarehe 9 Mei mwaka 2010, Sheikh Ponda ndani ya mwaka mzima alitakiwa kuhubiri amani na kuwa raia mwema jambo ambalo alishindwa kulitekeleza.

Katika kesi yake Sheikh Ponda alikuwa akitetewa na wakili wake Juma Nassor
 
Sheikh Ponda ni Maskini sana sana Kiuchumi lakini kakataa ofa nyingi sana za Watawala na Taasisi zingine za kiserikali na wapinzani pamoja na kukataa kujishughulisha kwny Kamati zozote zinazohusu fedha misikitini na Baraza kuu ili kuepuka fitna ya kuchonganishwa na Waumini hali hii inawanyima raha sana watawala.

Huyu Mtu ni Miongoni mwa Watu ninaowakubali sana kwa kuweza kusimamia wanachokiamini kwa gharama yoyote na akisema Maandamano humkuti Serena wala kwny Press conference bali anakuwa mstari wa mbele. He works the talks
 
Mbona viongozi wa dini zingine wanaongea kauli nyingi mbaya za kichochezi na hawaandamwi kiasi hiki? Wengine huongea hata ktk radio lakn KIMYAAA..!!
KWANINI MASHEIKH TU. Kuna agenda gani nyuma ya pazia.?
Kuna utofauti kwenye hizi Kauli.. Hapo ndo matatizo yanapoanza
 
Sidhani kama Ponda ni maskini kama unavyo sema.
Mm nasikia anataasisi ya dini inayo miliki shule zaidi ya kumi zikiwemo ilala islamic ambazo zipo tatu moja mt arusha yapili mtaa lindi na yatu mt wa bungoni ambayo wiki mbili hivi iliunguwa moto karibia yote nahivi sasa ipo katika matengenezo.
Na sidhani kama unavyo sema kakataa kununuliwa hi ni dhana tu au humjui Ponda.
Kwanza nasikia shule nyingi za taasisi yake zinaunguwa moto mara kwa mara hapo ilala mbili zimeshaunguwa moto.
Chakushukuru hakuna madhara yalio tokea kwa wanafunzi na binaadam wengine.
Watu wanajiuliza kulikoni hizi shule za ponda zinaandamwa sana na janga la moto.
 

Kazi sio kusikia kazi ni kuthibitisha ulichosikia!

Kajifunze thamani ya "hear say" kisheria unaweza ukanielewa!
kumfahau Sheikh Ponda sihitaji kusoma gazeti, kusikia story kwy Jamii forums au kuambiwa na mtu yeyote ila pia nategemea uwepo wa Watu kama wewe! Kuna msemo unasema ukiona Mapambano yako hakuna anaepinga wala kukejeli na kuzua uzushi ujue hayo ni mapambano feki.
 
Ilala Islamic kuna ugomvi wa kwni shule ipo msikitini,pia hiyo taasisi aliyopo yeye yenye hizo shule nami nilikuwa humo ila sikuona alichokua ananufaika!
 
O
Hawa mawakili wa serikali ni mbwembwe tu,kazi kuvaa makoti tu hawana uwezo wowote,wanataka kuonekana kwa Magufuli kama wanaweza kazi lakini kiukweli Ponda amewachapa na makoti yao mbele ya pilato wao.
Jana nimeshuhudia jinsi wakili was serkali anavyobabaika mahakamani. Nimesikitika na kujiuliza sana iwapo kwa mwenendo huo serikali itashinda kesi muhimu. Nawashauri wajipange upya kwa kutumia mawakili wenye uelewa wa kutosha katika sheria.
 
Sina sababu ya kujifunza hear say na sina sababu ya kuamini kama ponda ni maskini wa kupindukia.
Kama mtu anataasisi inayomiki shule zaidi ya kumi nitakuwa mpuuzi kuamini kama mtu huyo ni maskini wa kupindukia.
Ndio maana nikakumbia hujamjua Ponda vizuri.
Na siamini kama hizo harakati zake ni kwa maslahi ya uislam na waislam.
Maskini wakupindukia wapo sio Ponda.
Alhamdulillah kwanza chakushukuru kwa allah ni pale alipo mruzuku Ponda ilmu na akili za kutosha kabisha.
Hizo sifa tu zinamtoa Ponda ktk umaskini wa kupindukia achili hivyo vitega uchumi vyake.
 
O

Jana nimeshuhudia jinsi wakili was serkali anavyobabaika mahakamani. Nimesikitika na kujiuliza sana iwapo kwa mwenendo huo serikali itashinda kesi muhimu. Nawashauri wajipange upya kwa kutumia mawakili wenye uelewa wa kutosha katika sheria.
Mahakama ipi?
 
O

Jana nimeshuhudia jinsi wakili was serkali anavyobabaika mahakamani. Nimesikitika na kujiuliza sana iwapo kwa mwenendo huo serikali itashinda kesi muhimu. Nawashauri wajipange upya kwa kutumia mawakili wenye uelewa wa kutosha katika sheria.
mkuu dawa ya hawa mawakili wa serikali ni kuwapa mikataba kwa deiwaka tu, hakuna kumwajiri wakili jumla inatakiwa serikali ikiwa na kesi inatafuta mawakili wanasimamia kesi wanalipwa chao habari inaisha. tatzo wanapoajiriwa wanabweteka mno hawajipi muda wa kujisomea na kupitia sheria mara kwa mara ndo maana wakikutana na mawakiri wakujitegemea wanagalagazwa mno hii hupelekea kuiingizia hasara kubwa kwa serikali.
 
Wanamchokonoa tu mzee wa watu kamaamua kupumzika wao wanalianzisha,akijibu iwe nongwaa nafikiri zipo kesi nyingine zenye masrahi mapana kwa taifa kuliko hiyo ya ponda,mfano kesi ya samaki wa magufuri,escrow,simbion wangekomaaa angalau hata na hizo kwanza.
 
Miaka ya mwanzo ya sabini kulikuwa na wimbo maarufu toka Unguja kibwagizo chake kikiimba hivi
"kumbe wewe ni yahudi adui wa dini yangu"
Mnahangaika bure na Ponda lengo lenu ni nini?
 
Ulichoandika ni uongo wa kutupwa,hizo shule si zake na wala hajihusishi nazo,mnafiki mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…