Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,204
- 7,231
SHEIKH DOGA AMEFARIKI DUNIA
Kutoka ukurasa wa Sheikh Ibrahim Ghulaam
إنا لله وإنا إليه راجعون
INNAA LILLAHI WAINNAA ILAYHI RAAJIUUN
Mmoja wa Masheikh Maarufu na bobezi mno katika fani ya Shariah Sheikh Muharram Juma Doga amefariki usiku wa kuamkia leo Jumanne na kuzikwa wakati wa Adhuhuri Temeke jijini Dar es salaam
Sheikh Doga ni katika Masheikh wacheche ambao wakikwenda kusoma masomo yao ya elimu ya juu lakini wakiwa tayari ni Masheikh wa kitegemewa
Masheikh kadhaa wa Afrika Mashariki waliosoma nchini Saudi Arabia hasa katika jijini la Madina walipata msaada mkubwa wa Sheikh Doga pale walipotatizika na baadhi ya Masuala ya kifiq'h au misamiati ya Kisharia
Sheikh Doga pamoja na upeo mkubwa wa kielimu aliokuwa nao alidhihirika kwa ukubwa wa kujishusha kwake
Kwa kipindi kirefu Sheikh Doga alikuwa akifundisha Shule ya Alharamaini iliopo mtaa Shauri moyo Kariakoo Dar es Salaam pia alikuwa na darsa katika Madrasat yake iliopo Temeke mtaa mmoja nyuma ya viwanja vya Maulid(Mwembe yanga)
Sheikh Doga pia amekuwa ndie Mwanyekiti wa Kurugenzi ya FAT'WA ya Umoja Wa Wanazuoni Wa Kiislaam Tanzania (Hay-atul Ulamaa)
Mchango wa Mwanachuoni huyu ni vigumu kupatikana Mwanachuoni atakae ushikilia kwa ukamilifu wake
Kuna mengi ya kusema ingawa kwa Sasa tusimamie hapo
Twamuomba Allah amkubalie juhudi na nitihada zake na amsamehe makosa na mapungufu yake na amuingize katika rehema na pepo yake tukufu aamiyn
اللهم اغفر له وارحمه واسكنه فسيح جناتك يارب العالمين